MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,607
Hili ni nino lililojichukulia umaarufu mkubwa Duniani. R.I.P ni neno ambalo japo mzizi wake ni kwenye madhahebu ya kikristo maarufu lipo katika lugha za nchi nyingi mbalimbali duniani bila kujali dini wala muelekeo wa imani. Na wakati mwingine linatumiwa na hata wasiomuamini Mungu.
Mfano;
1:Urusi ( Покойся с миром )
2: Waarabu (Orqod fi salaam)
3:Wachina (Ān xī, )
4:Wakorea (Samga goinui myeongbogeul bimnida)
........ na wengine wengi nafasi haitoshi.
HISTORIA YA FUPI YA R.I.P.
R.I.P sio neno lililoanza leo, historia inaonyesha limeanza kutumiaka toka karne ya 8. . R.I.P ilianza kushamiri kwenye makaburi hasa ya wakristo na kuanza kutumika kama salamu ya kumuombea heri marehemu karne ya 18. Changamoto ikaja kuwa hakukua na ushahidi wowote wakujitosheleza kuamini kuwa Kuna roho inaenda sehemu ambayo inauwezekano isiwe na amani kwa hiyo inahitaji kutakiwa amani huko iendako. Muda mwingi kabla ya salamu hii ulielekezwa kuwapa pole wafiwa na kuwapa matumaini ipo siku yote haya yataisha.
Maswali kadhaa yanaibuka kuhusu heri/salamu hii anayotakiwa Marehemu.
1: Je kuna ushahidi wa kutosha nje ya imani kuhusu uhalali wa salamu/heri hii, au salamu/heri hii huwa inamfikia mlengwa?
2:Je, Kwa watu ambao hawaamini uwepo wa maisha baada ya kifo, kuna ulazima wa hii salamu?
3:Kuna uwezekano au uhakika wowote kuwa salamu au heri hii inamnufaisha mlengwa?
4:Kama salamu/heri hii ilianzishwa na imani moja ya dini, nini kilisababisha itapakae dunia nzima kwa watu wa imani nyingi zinazopingana?
5: Je dunia inaneno moja katika mazingira kama haya litakalokubalika na watu wote, wa imani zote na wasio na imani yoyote?
5:Ni njia ipi bora kama hii ikioneka haikidhi viwango vyako vya imani au kama hauamini Mungu itakayofaa katika mazingira ya kuondokewa na wenzetu?
Najaribu kuwaza,........
Nini maoni yako