Regia Mtema

Regia Mtema

Status
Not open for further replies.
Sidhani kama nimeelewa mada yako ni nini mkuu. Unajaribu kutuambia kwamba hukujua tangu umezaliwa hadi Leo kwamba mtu mlemavu anafikiri na kuongea kama wewe usiye mlemavu? Kama hivyo ndivyo basi nadhani tukujadili wewe.

Au unajaribu kutuambia kwamba regia alipewa fursa aliyo nayo kwa sababu Chadema walitaka kuonesha kwamba siyo wabaguzi? Kama hivyo ndivyo, unahitaji kuomba radhi kwa regia na Chadema.

Nikisema 1 + 1=2 sio lazima kila mtu akubali!
Unaweza sema 1+1=11 na ukaja na theory yako uka prove!

As a man think,so he is!
Hayo ndo yalikuwa kwenye moyo wako lakini mimi nimempongeza kwa maana wengi wa walemavu ambao nimebahatika kuwaona sio wapiganaji,....yawezekana ni kwa sababu ya ulemavu wao!

Lakini regia nilimfahamu kupitia jf,na kwa kuona avatar yake tu tena sikujua kama ni yeye kweli!
Pamoja na hayo yote,nilivo sikia anagombea ubunge nilifurahi sana na kusema "yes" we have women who can dare to go forward kama kina mdee!

Nilivo muona jana (na sio mimi tu),nikawa nimeongeza "credit katika sifa zangu kwake" kwamba pamoja na kuwa ni mlemavu,anaweza kufanya mambo makubwa na hata usiweze kujua kwamba ni mlemavu kabla ya kumuona!

That is it,na wewe umekuja kutoa lililo moyoni mwako pia,that's jf "where we dare to talk openly"
 
Mbona na wewe unatenda dhambi ile ile aliyotenda mwanzisha mada? Ukisema ni mwanamke wa shoka bado umembagua. Ushoka wake siyo kwa sababu ya jinsi yake bali kwa sababu ya uwezo wake. Vema ukisema ni mpiganaji wa shoka au ni mwanasiasa wa shoka.

Ukiitwa "mwanaume wa shoka" utakuwa umebaguliwa?
 
Mada yako haihusiani na siasa peleka kwenye jukwaa husika
kweli tabia haitibiki... dogo naona roho hwa inakuuma sana wenzako wakisifiwa, i thought you have grown up!! Pole sana
 
Namkubali sana Regia pia,ni kiongozi mwenye uchungu na watu wake,msikivu,mnyenyekevu na jasiri.

Nafurahi kuona amepambana kufika alipofika,anastahili na kweli ni mfano wa kuigwa na kinadada na kinamama.

Mungu azidi kumwinua,atuwakilishe vizuri na 2015 ashinde Kilombero awatumikie zaidi wananchi anaowapa kipaumbele.


Lazima ashinde am sure 2015,......zaidi ni kwa sasa kuwaonesha wananchi wake kwamba pamoja na kwamba hakushinda anaweza kuwatumikia na atakuwa ame wajengea imani zaidi
 
Regia keeep it up
walikuchakachua katika uchaguzi lakini leo upo hapo
Kilombero ni moja ya majimbo tajiri tanzania nikimaanisja bonde la kilombero na mto wake,mlimba na kihansi na pia reli ya uhuru imepita huko lakini bado wananchi wake hawajafaidika zaidi ya wageni tu
jitahidi uwaamshe hao ndugu zetu wandamba tujenge NewTz
 
what's the point?

Mwenye uwezo wa kuthubutu kupanda jukwaa?

Amesema nini, amefanya nini Mabibo au kokote?


Tasa,you are so literal mkuu and it wont help you coz am not going to tell you anything
 
Imenitokea kwamba binafsi namwamini sana Regia.
Sijawahi kukutana nae ana kwa ana, lakini nimeongea nae kwa simu mara kadha na kumwona kwenye kampeni kupitia tv na clips za you-tube jf. Ni dada ambae yuko committed sn na haamini ktk kushindwa.
Kama ataretain msimamo alio nao basi yeye ni potential ya pekee sn kwa cdm,makundi yote ya jamii, na taifa kwa jumla.
Mungu ambariki sana.
Ameolewa????
 
Binafsi namfahamu sana Regia.Regia ni kifaa cha aina yake,.She is courageous,very intelligent,ambitious na ziadi ya yote ni mwadada mvumilivu sana.Ni mchapa kazi,mwenye upendo,mtoaji,asiyekubali kushindwa.Ni mpenda haki,mwadilifu,mwaminifu katika mambo yote.Ni mcha MUNGU.

She is independent woman.Anachukia utegemezi.
 
Pole sana Shy.Nahisi hukuwa na nia mbaya ila ndio hivyo tena umegusa kipenzi cha watu.Pole sana siku nyingine soma alama za nyakati.Pole and take it easy.
 
Akina dada mnapaswa kuiga moyo na ujasiri wa mh mbunge Regia

Nina imani wale wadada machachari na cv zao humu waliopo ndani na nje ya nchi hii wakijitokeza kuwania ubunge wa kuchaguliuwa na hata viti maalum nina hakikia watashinda kwa 100%

Msiache nafasi zenu kuchukuliwa na waimba bongo flavour,taarabu,watangazaji na wale vimada wa wakulu

Hongera Regia umeonyesha njia nina hakika 2015 tutapata wengi kutoka humu wimbledon!

ahsante kwa kutupa moyo.
Tutatangaza tu nia, ngoja tuendelee kujifunza kwa regia.
 
Ameolewa????

Hivi angekuwa sio mmbunge ungeuliza hili swali?

Regia Mungu akubariki ubakie ulivyo( mwenye upendo, usikivu, heshim,ukarimu, uadilifu na ucha Mungu)
nakuahidi sala zangu Mungu akulinde na akubariki ktk adma yako ya kutumikia wananchi.
 
Ila mhakikishe hamna skendo za ngono na mahusiano, ni hilo tu huwa linawaweka kwenye wakati mgumu.

kaka usiwakatishe tamaa,hizo kila mtu huwa nazo ila huwa zinatumika vibaya na mpinzani wako akiishiwa hoja na sera
mahusiano ni dept nyingine kabisa
unakumbuka ya akina Zuma ,clinton na wengineo?
 
Nawashukuru wote kwa comments zenu.Nimezipokea kwa mikono miwili.

Ila kwa bahati mbaya comments zote ziko upande wa positive tu,nahitaji pia na zile nyingine ili niumbike upya.I like both positive and negative criticism ili wakati mwingine nijue na mapungufu yangu.Naona wanaonifahamu wamefagia tu. Tunajengana.

Aluta Continua
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom