Rev. Reinhard Bonnke: Kusanyiko kubwa la injili linalosisimua liambatanalo na uzushi mwingi

Rev. Reinhard Bonnke: Kusanyiko kubwa la injili linalosisimua liambatanalo na uzushi mwingi

Nimewahi hudhuria mkutano wake Malawi mwaka 1985 uliokuwa na miujiza kibao.
nakumbuka mabango yalikuwa yameandika " IDZANI MUDZAONE ZOZIZWA ZA MPAMVU YA MULUNGU ZOCHITIKA MMOYO WANU"
kumbe wewe ni mmalawi
 
Lile kusanyiko Kubwa la aina yake lililowahi kutokea nchini mwanzoni mwa utawala wa B.W. Mkapa June 1996 (miaka 20 iliyopita) leo lipo mjini Mwanza ambapo mwinjilisti wa kimataifa R. Bonnke atalitikisa jiji la miamba al maarufu Rock City kwa mahubiri yake ambayo huwavuta wengi.

Kusanyiko hili huvutia watu wengi wengine kutoka mikoa ya jirani ambapo pamoja na wengi kuja kushuhudia mahubiri wengine huvutiwa kushuhudia maandalizi makubwa ambayo hufanywa kufanikisha kutaniko hilo.

Matumizi ya teknolojia za kisasa na ghali ambazo huchukua muda wa kutosha kufungwa katika viwanja vya Furahisha, promo za kutosha kupitia vyombo vya habari na mapokezi makubwa ambayo hupewa mhubiri huyu naamini vitasababisha viwanja vya furahisha kutapika.
Mliokuwepo na kushuhudia mkutano wa 1996 mnakumbuka nini?
Mkutano huu utaacha gumzo kama la 1996 lililochukua muda kusahaulika?
Tuendelee kupeana updates za yale yanayoendelea hapo jijini na eneo la mkutano, picha mbalimbali zitanogesha zaidi habari hii.
Nipo nje ya jiji.

Nakumbuka Siku alipoita watu kuwaombea wasiumwe malaria tena nilikuwa ni mmojawapo. Niliombewa na mpaka leo sijawahi Kuumwa tena malaria na uzao wangu. Msikose mkapokee kwa hitaji lenu
 
Kwa hiyo unataka kutueleza kuwa al Qaeda na so called magaidi ni viongozi wa dini na mnawatambua? Sometimes tumia akili uweze kupambanua ukweli wa neno na Imani ya dini husika. Mungu amekupa utashi kupambanua.
 
Ni zaidi ya saa moja nimeona kile ambacho kimefanyiwa kazi na jicho pevu kwanza nianze kumpongeza Mohamed Ally kwa weledi mkubwa kwa kufichua ufedhuri wa Victor kanyari na hii ipo sana kwenye ulimwengu wa leo kwa kila dini , muhimu ni kuwa na elimu ya kuyendea mambo ,
kingine faiza unapo ona ubaya jua pia na uzuri upo kwa maana kwamba si wote wanahubiri kutaka fedha kam Mohamedy mchambuzi makini tofauti na wewe Faiza alivyo muhoji Askofu ambaye alikiri uwepo wa mambo haya kama yalivyotabiriwa kwenye maandiko matakatifu
sasa unaweza kudhibitisha hicho cha Askofu kanyari na mahubiri yanayoendelea Mwanza kuwa yana ufanano na hiki ulicho post?
 
Yupo viwanja vya furahisha na mwanae DANIEL COLENDA
 
Utapeli wa Global Church Mission Tz-Mwanza Serikali Wapi?
 
Habari njema za Yesu Kristo anayesamehe dhambi za watu WOTE zinaendelea kuhubiriwa. Ni bora uwe sehemu ya wale wanaotaka kusamehewa dhambi zao. Kwa kuwa tangu kufufuka kwake wengine walipinga na wanapinga na bado watapinga LAKINI Yesu Kristo anaendelea kusamehe dhambi hata sasa.
 
Mungu aendelee kuubariki mkutano huo
Na miujiza iendelee kutendeka na watu wampokee yesu.
 
Huu uzi ni aina ya promo yenye ubunifu, kasema unafiki lakini hakuna sehemu kagusia, pia kajidai kakosea muhubiri kwa kufanya masahihisho pale mwishoni mwa uzi. Hovyo kabisa
 
Huu uzi ni aina ya promo yenye ubunifu, kasema unafiki lakini hakuna sehemu kagusia, pia kajidai kakosea muhubiri kwa kufanya masahihisho pale mwishoni mwa uzi. Hovyo kabisa
Hovyo mwenyewe, uliza ujibiwe
 
Mengine siwezi eleza, yaliyoelezwa na waliochangia kuhusu uzushi ndio habari zenyewe zilizokuwa zikipita hapa na pale.
 
Back
Top Bottom