Reli ya SGR itakidhi mahitaji ya baadaye?



Hii ni station ya Morogoro (Sina hakika)

Kuna track 5, kuna weza kukawa na train ambayo itaanza safari nusu saa au dk 45 baada ya hii kwenda dodoma, pi kuna weza kukawa na train ambayo inaenda dar baada ya hii kufika hicho kituo nk.

Swa ni lini tutaunganisha mikoa mingine na SGR
 
Nilikuwa najua kuna track moja inayoingia pale ndiyo msingi wa hoja yangu ulipokuwa. Tunaelimishana. Hivi ndiyo majadiliano yanatakiwa kufanyika. Wewe umejibu hoja yangu kwa usahihi.
Hoja yako ni ya msingi sana hasa kwenye mwendo kasi.

Barabara zetu huwa zinafata straight line, so hilo sio sustainable njia ya mwendo kasi zilitakiwa zitafutiwe route za peke yake
 
Hoja yako ni ya msingi sana hasa kwenye mwendo kasi.

Barabara zetu huwa zinafata straight line, so hilo sio sustainable njia ya mwendo kasi zilitakiwa zitafutiwe route za peke yake
Hizi treni zije na nauli rafiki ili nauli za mabasi pia zishuke sana. Mwenye haraka sana anapanda treni, mwenye nauli ndogo ambaye yuko tayari kwenda taratibu anapanda basi. Pia barabara kubwa sipanuliwe ili wenye magari binafsi wanaotaka kushindana na speed ya SGR wajiachie 😀😀
 
Dar moro ni kilomete 200 ila zimejengwa 300 kwa ajili hiyo unayoseme ukitoa kituo kikuu pale reli inapo anzia pi pana njia mbili kama kilomete 3 kila upande ukija pugu ivyo avyo soga ruvu vituo vyote hadi Moro vinanjia mbili mbili kwaiyo kama treni moja inatoka Moro kuja dar na dar kwenda Moro zitapishana kituo cha kati kimo wapo
 
Kwani Kwenye stesheni hujaona tracks zaidi ya 5?!
Nimeshafafanuliwa, nimeelewa na kuridhika na majibu ya stormryder
 
Niliwahi sana kuonya serikali kuhusu jambo la kujenga reli yenye railway track moja tu kwa nchi kubwa kama hii inayotarajia kuwa gateway ya nchi majirani kama Congo, Uganda, Rwanda, Zambia, etc. Nilisema pale mwanzoni kabisa kuwa tusijenge reli kisiasa, tujenge two-way railway track kama tupo serious. Gharama za ujenzi zisingekuwa mara mbili kama watu wanavyofikiri, pengine ingeongezeka 15-20% tu ya gharama zote. Nchi tunaongozwa na wanasiasa katika mambo yote na tutaendelea kupigwa sana!

Zitawekwa sehemu maalumu za kupishana mkuu, hata USA zipo hivo, huwez jaza reli track mbili dar mwanza, gharama ni kubwa sanaaa,

Reli ndivo zilvyo ndugu, Hazitengenezwi kama barabara za lami

Kuna njia za kupishana

Sawa. Ila nadhani kulihitaji tracks zaidi ya moja zinazoingia stesheni kuu ili kuepusha jams. Muda utasema

Swali lako ni la kitoto sana, kwani kwenye hizi MGR zinapishana vipi?

Yeah huyu ni mtoto kweli na si ajabu hajawahi panda treni, ni wa kuhurumia tu

 
Ni wazi kutakuwa na uhitaji wa kufanya upanuzi wa miundombinu wanayojenga sasa kwa siku za mbele na inawezekana siku hizo za mbele siyo nyingi kama wanavyodhani.

Mimi naamini funzo la yale makosa yaliyofanywa kwenye barabara zetu bado halijatuingia kwa hiyo ni rahisi kurudia makosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…