Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Rehema.Pole mzee Mwakangale na familia yote na wajukuu wote wa Mzee John Mwakangale (Mwenyekiti wa zamani wa CCM-Mbeya). Steven popote ulipo nakupa pole sana katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na binamu yako.
P.I.P Rehema. Mungu awape faraja familia ya Mwakangale. Binafsi nilivutiwa sana na kazi yake ya utangazaji kwa lugha fasaha na tabasamu juu. Binadamu tu mavumbi na mavumbini tutarudi.
Msiba upo sinza karibu na sinza delux hotel kwa watakaoweza kuhudhuria,mwenyezi mungu mwema akukumbatia katika mikono yake na akupumzishe kutokana na shida zote ulizopata hapa duniani
Inauma sana, kweli vizuri havidumu, REHEMA hakuwa na majivuno kabisa kama ilivyo kwa wasichana wengine walio maarufu, alisalimia kila mtu mtaani hata watoto, yeye kwake ni tabasamu tu muda wote!! aliwapenda watoto sana!! basi tena bwana ametwaa jina lake libalikiwe.
Nasi tujiandae kwa safari ambayo hatujui muda wala saa.