Jeff Gemo
Member
- Jul 11, 2015
- 34
- 26
1. UBINGWA KOMBE LA KAGAME
Licha ya Yanga kujivunia rekodi ya kutwaa taji la Kagame nje ya Dar es Salaam, Simba ndiyo vinara wa kulitwaa taji hilo nchini. Simba imewahi kulitwaa taji hilo la Kagame mara sita na kuwa timu ya Bara yenye historia ya kulitwaa zaidi kombe hilo kuliko timu nyingine yoyote.
Mbali na kuwa timu ya Bara iliyotwaa taji hilo mara nyingi, Simba ndiyo timu inayoongoza kwa kutwaa Kombe la Kagame kwenye historia ya michuano hiyo na kuzipiku timu zote za ukanda huo.
2. FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO (CONFEDERATION CUP).. ambalo Yanga anagawa mipointi nje na ndani
Wekundu wa Msimbazi ndiyo timu pekee ya Tanzania iliyofanikiwa kucheza fainali za Kombe la Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika yaani CAF. Ilikuwa mwaka 1993 wakati huo likijulikana kama Kombe la Caf.
Simba ilicheza fainali hiyo na Stella Abidjan ya Ivory Coast na kutoka sare katika mchezo wa awali kabla ya kukubali kipigo cha mabao 2- 0 katika marudiano jijini Dar es Salaam.
Licha ya Simba kupoteza mchezo huo ambapo wachezaji wake waliahidiwa zawadi za magari kama wangeshinda, inasalia kuwa timu pekee kutoka Tanzania Bara iliyofanikiwa kucheza hatua hiyo ya fainali hizo.
3. NUSU FAINALI CLUB BINGWA AFRIKA (CHAMPIONS LEAGUE) ambalo Yanga huwa anatolewa siku ya ufunguzi asubuhi na mapema.
Historia ya klabu ya Simba inavutia! Ndivyo unavyoweza kusema kwa lugha rahisi baada ya timu hiyo kufanikiwa kucheza nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1974.
Hata hivyo iliondolewa katika hatua hiyo ya nusu fainali na klabu ya Mehala El Kubra ya Misri na kuzima ndoto za kucheza fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi katika bara la Afrika.
Rekodi hiyo ya Simba bado haijavunjwa mpaka leo hii ni timu yoyote ya Tanzania, japo mwenendo wake kwa sasa unaonekana kuwaghafilisha wanazi wengi wa timu hiyo.
4. KUWANG'OA MASHINDANONI KIKATILI SANA, MABINGWA WATETEZI AFRIKA, tena Waarabu wa Misri, Zamalek (waarabu hawataki hata kusikia jina la Simba maana kwao lina maana ya kifo)
Mbali na rekodi tajwa hapo juu ambazo huenda zikazidi kuchagiza machungu kwa mashabiki wa timu hiyo. Simba SC bado inajivunia rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kufanikiwa kuiondosha timu ya Misri katika michuano ya Afrika.
Wanaume hawa walifanya hivyo mwaka 2003 baada ya kuifunga Zamalek ya Misri ambayo ilikuwa inatetea ubingwa huo.
Pengine ninaweza nikawa nimewaudhi mashabiki na wafuasi wengi wa klabu ya Simba kwa maelezo hayo machache kuhusu klabu ya Simba. Lakini siku zote ukweli huwa haujifichi.
Ni kweli rekodi na takwimu hizi tamu zinaifanya Simba ibaki kuwa na historia nzuri na ya kuvutia kimataifa, rekodi ambayo Yanga wanaweza kutumia miaka kama 50 kuifikia.
Msumba anatoa wito kwa viongozi husika kuhakikisha kuwa wanafanya usajili wenye tija zaidi kwa lengo la kukiboresha kikosi chao na hata kuweza kuirudisha heshima ya timu hiyo, heshima ambayo kwa sasa imeonekana kupungua.
Kwa nijuavyo mimi, hakuna linaloshindikana chini ya Jua. “Ni kweli imebaki historia! Ngoja tuusubiri msimu mpya wa Ligi huenda ikaja kivingine.
Author : Issack Msumba
Publisher: Issack Msumba
Unauthorized Distributor :
Jeff Gemo Mnyama Machine
The One Man Army
Affirmative Gemo The Great
Simba Soldier, Nguvu Moja
THE TOUGHEST.