Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 416
- 414
Baada ya Shirikisho la Riadha Tanzania, Kamati ya ufundi na Kocha wa timu ya Taifa , Suleiman Nyambui kumfukuza Mwanariadha Failuna Abdi Matanga,
Gidabuday alihoji uhalali wa kumfukuza Mwanariadha huyo, ndipo alipopata Vitisho na Mengine.
Gidabuday Anasimulia hapa;
Juni Mosi nilibishana sana na Kaimu KM wa RT kwa kile nachokiona ni Ubabe, Vitisho, na kutaka kuonyesha "he's superior" and can't be questioned, na Gidabuday akinyamazishwa nani atathubutu kuongea?
Naomba wajumbe wa mikaoni wote waelewe haya machache nitakayoyasema bila kurudi nyuma kwa changamoto tulizowahi kuwa nazo. Pamoja na mapungufu yangu ktk utendaji wangu wa miaka mitatu kwa kushirikiana na Viongozi wenzangu tumefanya haya hapa;
1) Kila tukipata udhamini huwa tunaita waandishi kuhabarisha umma kwamba tumepata kiasi hiki kutoka kwa kampuni au taasisi fulani na kazi yake ni hii.
2)Kambi zote za taifa ziliamuliwa na Kamati ya Ufundi na kupitishwa na Kamati Tendaji na tunafanya mpangilio wa Kambi kutembelewa na Viongozi wa Vyama vya Mikoa, lakini Kambi kama ipo Arusha ni lazima Viongozi wa Mkoa wa Arusha wahusike moja kwa moja kambini.
3)Kambini ni lazima Manager awepo, Coach Mkuu na msaidizi, Matron, mpishi na mtu wa masaji (kuchua misuli), tunawaalika waandishi wa Habari waje watembelee Kambi na hata kuwahoji wanariadha na Viongozi ili Taifa na wadhamin wajue kinachoendelea.
4)Kampala World XC 2017 tulipeleka wanariadha 29, Makocha 4 na Viongozi 3 jumla watu 36 Tanzania ikashika namba 6 duniani (wanawake), London 2017 tulipeleka wanariadha 8 Makocha 2 na Kiongozi 1 jumla watu 11 baada ya Dr Ndee kukwama kusafiri, hapo ndipo Simbu akawa wa 3 duniani na kurejea na medali tukapokelewa na JKT viongozi wa serikali wakiongozwa na Waziri wa Michezo. Denmark tukapeleka wanariadha 14 Makocha 2 na Viongozi 2 jumla watu 20 ambapo tulilipa tiket zote 20 cash dola 1900 x 20 plus allowance ya dola 100 kila mtu plus dola 1000 ya dharura, ukipiga hiyo hesabu utafahamu kwamba tulipiga kazi. Doha tukapeleka wanariadha 4 Kocha 1 na Viongozi 2 kwa ajili ya Mkutano wa WA.
5)Mambo yote hayo yalikuwa yanatangazwa na mimi au Afisa Habari ndg Tullo Chambo. Nakiri kwamba tofauti za kiuongozi na kiutendaji ndiyo ilikuwa tatizo kwetu lakini tulichapa kazi.
6)Tumeandaa Mashindano ya nchi 11 (EAAR) 2017 na 2018 Tanzania ikawa ya pili mfululizo, tulishirikisha mikoa kwa kiasi kikubwa, tulitangaza kwenye vyombo vya habari na hatujawahi kupata lawama.
Nimeyasema haya ili Kaimu KM asione mimi sikufanya kitu, wala asione ni rahisi kufuta mahusiano mazuri niliyonayo na wanariadha na Viongozi, yes kwa sababu ya tofauti kati yangu na mabosi wangu ilifanya nibambikiwe mabaya lakini naomba MKUTANO MKUU ujao nialikwe na kama Wajumbe watataka ufafanuzi ntafurahi kufanya hivyo.
Maswali yangu kwa Wajumbe wa Riadha mikaoni, wanariadha na wadau;
1)Je kwa sasahivi hayo niliyoainisha hapo juu yanafanyika?
2)Je viongozi wa mikoa hususan Arusha walishatembelea Kambi?
3)Je waandishi wa Habari (jicho la Taifa) walishatembelea Kambi?
4)Kwa bahati nzuri tunasikia serikali imedhamini Kambi, je ni shilingi ngapi?
5)Je Mashindano ya EAAR yalitangazwa? na je viongozi wa Mikoa walishirikishwa?
6) Kwanini timu ihamehame bila maelezo kwa umma? West Kilimanjaro, Olmotonyi na sasa Habari Maalum College?
7)Hii timu ni ya mtu au ni ya TAIFA? kama ni ya Taifa na inagharimiwa na Taifa basi Watanzania wanapaswa kupata taarifa
Nimeongea kama mdau bila kejeli yoyote ili haya mambo ya usiri na pale unapohoji unapewa vitisho yakome. Sisi wote tunataka nchi yetu isikike ulimwenguni.
Waraka wangu huu haujagusa Utawala wa RT bali Utendaji wa RT; hata hivyo Utendaji unaposuasua Utawala utalaumika. *Mhe Kaimu Katibu Mkuu bado ana nafasi nzuri sana ya kuyarekebisha haya tusonge mbele.
"Mnyonge mnyongeni - Haki yake mpeni"
Gidabuday, W.F.
Juni 2/2022.