Andy Ruiz Jr aka Destroyer nyota inazidi kung'ara upande wake.
Pambano la juzi dhidi ya Anthony Joshua lilikuwa ni pambano lilimwingizia kipato mara 10 ya ambacho amewahi kukipata.
Ameingiza takribani USD 5 Mil kwenye hilo pambano, wakati kiasi kikubwa alichowahi kupata ni USD 500,000.
Rematch inapangwa kwamba atapata USD si chini ya 10 Mil. Ukiacha add ons.
Tipwa Tipwa anairudisha Boxing kwenye ramani, mimi binafsi nilipunguza kuangalia boxing kwa sababu imepoteza mvuto, watu wanajilinda na kukwepa zaidi ya punching, ila Tipwa Tipwa kanionyesha radha ambayo sikuiona wakati Mayweather anapigana na Manny Pacq, Joshua vs Klitchko, Wilder vs Fury, etc etc.
Na kitendo cha kumshinda Joshua, ukilinganisha na body buildups zao, records na odds walizopewa, Randy kafurahisha watu wengi sana.
Namwombea pambano lake la kurudiana ashinde.
Kuna watu tulikuwa tunasema kwamba Joshua hajawahi kukutana na real tests, na muda wote kambi yake walikuwa wanakwepesha kumpa mapambano yenye uzito, lakini katokea Randy katuthibitishia.
Ama kweli, kurukaruka siyo dawa ya ulimbo.