Rekodi ya Diamond Platnumz YouTube inapoteza mvuto Afrika!

Sema hata hivyo Mondi kapambana sana Wakuu na inabidi tumpe support ili apate nguvu ya kurudi kwa kasi...

Save hii comment ikitokea Diamomd akaanguka leo kimziki bhas ujue Tanzania kwenye sekta ya muziki tutaanza kulinganishwa na Wazambia yaani kwa ufupi hata hao Wanaija mnaowashadadia kila siku wataanza kuwafungia vioo kwa sababu mtakuwa hamna impact yoyote kwao zaidi ya kutaka kuiba mpaka soko lenu la ndani muachwe mnashangaa tuuu.....
 
Unacompare msanii wa west tena Nigeria yenye population ya zaidi ya milioni 200 na msanii kutoka East Africa Tena anayeimba kiswahili.

Kuna kitu hakipo sawa kwenye hiyo makala.
Upo sahihi kwani hizi taarabu anazoimba siku hizi hazina mvuto kwa wasio juwa Kiswahili
 
Huu ni uchawi
 

Mwandishi ametumia nguvu nyingi sana “kumshusha” Mondi kwa kumlinganisha na wanaijeria....... kwani ni lini Mondi amewahi kuwazidi hao wanaijeria kwa hizo namba?

Wanaijeria wana soko kubwa sana kwa maana ya population yao na wamesambaa sana duniani kuliko sisi wa Tz

Na lazima tujue pia kwamba wasanii wetu wote wa bongo viewers zimedorora baada ya vifurushi kupandishwa bei

Pamoja na hayo yote Mondi bado anaendelea kukimbiza kwenye ukanda wake anaojidai nao miaka yake
 
Mbona ni simba tu mnampambanisha na wa huko Nigeria na mnajua hiyo nchi imetuzidi kwa kila kitu. Hata hivyo hongera kwake simba anasimamishwa mwenyewe na wasanii 10 tena chipukizi sio hata wale wa kitambo kama yeye
 
Ni vizuri hii taarifa imekuja kitaalamu na namba zake kabisa. Watasema una nia mbaya na chuki binafsi ila mimi nimependa hii taarifa maana inatukumbusha uhalisia ulivyo.
 
Upo sahihi kwani hizi taarabu anazoimba siku hizi hazina mvuto kwa wasio juwa Kiswahili
Diamond aache kupambana na madogo wanaokuja, muziki wake ubadilike kwa jinsi na yeye umri unavyokwenda. Hii tabia ya kumuweka Diamond kama kioo cha muziki wetu, kwamba akishuka, muziki wote wa Tanzania unashuka inatukwamisha sana maana haitoi nafasi kwa wanamuziki wapya kuja na kufanya vizuri. Nigeria wanatuachia hapo.

Ni mtazamo wangu tu.
 
Hao wanigeria waimbe kwa lugha igbo tuone watafika wapi
 
Mziki ukianguka wewe utaathirika na nini ?
Hao hao wanamuziki ndiyo wataamia

Ova
 
Ndio kawaida ya muziki kuna zama ambazo utatamba halafu lazima ushuke hata utoe ngoma kali kiasi gani lazima game likamatiwe na wengine tu

Hii ni kokote duniani ndivyo ilivyo kwenye music industry

Vizazi vinaenda vinabadilika nao wanakuwa na wasanii wao pendwa

Tukubali tusikubali jamaa kaweka legacy kwenye mziki wa bongo. Apewe heshima yake
 
Mtoa post jaribu pia kuangalia total population ya nchi ya wanaozaliwa hawa wasanii.

Ukubwa wa nchi katika muziki,aina ya mziki wenyewe.

Diamond akiiba miziki/midundo ya Kinigeria au congo au kushirikiana na wasanii wa nje ndiyo hupata viewers kwa maana ya kwamba jamaa hana mziki huo ila sauti kwake kwa kuikuza nchi lakini sio mziki wa bongo fleva.
 
Wanatakaje kwa mfano niwapumbavu sana hao
 
Naona watu wanatoa povu, wanataka Mondi Asifiwe tu. Hoja zijibiwe kwa hoja.
Je ameshuka au anazidi kupanda kimuziki?
Je anaelekea kubaki kuwa local artists au anazidi kutawala nje ya TZ na Afrika?
 
Naona watu wanatoa povu, wanataka Mondi Asifiwe tu. Hoja zijibiwe kwa hoja.
Je ameshuka au anazidi kupanda kimuziki?
Je anaelekea kubaki kuwa local artists au anazidi kutawala nje ya TZ na Afrika?
Post inataka kutuamisha ya kwamba hapo awali alikuwa nyimbo zake zikiongoza Sub-Saharan na sasa zimeshuka kitu ambacho ni uongo, Diamond kuwa na more than 2b views si nyimbo zake peke yake bali ni mkusanyiko wa contents zake zote anazozipost YouTube na hakuna wakati ambapo nyimbo zake zimekuwa zikipata views zaidi ya hit songs za Nigeria hivyo negativity ya post husika imekosolewa hapo kwani analazimisha kutuamisha kuwa Diamond ameshuka kwa kutumia mfano ambao si halisi.
Kwanini asiseme Wiz Kid, Burna Boy na Davido pia wameshuka kwani hawa youngsters wao wanawazidi kwenye views?
Kushuka kwa msanii si jambo geni lakini hata kama ni hater aweke mifano iliyo halisi.
Nimekubaliana na mchagiaji mmoja aliyeandika kwamba siku Diamond akiacha music tataacha kujilinganisha au kumnanga artist kwa kuzidiwa na artist wa Nigeria bali tutakuwa tukijipambanisha na
Wazambia na Wamalawi, levels za kujishindanisha na Nigerians(japo wala hatuwakaribii kwa achievements zao tangu enzi na enzi) ni kwa sababu tu kuna Diamond kwani wasanii wengine wote are just local artists.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…