Rekodi za Umoja wa Mataifa juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Nauliza hivi: Je, Umoja wa Mataifa wameulizwa rasmi na Mamlaka wanayoitambua, kwa mfano Ikulu, Mambo ya Nje, Balozi wa TZ huko UN, Minister Plenipotentiary with Full Powers kwa maandishi na wakakana?

Jibu utalipata muda si mrefu kutoka wa JF members.
 
Nauliza hivi: Je, Umoja wa Mataifa wameulizwa rasmi na Mamlaka wanayoitambua, kwa mfano Ikulu, Mambo ya Nje, Balozi wa TZ huko UN, Minister Plenipotentiary with Full Powers kwa maandishi na wakakana?

Kuna tofauti kati ya kutambua nchi na mamlaka za nchi.
 
Kwahiyo UN ni Vihiyo? Wanaambiwa hati imeambatanishwa halafu wao wanapokea na hawafanyi kitu kuchunguza kama ipo au haipo?

Halafu kuna watu wanasema hati ya Muungano ilikuwa siri, hapana, hii hati imekuwa ikinukuliwa kwenye maandishi mbalimbali tokea huo mwaka 1964. Hata maktaba za sheria mlimani nakala ya hii hati ipo.

Kilichokuwa siri ni ile original copy ambayo ilisainiwa na Nyerere na Karume. Lakini hati yenyewe haijawahi kuwa siri na
hata wakati wa uhai wa Nyerere na Karume hakuna aliyewahi kukana hayo maandishi ya hati ya makubaliano ya Muungano.

Waziri wa mambo ya nchi za nje kisha sema hati ilipelekwa UN. Kwa wale ambao bado wana wasiwasi na Muungano wetu basi ulizeni UN kama TZ ilitimiza masharti yote ya kuwa mwanachama wa UN.
 
Asante sana mkuu EMT hakika umetoa ufafanuzi unaojitosheleza hasa. Kwa hiyo iwapo utaibuka mgogoro wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar international law itazitreat kama nchi mbili tofauti maana Hati ya Muungano haikusajiliwa UN? Naomba ufafanuzi wako wa kisheria mkuu EMT.
 
Kwahiyo UN ni Vihiyo? Wanaambiwa hati imeambatanishwa halafu wao wanapokea na hawafanyi kitu kuchunguza kama ipo au haipo?

Ni wapi hapo UN waliambiwa kuwa hati imeambatanishwa? Badala ya kusingizia UN ni kihiyo, soma the details na utajua nani kihiyo.

Waziri wa mambo ya nchi za nje kisha sema hati ilipelekwa UN.

Kama imeshapelekwa UN mbona haonekani huko? Au UN wameambiwa ni ya siri?

Kwa wale ambao bado wana wasiwasi na Muungano wetu basi ulizeni UN kama TZ ilitimiza masharti yote ya kuwa mwanachama wa UN.

Kwani criteria gani huwa zinatumika ili nchi iweze kutambuliwa na UN?

Ni kama vile unadhani kuwa kupeleka hati ya muungano UN ndiyo kigezo cha kutambuliwa na UN.
 

Usichokielewa ni kuwa chochote ni halali duniani kwenye anga za kimataifa kama ipo kwa masilahi ya USA!

Sidhani kama utahitaji mifano kwenye hilo.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…