Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Mwanaume wa kweli haumizwi na mwanamke hata siku moja, unajinyima unampa yeye huyo mkeo? Haya ni maneno ya kishujaa tu sio chochote unachoweza kumfanyia maana dume kamili huwezi lialia huku mbele ya Umma ila ungefanya tu kwa kitendo ukutane na sheria ukavunje mawe maweni tanga kwa ujenzi wa Taifa.
Wewe umekutana na mtu keshapendeza unataka kujimilikisha kirahisi kimikwara unajua alikotokea mpaka akakuvutia? Kila mtu na uhuru wake, sio mkeo huyo na hakukutongoza wala hajakutuma kumgarimikia, tumia akili wakati mwingine badala ya ujinga.
'Well said'
 
Asee mkuu umeongea point sana kuna watu huwa hatuwezi kuwa na umiliki wa mtu zaidi ya mmoja.unampa mtu moyo wako Halafu anacheza nao kwa kudhani amekuwin.ukigundua na kuhakikisha bila chenge revenge is the best answer.kunywa soda kwa mangi hapo nakuja kulipa aisee
Pole sana achana na visasi jua karma is real atajuta muda sio mrefu
 
Mkuu safari yako bado ipo tarehe 22 ni kesho ? Na vipi asipoenda kwa huyo mwanaume Bado utapeleka kilio utabadili msimamo ?
 
Songa mbele
Japo umekataa ushauri nakushauri usigeuke
 
Hakuna kitu bitter kama kumnunulia dem wako chupi kaaaaali afu mchizi anakuja kuivua na kuitupa juu ya neti kisa tu aupate utamu ulojaribu wewe kuuficha.
Mzee kama mwisho m'baya naiwe nitakusotea mpaka laana ulofanya ikutafune.
 
Kwa ufupi hii ni taarifa tu, so ushauri wako hautabadili chochote wala kuongeza chochote, vipi lakin uzima upo??

Ni hivi, mi huwa siumizwi alafu anayeniumiza akabaki salama, nikiumizwa mi nakuumiza mara 10 alafu fresh, maisha yenyewe mafupi haya, mi niwe na stress alafu wew ucheke ili kiwe nini... sipendagi ubwege kabisa, na nitabaki kwenye kumbukumbu zako milele ukijifanya kuniletea habari za ajabu..

Miez 8 iliyopita nilidate na dada mmoja hivi mrembo, height moja hivi mauzo sana na mzigo wa kuvuta huko nyuma haukuwa haba, kifupi mvuto wa yule dem hauna shaka, kama ni maksi basi A ya 95+... mapema nikamwambia mambo ya kiboya sitaki, km utacheat jitahidi nisijue, nikijua umeumia....Akajifanya hadi kulia pale kwamba ananilove nyang'anyang'a na kamwe hakuna mwanaume kama mimi, nikasema poa but take my words ukinizingua hutoamini nitakachokufany, na km hunitaki niache uende, na kama pia itakuw mechi za dharula tu alafu kimya tuambiane, moyo wangu hauchezewi.. akasema nisiwe na shaka ananipenda, nikasema poa.

Tabia yangu ni kwamba kamwe siwezi kuwa na mpenzi zaid ya mmoja kwa wakati mmoja, so nikiwa na mmoja huyo huyo. Sasa mwezi mmoja nyuma nikausoma mchezo dizain kama demu wangu analiwa hivi, sikumuuliza, nikakomaa hadi nikapata password zake facebook na insta.. nikazama inbox yake, daah ni balaa tupu, ashapigwa mashine na mshikaji mmoja hivi, then jamaa dizain kama anakomaa naye amle 0715 hiv sema demu anabana.. text yake hii hapa..

"Baby naridhika sana nawew, ila unanibania side B, nyimbo za side A zote nimeskiliza why uninyime za side B mpenz?, kama side A nilsikilza kwa elfu 70 bas side B lazma dau lipande.. nielewe bas"

Demu akajibu..

"Mi nina mtu na tuna malengo je akigundua na kuniacha itakuwaje"

Jamaa..

"Hawezi gundua, kwani huwa anakagua huko, ila navyokujua huwez nibania.. nitakutoa out ukafanye shopping ya maana, na nitakutumia 100,000 kesho"

Demu...

"Mmh poa tutaangalia tukikutana tar.22 jamaa akiondoka kama tulivyopanga".

Zipo nyingi nying but hizo kiufupi,....

Mimi kwa huyu demu..., nampa nachopata, najinyima sana apate yeye, nishamtoa shopping za maana mara kibao na tayari nishaandaa pesa nzuri tu kwa ajili yake, Krismass na mwaka mpya, maana tar.hizo sitakuwepo kutokana na majukum ya kazi yangu, nammudu kiujumla, nguo, usafiri, pesa ya kula, malazi nafanya mimi.. yeye hana chochote zaid ya gamba lake la diploma. Muda wote huo sina demu zaid yake.. na on bed naperfom fresh hadi anaomba poo yeye..

Nilichokifanya baada ya kugundua hilo, nimescreenshot charting zote hadi picha walizopiga wakiwa lodge wametumiana kupitia fb messenger nimejitumia kwenye simu yangu, then nimeuchuna.. kifupi tayari nimeshampiga chini ila siwez kumwambia tuachane kiboya boya hiv bila yeye kuonja joto la jiwe kidogo, na kamwe sitafanya naye mapenz tena.. ambacho kimebaki kwake ni kumpa kidonda cha milele..

Ifahamike ananipenda japo tamaa anazo, ashanitambulisha kwa rafiki zake wote, dada yake, hadi mama yake.. kifupi anaitwa mrs mimi... na uchafu anaoufanya ni siri kubwa sana na ndo maana anatumia fb messenger maana anajua siwez hisi chochote huko.. tayari tarehe ya kupeleka barua ishapangwa, tarehe 07 jan... mashangazi zake wote wanajiandaa kwa tukio hilo.. upande wetu pia tunajiandaa..

Nataka nifanye nini?? Siku hiyo ya tukio la kwenda kwao kujitambulisha rasmi ndo siku yangu ya kumuumiza, maana kwao anaaminika sana, anaimba kwaya kanisan, ana vyeo vingi ving vya huko kanisani.. na huwezi mzania hata kidogo kama ni mshenzi.. siku hiyo mbele ya Mchungaji wake, ndugu zake, mama ake, mashangazi na marafiki zake wakiwa na smartphone zao naenda umiza mtu vibaya sana, sio kwamba nitampiga hapana, ila nataka nimafanyie tukio ambalo litaweka maumivu ya kudumu kwenye moyo wake na kamwe hatokuja nisahau..

Tarehe 7 january, save the date....

USIPOTEZE MUDA KUNISHAURI CHOCHOTE, HUWA NIKIPANGA SIPANGUI..
ukifanya hivyo akijiua utashukuru mungu au utajuta fikiri kabla ya kutenda kikubwa ni kuachana naye tu c o kumfanyia hvyo je ww u msafi kiasi gani?
 
Back
Top Bottom