Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kauli na vitendo vya Mh. Simbachawene vinanipa matumaini kuwa huenda tatizo la police kuwa kero kwa wananchi likawa limepata ufumbuzi.
Katika kipindi hiki kifupi toka ameshika hatatamu, angalau tumesikia akikemea police kuendesha ukamataji usiozingatia sheria, mathalani police wanaokamata watu wakiwa wamevalia kininja, hawana vitambulisho n.k.
Ninapomsikia Mh. Waziri akikiri wazi kuwa wananchi wanaonekana kufurahia police wanapopata matatizo mathalani kufariki naona angalau tumeanza kuwa wakweli kwa hali halisi ilivyo.
Hata hivyo natamani tutafakari kwanini mahusiano ya police na wananchi yamefika hapa. Kwamaoni yangu, hata kama police hana maadili kwa kiwango gani, kama hakuna sheria kandamizi na mifumo legelege, police huyo atashindwa kuonea wananchi. Hapa ninamaanisha tunayomazingira yanayowezesha police kuonea wananchi ndio maana wanafanya hivyo.
Kwa mfano, hivi tunasababu gani ya kuwa na kosa la uzurulaji kwenye dunia ya leo? Ni muda gani kisheria mtu anatakiwa kuwa amelala? Lakini kwasababu tumeamua kukutwa unatembea bila kitambulisho itamtosha police kukukamata, basi police wakiishiwa hela, wataingia mtaani, watajikamatia watu wanaotembea bila vitambulisho, watawaweka mahabusu baada ya hapo hutoki mpaka utoe hela.
Sijui kama Mh. Waziri una taarifa, police wanaweza wakapita nyumba za kulala wageni, wakakusanya wageni kwakuwa hawana vitambulisho au majina yao hayapo kwenyevitabu kwenda kuwalaza mahabusu. Na hilo linapotokea utaratibu ni huohuo, hujatoa hela huachiwi. Sasa hii ni nchi ya namna gani? Katika mazingira haya wahanga wa haya matukio watawapenda police kweli?
Kwakifupi sana, imefika mahali ukiwa unaenda safari ndefu inabidi uchenji elfu tano tano za kutosha ili barabarani mambo yasiwe mengi. Vinginevyo utapata vyeti mpaka ukome. Police akikagua gari akakosa kosa, anaweza kukuandikia faini kwanini kadi yako ya gari haina muhuri wa mwanasheria!
Kwa maoni yangu nadhani imefika wakati police wapigwe marufuku kwenda kukamata mtu ambaye hakuna aliyemlalamikia. Makosa kama uzurulaji au kukutwa unakunywa bia baada ya saa sita usiku si dhani kama yanatija kwa sasa.
Mwisho ni muhimu kuwa na chombo cha kufuatilia na kusimamia watu wanaolundikwa mahabusu na police kama angalau kuna reasonable course. Hii angalau itafanya police waache kuzitumia mahabusu kama mapango ya ulanguzi badala yake zibaki kama sehemu mahsusi za kuhifadhia wahalifu wa kweli.
Tukifaulu kutatua malalamiko ya wananchi dhidi ya police huenda tukafuta nusu ya sababu za baadhi ya wananchi kuwa na hasira na chuki dhidi ya serikali yao.
View: https://vm.tiktok.com/ZMDrBrpWd/