Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

[emoji44][emoji44]mwanaume kuchepuka si ajabu???[emoji134]
Kwahiyo unataka uhalalishe dhambi ya uchepukaji kwa mwanaume!
Hufai.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jambo la kawaida sana. Mwanaume akitulia sawa ila akichepuka sio ajabu. Ajabu ni mwanamke kutoka nje ya ndoa yake.

Huwa inashangaza sana.

Hivi wewe leo usikie kuwa mzee wako kachepuka au usikie mama kachepuka ni ipi itakushangaza?
 
[emoji44][emoji44]mwanaume kuchepuka si ajabu???[emoji134]
Kwahiyo unataka uhalalishe dhambi ya uchepukaji kwa mwanaume!
Hufai.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijahalalisha mimi..nimesema kuwa sio ajabu sana.

Mfano

✓Si ajabu sana kwa baba mzazi kurudi usiku amelewa.

✓Ila ni ajabu sana kwa mama mzazi kurudi usiku huku amelewa chakari.

Read between the lines na uweke uhalisia kidogo.
 
Sijahalalisha mimi..nimesema kuwa sio ajabu sana.

Mfano

✓Si ajabu sana kwa baba mzazi kurudi usiku amelewa.

✓Ila ni ajabu sana kwa mama mzazi kurudi usiku huku amelewa chakari.

Read between the lines na uweke uhalisia kidogo.
Ulevi ni ajabu kwa jinsia zote.
Uchepukaji ni ajabu kwa jinsia zote.

Mungu alipoweka amri alitupa wote tuzifuate,hakutoa kwa wanawake tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mume aliyemuoa yule binti alinipigia, tukasalimiana akajitambulisha kuwa ni mwanaume wa yule binti na wapo kwenye ndoa kwa muda sasa, akasema yule binti alifanyiwa mpango na baba yake binti alidanganywa kuwa binti alikuwa anakosa aman kwasababu alikuwa anampenda jamaa, Kwahiyo mzee akamwambia haoni sababu ya binti yake kuteseka akaona amfuate tu, akamuahid kumpa duka moja na kiwanja ili amuoe binti yake, jamaa alikuwa ametoka chuo hana kazi akaona ni fursa akaona fresh tu, kumbe ilikuwa trick. Wazazi wakashauriana wakaona wafanye hivyo ili mtoto wao angalau apate amani labda.

Huyu mzee alifahamiana na yule kijana baada ya kukutana ofisin kwa mzee, kijana alikuwa field na huko ndipo walikofahamiana, na hata binti wa mzee walikuwa mara kwa mara wanakutana na yule kijana enzi hizo.

Binti akapangwa kwamba huyo kijana anampenda sana anataka kumuoa ndo akawa mbishi kwasababu ananisubiria mimi ndipo mama aliamua kunipigia simu na kuongea namimi kuhusu kumhakikishia binti mim nimeoa.

Taratibu za kulipa mahari zikakamilika ndani ya miezi 2, aliambiwa ajipangie mahari jamaa akasema yeye hana kitu ila ana kias kdg kimebaki kt boom lake, ni km laki 2 hv, mzee akamwambia kinatosha hicho, so amtume mshenga na atoe taarifa kwao waje, but wakacheza trick kwamba atatajiwa million 2.5 ila yeye asijali atatoa hiyo hiyo laki 2, walifanya hivyo ili kuondoa soo maana ingesikika ameolewa kwa laki 2 ingekuwa dharau sana.

Jamaa akatoa taarifa kwao kwamba anataka kuoa haraka iwezekanavyo, mzazi wa jamaa akamdadis kuhusu mahari na endapo anamfahamu binti vema, akadanganya kwamba kipindi yupo chuo alikuwa anafanya buziness sema alificha, so yupo njema kiuchumi na wapo kwenye mahusiano kwa miaka kadhaa basi mshenga akatumwa taratibu zikakamilika na michakato ya ndoa ikaanza sasa, jamaa alisema kiukweli yule binti hakumuelewa sana ila akajipa moyo atajifunza kimpenda ndani ya ndoa lakin kikubwa ni fursa pia ya kutoka kimaisha maana mtaa ulimkalia vibaya mwana. Baada ya taratibu zote kukamilika jamaa akaoa.

So wakaingia kwenye ndoa kila mtu akijua mwenzake ndo amempenda sana kuliko yeye, binti anajua jamaa amemuelewa zaid kuliko yeye na jamaa akajua binti ndo amemuelewa zaidi, so wakawa wote wanasubiri kuprove upendo, wakajikuta wanategeana sasa, wote hawapendane ila trick imetumika lengo likiwa ni binti awe sasa, mshkaji hajui na bad luck hakujsumbua kupeleleza sana, ingawaje taarifa za ndoa kuahirishwa kwa yule binti alikiri kuzisikia ila hakuichimba kiundan maana alijua ni kawaida tu kuchumbiwa na kuachwa. Mzazi wa binti alitimiza ahadi of course alimpa kiwanja na duka moja alilitoa km zawadi siku ya ndoa, na kuna pesa ilipatiakana siku ya harusi na vyombo na vitu vingine, so maisha yakaanza.

