EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,325
Kwa mujibu wa Ibara ya 102(a) ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kila mkataba na makubaliano yaliyofanywa na mwanachana yoyote wa Umoja wa Mataifa lazima isajiliwe na kuchapishwa na Sekretariati ya Umoja wa Mataifa. Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni mkataba au makubaliano ya kimataifa yaliyofanywa baina ya wanachama wawili wa Umoja wa Mataifa wa wakati huo, yaani Tanganyika na Zanzibar kuwa nchi moja. Kwa maana hiyo basi, Hati ya Muungano ilitakiwa isajiliwe na kuchapishwa na Sekretariati ya Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa Ibara ya 102(a) ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Maraifa ina kitu kinaitwa UN Treaty Collection ambapo mikataba na makubaliano yote ya kimaitaifa huifadhiwa na kuchapishwa. Taarifa zinazohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinapatikana kwenye Document A/5701 ya May 18, 1964. Document hiyo ina barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenda kwa wawakilishi wa kudumu wa wanachama wa Umoja wa Mataifa akiwataarifu kupata "note" kutoka kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuhusiana na kuanzishwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar chini ya Rais Mwalimu Nyerere.
Katika barua hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliambatanisha barua kutoka kwa Waziri wa Mambo ya nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya tarehe May 6, 1964 ikimtaarifu Katibu wa Umoja wa Mataifa kuwa Tanganyika na Zanzibar zimeungana tarehe 26/04/1964 na kuwa nchi moja baada ya kusaini Hati ya Muungano (Articles Union). Nimeambatanisha Document A/5701 hapo chini. Pia waweza kuisoma hapa: http://ask.un.org/data/answers/files/178094/A5701-E.pdf
Ukisoma hiyo document hakuna sehemu yoyote inayosema kuwa katika barua yake, Waziri aliambatanisha Hati ya Muungano. Kama aliambatananisha Hati ya Muungano hata kama ni feki lazima ingeambatanishwa kwenye Document A/5701 kama barua ya Waziri ilivyoambatatishwa. Maandishi mengine ya Umoja wa Mataifa kuhusu historia ya Tanzania, yanasema kuwa katika mawasiliano mengine yaliyofanywa na Ubalozi wa Kudumu wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar November 2, 1964, kwenda kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yalimtaarifu kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar itajulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilimwandikia Katibu wa Umoja wa Mataifa ikimtaarifu kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuheshimu mikataba iliyosainiwa na kwa niaba ya Tanganyika: https://treaties.un.org/Pages/HistoricalInfo.aspx?#"United Republic of Tanzania"
It is questionable kama Hati ya Muungano iliwasilishwa au itawasilishwa lini mbele ya Sekretatiati ya Umoja wa Mataifa ili isajiliwe na kuchapishwa kwa mujibu wa Ibara ya 102(1) ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Maana kama ilishawasilishwa lazima ingechapishwa na kuonekana kwenye UN Treaty Collection. Nini matokeo ya kisheria kwa kutosajiliwa na kuchapishwa kwa Hati ya Muungano na Secretariati ya Umoja wa Mataifa?
Ibara ya 102(b) ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa inasema kuwa nchi iliyoingia kwenye mkataba or makubaliano ya kimataifa haitaweza kuutumia mkataba au makubaliano hayo mbele ya chombo chochote za Umoja wa Mataifa mpaka hapo huo mkataba au makubaliano yatakapokuwa yamesajiliwa na kuchapishwa na Secretariati ya Umoja wa Mataifa.
Article 102 of the UN Charter
(1) Every treaty and every international agreement entered into by any Member of the United Nations after the present Charter comes into force shall as soon as possible be registered with the Secretariat and published by it.
(2) No party to any such treaty or international agreement which has not been registered in accordance with the provisions of paragraph 1 of this Article may invoke that treaty or agreement before any organ of the United Nations.