Mkuu dunia inabadilika. Liberals nao kwa kipindi kirefu wame-overreach ndio maana huko West sasa watu wengi wanatamani conservatives warejee kupunguza speed ya liberals na "kuokoa" wanachoona kama kuvuruga kabisa identity na mpangilio wa maadili na nidhamu katika nchi zao.
Yaani safari hii masuala ya "utamaduni" yamekuwa na umuhimu mkubwa kuliko ya uchumi.
Ndio maana watu kama Trump wanapewa nafasi ya kusikilizwa hata wakiongea uongo, upuuzi na ujinga wa kila aina na hata kutamani udikteta kama wa Putin, Kim Jong Un, Victor Orban, n.k.
Inasikitisha lakini ndio uhalisia. Demokrasia imeanza kuchokwa sababu ya liberals kuzidi kuvuka mipaka.