Ndani ya ndoa vitimbwi vikawa vingi, binti akawa mkorofi na jeuri, ikabid mshkaji arudi kwa wazazi wa binti na kuwaambia mbona haoni dalili za binti kumpenda but daily imekuwa akiimba mahusiano yake yaliyovunjika huko nyuma, na kwamba mimi najisumbua tu yeye ana mtu anayempenda, na ipo siku atamtoroka aende kwa huyo anayempenda, na kwamba jamaa ni chaguo la wazazi na sio yeye. Wazazi wakawa wanamtuliza kwamba amvumilie tu haya yataisha. Sasa siku zinavyozid kwenda mambo kwa jamaa yakawa magumu,demu anamnyima hadi penzi sasa, akaona ni shida na kwa kuwa alkuwa msomi wa chuo kikuu, akaamua kufungua akili apeleleze kiundan, ndipo alipopata habari zangu sas kwa kina na jinsi ilivyotokea hadi kushindikana kwa ile ndoa yangu na binti.

Akarudi kwa demu, demu akamchana ni kweli kbs, binti akashangaa kivipi yeye hajui wakat wazazi wake walimueleza kuwa jamaa anajua kila kitu na yupo tayari kumvumilia. Jamaa kichwa kikawaka moto akajua tayari ameuingia mtego na ndoa ishafungwa, balaa zito.

Akaona hana jinsi zaidi ya kijaribu kulitatuta hili maana demu akawa anamchanganya mshkaji na kumdanganya eti anawasiliana namimj na muda wowote atamtoroka aje kwangu, mshkaji alikuwa hampendi kivile ila ndo hivyo alijipatia fursa ya kupata ugali wake angefanyeje na maisha haya magumu hivi.

Nikamuuliza kwanin amenipigia simu, akasema ashapata ukweli wote so anaomba nisiendelee kuwasiliana na binti yule maana nakwamisha maisha yake, nikamwambia asiwe lofa, mim siwez kumpigia huyo bint na wala sijawahi kumpigia tangu lile tukio pale kwao lilivyotokea, nikamwambia apambane yule demu anamchezea akili, kwa kuwa amekuwa mpuuzi wa kutaka kitonga basi agangamale sasa ila mimi sina mpango na mke wake kabisa, nikamuuliza nani kampa namba yangu akadai aliifuatilia kwa mke wake, so tukamalizana hivyo.

Mwaka jana mwishoni kabisa yule binti akanipigia akasema amegundua kila kitu na kwamba sijaoa na zile picha ilikuwa trick tu amewasilana na rafiki yake na amepata ukweli, ashagundua nilicheza mchezo na mama yake, so amepata ukweli na anaomba tuonane, nikamwambia asiwe boya mimi kama mim siwez kumuoa kwanza hata kuongea naye tu kwa simu ni neema, na pia yeye ashafunga ndoa madhabahuni, inyeshe jua au mvua yey ni mke wa mtu aache umalaya atulie kwenye ndoa yake. Demu akakataa akasema haelewi chochote zaidi yangu.

Baada ya wiki kadhaa yule rafiki yake akanitafuta, of course tulikuwa tunawasliana wasiliana lakn sio mara nying, kwasababu nilishamuona anataka kunifelisha so nikawa nampotezea poteza, alivyonitafuta akaomba aoanen namim, kipind hicho sasa nipo Geita huko, nikamwambia kuna nin, akasema ana ujumbe muhimu sana tuonane, nikamuona nayey lofa, nikasema sawa nikija dar nitakushtua.

Nilipofika jijin dsm mwaka huu sasa hiyo mwanzon kabisa, nikapiga kimya nikaona nisije nikanaswa kwa huyo demu nikaharibu cv, km kawaida yake kuja kuja home akanibahatisha, safari hii nikamchana tu aongee point zile pumba zake akiongea nitampapasa then tutakuwa maadui kbs, nikampa nafasi asema anachokusudia kusema sasa, kiukweli kibinadamu kwa mbali udenda ulikuwa unanitoka, mtoto alikuwa mtamu yule jamani kwa macho tu hv alikuwa anaita sana, lakn kiburi changu cha ndani kbs kikawa kimeizid tamaa ya mwili.

