repoti ya kifo cha albert mangweha ni fake! aliye fanya hivyo alaaniwe!

repoti ya kifo cha albert mangweha ni fake! aliye fanya hivyo alaaniwe!

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Report iliyo jaa kwenye blog mbalimbali za bongo hata jamii forums imegundulika kwamba ni fake yaani wamecopy na kupaste kutoka kwenye report ya doctor aliyo itoa baada ya msanii amy winehouse kufariki.angalia HAPA. mia
 
FP hebu njoo huku rafiki. Unakumbuka nilihoji kuhusu authenticity ya hiyo ripoti?

Common sense yangu iligoma kukubali haraka haraka maana, kwanza, ni mapema mno kwa toxicology report kutoka haraka namna hiyo. Pili, hakukuwa na link yoyote kwenye hiyo taarifa ambayo inathibitisha kwamba iliandikwa na huyo daktari. Tatu, hakukuwa na contact info zozote kwenye hiyo taarifa.

Ndo hapo radar zangu zikaanza kubeep. Sasa wasemaje rafiki? Haya mambo ya taarifa za kwenye mitandao ni ya kuyachukulia kwa makini sana la sivyo kuingia mkenge ni rahisi sana.

Bofya hapa uone uchambuzi wa wengine kuhusiana na hiyo so called taarifa.
 
Binafsi pia nilishangaa ripoti inasema ana miaka 28 ilhali alikuwa in early 30's.
 
Magazeti ya leo yamenukuu hiyo taarifa kama ilivyo eti ndo sababu ya kifo cha Mangwea. Kama ni kweli hyo taarifa ni ya uongo basi magazeti yetu kweli hayana weledi hata karesechi kadogo tuu kuhusu uhakiki wa taarifa hawana.
 
Aiseee kila kitu fake Tz....hata picha ya yule dada aliyehusishwa na. Kifo cha RPC Barlow ilikuwa fake
 
Nchi ina ombwa (vacuum) kubwa kuliko tunavyo weza kufikiri! Wasiwasi wangu ni kwamba, sijui kama watanzania tunajua kuwa yote haya ni kutokana na mfumo mbovu wa elimu yetu?! Watu wana desa hata ripoti za vifo wana chakachua majina, magazeti nayo kwa kuwa mengi yana waandishi wasio na weledi na taaluma bora nayo yana copy na ku-paste huku yakiweka vikorombwezo, walaji (wanunuzi) nao kwa kuwa elimu ni duni wanakosa tafakuri jadidi (critical thinking) nao kwa kuwa elimu ni kanyaboya wanameza na kusambaza uwongo kama walivyo usoma kwenye gazeti na kama gazeti lilivyo udesa uwongo huo kwenye mtandao.

Hitimisho.

MAJANGA
 
Kizazi cha kupaste hicho na bado wengine matokeo yao yapo jikoni kwa mara ya pili.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hv mnataka mtueleze nini hapa?ngwea amekufa au hajafa?
 
Hv mnataka mtueleze nini hapa?ngwea amekufa au hajafa?

Mkuu sio hivyo. Kufa kwa ngwair sio sababu ya kutunga report fake. ilitakiwa marehemu atendewe haki. Kufa alikufa lakini kilicho muua hakijajulikana, sasa kwani walete report fake ya kifo chake? je wewe unaona si sawa?. mia
 
The fact Ngweir is dead, haya mengine ni mapambio tu na kushrehesha, sidhani kama Watanzania tuna kazi au tunahitaji report za chanzo cha kifo.

Ingekuwa ni hivyo mauwaji ya kitu chenye ncha kali yasingekuwepo hapa kwetu.
 
Back
Top Bottom