Jamani kabla hatujamtukuza Mungu KWA KAZI YAKE KAMILIFU ni vyema tukajiuliza maswali.
Mwenzetu alikuwa anasumbuliwa na nini? aliugua kwa kipindi gani? Ingewezekana juhudi za kibinadamu kuuokoa uzima wake? Ofcourse haya maswali hayamrudishi mpendwa wetu. LAKINI itasaidia hata sisi tuliobaki hai. Kama amekufa gafla kwa ugonjwa aliokuwa hajui kama anao..basi watu tujue ....na tuweke mkazo wa kupima afya zetu mara kwa mara.....kama ni uzembe/umaskini wa hospitali zetu tujue..tupate maswali ya kuwapa wabunge wetu waikoromee serikali nk...
WANDUGU lets be real hawa ni vijana ambao ndo taifa letu linawategemea. They are fully of life and creativity. Unajua mtu kuondoka in her 30s kweli inauma sana! si kwa wazazi tuu..hata sisi wananchi.. Huyu dada hata ungemuona kwenye TV anatangaza ungejua kabisa ni dada anayejua analolifanya. Her best days were still ahead of her.
Ni vyema, tukawa tunajiuliza matatizo yanayowakumba wananchi wenzetu..je chanzo ni nini? na ni vipi vifo kama hivi vinaweza kuepukika? Haitoshi kusema ni mapenzi ya Mungu...we have to do more.. Leo dereva anaendesha gari kwa uzembe anasababisha ajali ya watu hamsini wote wanakufa..lakini hakuna anayeuliza hard question..wote...ni msemo ule ule.."mipango ya Mungu" really? Leo tunamzika Albino..aliyeuawa kikatili..msemo ni ule ule..ni "mapenzi ya Mungu" NADHANI HUYU MUNGU tunamsingizia mengine.
Uhai wa mtu uthaminiwe. na Kuuthamini ni kuuliza matatizo kama haya kusudi kama ni juhudi kufanyika next time..watu wajitahidi. Kama ni malaria..watu wajue namna ya kukabiliana na mbu. nk... Tuache kuchanganya imani zetu na vitu ambavyo hakika vinaepukika. Jiulize huyu dada kama ndo lets say kaolewa juzi juzi (simjui kiundani)..ameacha mme na mtoto..hii yote ni hasara tupu...mtoto atakuwa yatima..bwana atakuwa mjane nk...
RIP Rehema! You were an incredible girl full of life and energy!
Raha ya Milele umpatie ee bwana, Mwanga wa milele umwangazie.