Regina Ndege akabidhi mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Nangara

Regina Ndege akabidhi mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Nangara

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Regina Ndege Qwaray, amekabidhi msaada wa mifuko 30 ya saruji yenye thamani ya shilingi laki sita kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa ofisi ya chama hicho katika Kata ya Nangara.

Soma: Naibu Waziri Utumishi, Regina Ndege: Kwasasa ajira ni za ushindani na kigezo cha uzoefu hakipo

Regina ameeleza kuwa alipokea barua ya maombi kutoka kwa Mwenyekiti wa kata hiyo na kuamua kujitolea ili kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo. Katika ziara zake hivi karibuni, amekuwa akichangia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo shule na hospitali katika maeneo ya Kiteto, Galapo, na Dareda, na safari hii amefarijika kufika kusaidia mradi wa chama chake.

 
Back
Top Bottom