Demu akafunguka sas, kwamba yule binti amemtoroka mume wake huko na yupo jijini na yupo kwake na lengo lake ni kunivamia home akiingia tu anakomaa hatoki, hata polisi wakija atazusha nimemtelekeza kisha uwe msala, so yeye ndo akamwambia asijali ratiba zangu zote anazijua kwahiyo awe mpole nikirudi kutoka safari lazima yeye ajue then atamdirect aje, Kwahiyo leo amekuja kwanga kuniambia hilo lakin kikubwa yeye hayupo tayari kuona mimi naishi na rafiki yake, yeye anaitaka hiyo nafasi kwasasa, so hawezi kuruhusu eti yule dada aje kwangu tena. Nikamwambia aache uongo mimi sidanganyiki kirahisi, akampigia simu na kuweka loud akawa anamwambia asijali mimi nipo Mwanza na nikirud tu lazima yeye ajue na atampa taarifa, yule binti akawa anasisitiza amsaidie afanikishe tu kuingia home na anikute.

Nikabaki natafakari cha kufanya, so huyu demh sas ndo akanichana hivyo akasema ananipa siku 3 nitoe jibu either amdirect demu aje au nimkubalie ombi lake alafu yeye afajia jins ya kumfanya rafiki yake anichukie na aachane namim akaconcetrate kwenye ndoa yake.

Wakuu niliahid kumaliza lakin vidole vinauma, nipumzike dk 15 hv then nakuja kumalizia

ITAENDELEA...

Mrejesho: Sehemu ya saba
Aisee mkuu you nailed it..Yani mpaka mwili unanisisimka.Hiki kisa kuna jamaa yangu mmoja ni msanii maarufu sana hapa tz na nje ya nchi.Kisa hiki kilimtokea sema yeye binti alimkataa jamaa na kurudisha mahali ili aolewe na mtu mwingine alitoka nje ya nchi(mbongo) na alikua na uwezo kifedha na akazaa nae mtoto mmoja wa kike.Baadae yule binti akaachika kwa yule jamaa mwingine so akawa hana direction.Ikabidi arudi kwa jamaa yangu akiwa analia anataka kurudiana nae.Jamaa akakaza vibaya mno kama ulivofanya wewe,tatizo hakua na msimamo wa kudumu.Yule demu akatishia kujiua asipomkubalia ombi lake hapo jamaa yangu akategeka na akakubali kuonana na yule binti nyumbani kwa mshikaji(kosa kubwa alilolifanya).Bahati mbaya akafanya nae mapenzi na kufungua ukurasa mpya wa mapenzi,binti akanaswa ujauzito.Wazazi,ndugu,jamaa na marafiki wa jamaa yangu walishamkataa yule binti maana alionesha dharau kurudisha mahali na jamaa alikua process ya mwisho kufunga ndoa.So ilipotokea hivo ikabidi jamaa ampeleke kwa wazazi wake kwa kisingizio cha mimba[emoji16].Kishingo upande wazazi wakakubali na jamaa ikabidi aingie tena kwenye mfumo wa yule binti bila kujua kama ana mtoto.Saizi wanaishi pamoja na kamjengea nyumba huko Kijichi na anakaribia kujifungua,,ila binti ana mambo ya ajabu sana na kamshika sana jamaa hafurukuti wala hamsikilizi mtu yeyote zaidi ya binti(inasemekana jamaa katengenezwa).Nakupongeza kwa msimamo wako japo pale kwenye kushindwa kumla yule rafiki ake binti mimi ningemtafuna siku ile ile ndio mengine yafuate[emoji23]
 
Jambo la kawaida sana. Mwanaume akitulia sawa ila akichepuka sio ajabu. Ajabu ni mwanamke kutoka nje ya ndoa yake.

Huwa inashangaza sana.

Hivi wewe leo usikie kuwa mzee wako kachepuka au usikie mama kachepuka ni ipi itakushangaza?
Yaani mwanaume kuchepuka siyo ajabu???

Nikisikia mtu amechepuka nitashangaa sana bila kujali jinsia yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alo hapo kutomla huyo rafiki yake kayumba...hapo tu lakini
Mimi naona kafanya sawa kabisa. Kajiepusha na mambo mengi. Labda hata binti na wazazi wangekuja kujua kuwa anatembea na rafiki yake na binti wangeweza kudhani labda huyo rafiki yake nae ndio sababu jamaa hataki kusikia kitu. Hiyo ingemletea shida pia huyo rafiki.
 
Yaani mwanaume kuchepuka siyo ajabu???

Nikisikia mtu amechepuka nitashangaa sana bila kujali jinsia yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa kushangaa utashangaa. Nimekuwekea mfano hapo lakini. Je ni ipi itakushangaza zaidi?

Yani ipi itakufanya ujisikie aibu wewe kama mtoto kusikia baba yako kachepuka au kusikia mama kachepuka?
 
Back
Top Bottom