Rekodi nyingine bandari ya Mtwara: Meli kubwa kutoka Uholanzi yatia nanga tayari kusafirishia shehena ya Makaa ya Mawe

Rekodi nyingine bandari ya Mtwara: Meli kubwa kutoka Uholanzi yatia nanga tayari kusafirishia shehena ya Makaa ya Mawe

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Chini ya wiki 2, Bandari ya Mtwara imeweka rekodi mpya kwa kupokea meli kubwa yenye uwezo wa kubeba Tani elfu 60 za Makaa ya Mawe.(60,000).

Meli hiyo imetia nanga tayari kupakia Makaa ya Mawe kutoka kampuni ya Mwekezaji mzawa Ruvuma Coal Mining Limited.

Hii ni baada ya Meli nyingine ya Uswisa kuondoka kwa wiki iliyopita.

Safi Sana kwa sasa tumepata soko jingine la Makaa ya Mawe barani Ulaya 👇

=========

MELI ya MV EGT Southern Cross inatarajia kusafirisha kiasi cha tani 59,960 za makaa ya mawe kupitia Bandari ya Mtwara kwenda Amsterdam nchini Uholanzi.

Inaelezwa kuwa shehena hiyo ni kubwa zaidi ya makaa ya mawe kusafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara.

Akizungumza mjini hapa leo (Jumatatu) kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano, Nicodemus Mushi amesema usafirishaji wa shehena hiyo kubwa kwenda barani Ulaya ni hatua muhimu ya kulifikia soko kubwa la Bara la Ulaya baada ya bidhaa hiyo baada ya lile ya Asia.

Akifafanua zaidi Mushi alisema mara ya mwisho bandari hiyo kusafirisha shehena kubwa zaidi ilikuwa ni tani 59,815.

"Hii ndio mara ya kwanza kwa shehena kutoka Bandari ya Mtwara kwenda Bara la Ulaya moja kwa moja," alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Mushi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza alisema, Serikali ya Mkoa wa Mtwara inaridhishwa na utendaji wa TPA na Bandari ya Mtwara hasa katika kutafuta wateja.

Alisema uwekezaji wa Serikali mkoani Mtwara ni mkubwa, ikiwemo Ujenzi wa gati ambao umegharimu Shilingi Bilioni 157.8.

Aidha aliongeza kuwa Serikali imeiwezesha TPA kununua vitendea kazi na kuboresha mazingira ya kufanya kazi hivyo kuna kila sababu ya kuunga mkono jitihada hizi za TPA.

"...Ili kupata wateja zaidi na sasa mwelekeo uwe katika nchi jirani ya Comoro ambayo ina fursa kubwa ya kufanya biashara na Tanzania.
Kwa kushirikiana na Kampuni ya Ruvuma Coal tunaendelea kutafuta masoko zaidi ili kuufanya uwekezaji wa Serikali katika Bandari ya Mtwara kuwa na tija," alisema Brigedia Jenerali Gaguti.

Chanzo: HabariLeo
 
Attachments

  • Screenshot_20220531-134137.png
    Screenshot_20220531-134137.png
    129.1 KB · Views: 37
  • Screenshot_20220531-134325.png
    Screenshot_20220531-134325.png
    149.6 KB · Views: 37
Chini ya wiki 2, Bandari ya Mtwara imeweka rekodi mpya kwa kupokea meli kubwa yenye uwezo wa kubeba Tani mil.60 za Makaa ya Mawe.

Meli hiyo imetia nanga tayari kupakia Makaa ya Mawe kutoka kampuni ya Mwekezaji mzawa Ruvuma Coal Mining Limited.

Hii ni baada ya Meli nyingine ya Uswisa kuondoka kwa wiki iliyopita.

Safi Sana kwa sasa tumepata soko jingine la Makaa ya Mawe barani Ulaya 👇

View attachment 2245402
Ni muda muafaka sasa tufute tozo za miamala kwasababu fedha zinaingia huko kwenye makaa ya mawe.
 
Chini ya wiki 2, Bandari ya Mtwara imeweka rekodi mpya kwa kupokea meli kubwa yenye uwezo wa kubeba Tani mil.60 za Makaa ya Mawe.

Meli hiyo imetia nanga tayari kupakia Makaa ya Mawe kutoka kampuni ya Mwekezaji mzawa Ruvuma Coal Mining Limited.

Hii ni baada ya Meli nyingine ya Uswisa kuondoka kwa wiki iliyopita.

Safi Sana kwa sasa tumepata soko jingine la Makaa ya Mawe barani Ulaya [emoji116]

View attachment 2245402
Sawa. Lakini hii tani milioni 60 uliyoisema ni sahihi au typing error?

[emoji116][emoji116][emoji116]

Chini ya wiki 2, Bandari ya Mtwara imeweka rekodi mpya kwa kupokea meli kubwa yenye uwezo wa kubeba Tani mil.60 za Makaa ya Mawe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tani milioni 60 unazielewa barabara, anyway ni jambo jema ikiwa mabeberu wanaendelea kutumia makaa ya mawe huku wakitupiga madongo kwenye mradi wa bomba la mafuta kwamba unachafua mazingira. Hapo ndo utajua namna beberu alivyo mnafiki..........
 
Makaa yana Kazi nyingi Sana,pili technology zimebadilika
 
Washenzi watafurahi kuona rasilmali zinaenda kwa wazungu..badala ya kupambana wazungu wawekeze teknolojia na viwanda ili hayo makaa ya mawe yatumike kwaajili ya manufaa ya nchi na kwa kuwapa ajira watu wetu.

Mbaya zaidi hawajui bei gani yameuzwa na nchi imejipatia kiasi gani cha pesa kwenye hayo makaa ya mawe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Makaa yana Kazi nyingi Sana,pili technology zimebadilika
Kwani mafuta hayana kazi nyingi na huko teknolojia hazijabadilika?........unaanzaje kupinga mradi mmoja wa bomba la mafuta wakati kuna mamilioni ya project za kuzalisha mafuta duniani na dunia bado inatumia nishati ya gesi na mafuta kwa kiwango kikubwa..........unafiki wa beberu upo palepale.
 
Washenzi watafurahi kuona rasilmali zinaenda kwa wazungu..badala ya kupambana wazungu wawekeze teknolojia na viwanda ili hayo makaa ya mawe yatumike kwaajili ya manufaa ya nchi na kwa kuwapa ajira watu wetu.

Mbaya zaidi hawajui bei gani yameuzwa na nchi imejipatia kiasi gani cha pesa kwenye hayo makaa ya mawe.

#MaendeleoHayanaChama
Mkuu kupanga ni kuchagua, hata nchi zilizoendelea kama urusi zinauza nishati nje kama moja ya njia za kuingiza mapato, Australia ina export mamilioni ya tani za makaa ya mawe kwenda china kila mwaka......
 
Washenzi watafurahi kuona rasilmali zinaenda kwa wazungu..badala ya kupambana wazungu wawekeze teknolojia na viwanda ili hayo makaa ya mawe yatumike kwaajili ya manufaa ya nchi na kwa kuwapa ajira watu wetu.

Mbaya zaidi hawajui bei gani yameuzwa na nchi imejipatia kiasi gani cha pesa kwenye hayo makaa ya mawe.

#MaendeleoHayanaChama
Akili huna wewe ni zero brain kabisa
 
Back
Top Bottom