Revealed: Maamuzi mabovu kwenye EPL yameibeba Man United msimu huu

Revealed: Maamuzi mabovu kwenye EPL yameibeba Man United msimu huu

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Posts
13,203
Reaction score
23,027
Kutokana na uchambuzi uliofanywa (na unaoendelea kufanywa) na mtandao wa "You Are The Ref" kwenye mwenendo wa ligi kuu ya England (EPL), msimu huu maamuzi mabovu ya marefa yameibeba sana Man United.

Mtandao huo unanyetisha kuwa hadi round ya 27 ya ligi inakamilika, Man United walitakiwa wawe nje ya top 4 huku wakiwa wamejikusanyia pointi 52 badala ya 56 walizonazo sasa.
Pia, walipaswa kuwa kwenye nafasi # 5 kwenye msimamo wa ligi.

Kwa upande wa Man City, uamuzi mbovu wa marefa nao umewapa pointi 4 zaidi ya walizopaswa kuwa nazo (walitakiwa wawe na pointi 68 badala ya 72 walizonazo sasa). Hata hivyo, matokeo hayo yasingeweza kuwaondoa kwenye nafasi yao # 1 waliyo nayo sasa. Man City msimu huu wana bahati ya pekee kwa kujiweka kwenye ligi yao wenyewe ya timu 1.

Liverpool wao wameathirika negatively na uamuzi wa marefa. Wanazo pointi 54 lakini walipaswa kuwa nazo 56 na hivyo walipaswa kukalia nafasi # 2 kwenye msimamo badala # 3 ya sasa.

Halikadhalika - Chelsea, Spurs na Arsenal nao wamekuwa wahanga wa maamuzi hayo mabovu. Hapa chini ni takwimu za points na nafasi zao (kwenye mabano ndiyo stahiki yao kama maamuzi yangekuwa sahihi):

Chelsea: pointi 53 (54) / nafasi #4 (#3)
Spurs: pointi 51 (52) / nafasi #5 (#4)
Arsenal: pointi 45 (50) / nafasi #6 (#6)

Ingia hapa ujisomee mwenyewe ------> Premier League referees DO favour Manchester United - and here's the proof

My take:
Jose Mourinho alinukuliwa hapa majuzi baada ya Man U kubanjuliwa 1-0 na Newcastle akidai "miungu ya mpira ilikuwa upande wa Newcastle siku hiyo". Kama yupo sahihi, basi ni miungu hiyo hiyo ya mpira ndiyo imekuwa upande wa Man United msimu wote huu tangu uanze!

Wanazi wa Man United - povu ruksa!!!
 
Za kuambiwa changanya na zako.

We jamaa bana umeniacha hoi manchester ana point 56 sijui liverpool 55 haya unapigwa na swansea manchester anapigwa newcastle hapo waamuz wanazuia nn kuishika nafas ya pili

Tuje city anafumua wote na mchezo mzur ina maana yy hakutan na maamuz mabovu?

Toka timu ya pili hadi ya 6 wapo hoi uongo mbaya tusitafute visingizio chelsea kapigwa mech mbili mfululizo ina maana marefa walikuwa wanatumbukiza magoli yale?

Timu ukicheza kandanda safi hata refa ubebeje point 3 zinanyakuliwa.
 
soma tena post yangu mdau wa manure!
 
soma tena post yangu mdau wa manure!
Nani kaizuia liverpool kushika nafasi ya pili kwa akili yako point 3 za marefa na mechi walizocheza huo ndo mwisho wa liverpool? Kopi vitu vyenye afya city point 72 liverpool point 54 unalilia point 2 upo timamu kweli mshabik wa liverpool?
 
msisitizo hapa ni Man U kuwa nafasi # 2 badala ya # 5 wanayostahili kutokana na kugewa point 4 za dezo na marefa!

Mourinho juzi alikuwa anatoka machozi kwa kukosa pointi 3 kutoka Newcastle, so Liverpool kuzikosa pointi 2 kutokana na maamuzi mabovu si jambo la mchezo mchezo!
 
Kama Man yu wa nafasi ya tano basi ataenda kwenye nafasi yake tu mbona ligi haijaisha
 
Back
Top Bottom