KMkhalid
Senior Member
- Feb 26, 2018
- 118
- 225
Habari wana jukwaa. Kwa kweli hivi sasa bila connection ni ngumu kupata kazi, vinginevyo Mungu aingilie kati. Binafsi kwa neema ya M/Mungu nimefanikiwa kuwa nahistoria ya kufanya vizuri darasani, na kuwa mwanafunzi bora kuanzia nilipokuwa shule ya msingi mpaka chuo kikuu. Historia yangu kwa ufupi ipo hivi.
Primary
Ufaulu mzuri nikapangiwa kwenda sekondari, japo ni ya kata, wakati huu ndo shule za kata zimeanzishwa kwa wingi, hivyo hata wenye ufaulu mzuri walipelekwa shule hizi ili kufidia gap la wanafunzi
Sekondari
Nilifanya vizuri sana. Nimekuwa mwanafunzi namba moja darasani tangu kidato cha kwanza mpaka cha nne na nikafanikiwa kuzawadia cheti cha mwanafunzi bora na uongozi baada ya kufanya vizuri kwa miaka yote minne ya sekondari.
Nikafaulu kwa ufaulu wa daraja la kwanza, nikiwa mwanafunzi pekee darasa nzima la wanafunzi 138 mwenye daraja la kwanza na nikapangiwa kwenda Advance kwa mchepuo wa PCM (Physics, Chemistry, Advance Math)
Advance
Hapa napo sikukaa kizembe, katika darasa la wanafunzi 38, kidato cha tano na cha sita vyote nilikuwa mwanafunzi namba moja ama namba mbili kwenye mitihani ya terms na kikanda. Katika wanafunzi 38 wa PCM, wanafunzi 2 pekee tukafanikiwa kupata Div I. Hivyo moja kwa moja tukapangiwa chuo kikuu, na wote tulikwenda chuo kimoja, UDSM (University of Dar Es Salaam)
Chuo Kikuu.
Nikasomea program ya engineering (Engieering Geology), ni program ya miaka minne. Kwa ufupi hapa shule ilikuwa ngumu sana, ukijumlisha na changamoto za kifedha, lakini historia ya nyuma ya shule ilinibeba nikapata mkopo wa serikali 100%. Chuoni tulianza wanafunzi 14, lakini tuliobahatika kumaliza mpaka mwaka wa mwisho ni wanafunzi 6, na katika hao sita, ni mimi pekee nilifanikiwa kufaulu kwa kiwango cha juu kidogo ukilinganisha na wenzangu cha Second class honors, Upper division ambacho na hakika si kiwango haba kutokana na ugumu wa program husika.
Hio ndo historia yangu ya shule kwa ufupi sana, nimeelezea matokeo tuu, sijaelezea matukio. Lakini nasikitika kuona kwamba rekodi hio haijawa na mchango chanya kuniwezesha kupata kazi. Mpaka sasa kijana natangatanga, hapa na pale. Nipo wazi kufanya kazi kwenye migodi ya uchimbaji, kampuni za ujenzi wa majengo na barabara. Na kwa sasa nina leseni ya ulipuaji (blasting licence for both Open pit & Underground mining)
Hahah! Ama hakika kupata kazi zama hizi connection... Wakuu nipeni CONNECTION!! Umri ni miaka 27.