Nchi ina ombwa (vacuum) kubwa kuliko tunavyo weza kufikiri! Wasiwasi wangu ni kwamba, sijui kama watanzania tunajua kuwa yote haya ni kutokana na mfumo mbovu wa elimu yetu?! Watu wana desa hata ripoti za vifo wana chakachua majina, magazeti nayo kwa kuwa mengi yana waandishi wasio na weledi na taaluma bora nayo yana copy na ku-paste huku yakiweka vikorombwezo, walaji (wanunuzi) nao kwa kuwa elimu ni duni wanakosa tafakuri jadidi (critical thinking) nao kwa kuwa elimu ni kanyaboya wanameza na kusambaza uwongo kama walivyo usoma kwenye gazeti na kama gazeti lilivyo udesa uwongo huo kwenye mtandao.
Hitimisho.
MAJANGA