Rekodi za Umoja wa Mataifa juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Rekodi za Umoja wa Mataifa juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Nauliza hivi: Je, Umoja wa Mataifa wameulizwa rasmi na Mamlaka wanayoitambua, kwa mfano Ikulu, Mambo ya Nje, Balozi wa TZ huko UN, Minister Plenipotentiary with Full Powers kwa maandishi na wakakana?

Jibu utalipata muda si mrefu kutoka wa JF members.
 
Nauliza hivi: Je, Umoja wa Mataifa wameulizwa rasmi na Mamlaka wanayoitambua, kwa mfano Ikulu, Mambo ya Nje, Balozi wa TZ huko UN, Minister Plenipotentiary with Full Powers kwa maandishi na wakakana?

Kuna tofauti kati ya kutambua nchi na mamlaka za nchi.
 
Kwahiyo UN ni Vihiyo? Wanaambiwa hati imeambatanishwa halafu wao wanapokea na hawafanyi kitu kuchunguza kama ipo au haipo?

Halafu kuna watu wanasema hati ya Muungano ilikuwa siri, hapana, hii hati imekuwa ikinukuliwa kwenye maandishi mbalimbali tokea huo mwaka 1964. Hata maktaba za sheria mlimani nakala ya hii hati ipo.

Kilichokuwa siri ni ile original copy ambayo ilisainiwa na Nyerere na Karume. Lakini hati yenyewe haijawahi kuwa siri na
hata wakati wa uhai wa Nyerere na Karume hakuna aliyewahi kukana hayo maandishi ya hati ya makubaliano ya Muungano.

Waziri wa mambo ya nchi za nje kisha sema hati ilipelekwa UN. Kwa wale ambao bado wana wasiwasi na Muungano wetu basi ulizeni UN kama TZ ilitimiza masharti yote ya kuwa mwanachama wa UN.
 
UN haijatumia barua kutoka kwa waziri wa mambo ya nje kuitambua Tanzania. Bali kuna vigezo ambavyo kila nchi mpya inatakiwa iwe navyo ili kutambuliwa na mataifa mengine na mashirika ya kimataifa. Baadhi ya vigezo hivyo ni pamoja na kuwa na permanent population, defined territory, government and the capacity to enter into international relations with other states. Kwa vile Tanzania ilikuwa inatimiza vigezo hivyo kulikuwa hakuna hata haja ya Waziri kuandika hiyo barua.Ni muhimu kuelewa kuwa Ibara 102(1) ya UN Charter inayotaka "Every treaty and every international agreement entered into by any Member of the United Nations... [to] be registered with the Secretariat and published by it" haina maana kuwa kutofanya hivyo basi hiyo nchi haitatabulika na Umoja wa Mataifa. Bali Ibara ya 102(2) inaeleza wazi kuwa "No party to any such treaty or international agreement which has not been registered in accordance with the provisions of paragraph 1 of this Article may invoke that treaty or agreement before any organ of the United Nations". Theoretically, one could argue that kama ikitokea malumbano baina ya pande mbili zilizotia saini hati ya Muungano halafu upande mmoja ukataka ku-rely kwenye hiyo hati mbele ya chombo chochote cha UN, upande wa pili unaweza ku-argue kuwa hiyo hati ya Muungano cannot be relied upon by the other party before the UN because it has not be registered by the UN Secretariat in accordance with Article 102(1) of the UN Charter. Umenielewa sasa?
Asante sana mkuu EMT hakika umetoa ufafanuzi unaojitosheleza hasa. Kwa hiyo iwapo utaibuka mgogoro wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar international law itazitreat kama nchi mbili tofauti maana Hati ya Muungano haikusajiliwa UN? Naomba ufafanuzi wako wa kisheria mkuu EMT.
 
Kwahiyo UN ni Vihiyo? Wanaambiwa hati imeambatanishwa halafu wao wanapokea na hawafanyi kitu kuchunguza kama ipo au haipo?

Ni wapi hapo UN waliambiwa kuwa hati imeambatanishwa? Badala ya kusingizia UN ni kihiyo, soma the details na utajua nani kihiyo.

Waziri wa mambo ya nchi za nje kisha sema hati ilipelekwa UN.

Kama imeshapelekwa UN mbona haonekani huko? Au UN wameambiwa ni ya siri?

Kwa wale ambao bado wana wasiwasi na Muungano wetu basi ulizeni UN kama TZ ilitimiza masharti yote ya kuwa mwanachama wa UN.

Kwani criteria gani huwa zinatumika ili nchi iweze kutambuliwa na UN?

Ni kama vile unadhani kuwa kupeleka hati ya muungano UN ndiyo kigezo cha kutambuliwa na UN.
 
Kama kweli kuna makosa hayo basi wa kwanza kulaumiwa ni UN wenyewe ambao wameshindwa kusimamia taratibu hizo na kuiruhus serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupata haki zote za uanachama huku ikiwa haijatimiza masharti.

lakini pia mkataba unaweza kupata uhalali kwa vitendo contract by conduct,kwa kipindi chote hicho cha 50yrs watanzania wamekuwa waki exercise mambo mengi ambayo yameanishwa katika mkataba ule wa muungano, kwa kwa dhamira zilizodhihilika kwa vitendo hiyo inatafsiriwa kama mkataba halali.

Jambo jingine mimi sijawahi sikia kwamba kule UN kuna tatizo la soveregnity ya jamhuri ya muungano wa Tanzania hii tafsiri yake ni kwamba Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni halali mbele ya UN kama sio halali pangekuwa na tatizo hilo la soveregnity.

Usichokielewa ni kuwa chochote ni halali duniani kwenye anga za kimataifa kama ipo kwa masilahi ya USA!

Sidhani kama utahitaji mifano kwenye hilo.


 
Back
Top Bottom