Reli hiyo iko kwenye ukingo wa kusini wa Jangwa la Taklimakan, ambalo ni jangwa la pili kwa ukubwa duniani linalotembea, ikianzia mji wa Hotan upande wa magharibi hadi wilaya ya Ruoqiang upande wa mashariki. Reli hiyo ina urefu wa kilomita 825, ambapo kilomita 534 zinapita katika eneo la dhoruba ya mchanga, pia inachukua asilimia 65 ya urefu wa jumla wa reli hiyo, hivyo ni reli ya jangwani.