Riba za mikopo kwa watumishi, CRDB na NMB

Riba za mikopo kwa watumishi, CRDB na NMB

RIBA KATIKA UISLAM
Kwa mujibu wa Qur’an tukufu, kuchukua riba ni dhambi ambalo linasababisha adhabu kali kabisa kutoka kwa Allah swt. Adhabu za kuchukua na kutoza riba ni kali kabisa kuliko madhambi mengine. Kama ilivyoelezwa katika Surah Aali Imran, 3, : 130 - 131:
‘Enyi Mlioamini! Msile riba, mkizidisha mara dufu kwa mara dufu; na mcheni Allah ili muweze kuwa na ufanisi’
‘Na ogopeni moto wa Jahannam ambao umetayarishiwa makafiri.’
Inamaanisha kuwa ukali wa moto ambao umetayarishwa kwa ajili ya wale ambao huchukua riba kama vile moto utakavyokuwa mkali kwa ajili ya makafiri.
Allah swt anatuambia katika Surah al Baqarah, 2, Ayah ya 275 :
‘ Wale wanaokula riba, hawasimami ila kama anavyosimama yule ambaye Shaitani kamzuga kwa kumsawaa; na haya ni kwa sababu wamesema, ‘biashara ni kama riba’, Allah ameihalalisha biashara na kaiharamisha riba. N a aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake, kishaakajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali) aliyoipata; na hukumu yake iko kwa Allah. Lakini wanaorejea (kula riba) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele.
Mkuu tuondolee hadithi zako zisizo na uhalisia, sisi tunazungumzia kukopa fedha na kurejesha fedha, nyie mnadai hamna riba lakini nikopeshe milioni kumi nirejeshe baada ya miaka mitano bila riba hutanipa. Technique inayotumika ni kuniuliza nataka kununua nn na hiyo 10m, nikisema nataka kununua kitu X unaenda kuninunulia hicho kitu kwa kuweka cha juu, say 3m then unanidai 13m alafu unadai hujanidai riba. Akili za kuambiwa changanya na za kwako. Mm nataka unikopeshe 10m nikurejeshee 10m after sometime! Hapo ndio interest free, vinginevyo ni blah blah tu
 
Waulize kwanza mnatumia straight or reducing balance method...anzia hapo kwanza
 
RIBA KATIKA UISLAM
Kwa mujibu wa Qur’an tukufu, kuchukua riba ni dhambi ambalo linasababisha adhabu kali kabisa kutoka kwa Allah swt. Adhabu za kuchukua na kutoza riba ni kali kabisa kuliko madhambi mengine. Kama ilivyoelezwa katika Surah Aali Imran, 3, : 130 - 131:
‘Enyi Mlioamini! Msile riba, mkizidisha mara dufu kwa mara dufu; na mcheni Allah ili muweze kuwa na ufanisi’
‘Na ogopeni moto wa Jahannam ambao umetayarishiwa makafiri.’
Inamaanisha kuwa ukali wa moto ambao umetayarishwa kwa ajili ya wale ambao huchukua riba kama vile moto utakavyokuwa mkali kwa ajili ya makafiri.
Allah swt anatuambia katika Surah al Baqarah, 2, Ayah ya 275 :
‘ Wale wanaokula riba, hawasimami ila kama anavyosimama yule ambaye Shaitani kamzuga kwa kumsawaa; na haya ni kwa sababu wamesema, ‘biashara ni kama riba’, Allah ameihalalisha biashara na kaiharamisha riba. N a aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake, kishaakajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali) aliyoipata; na hukumu yake iko kwa Allah. Lakini wanaorejea (kula riba) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele.
Biashara yoyote ambayo utanunua kitu kwa 5000 na kuuza 6000 basi ni haramu.
Biashara ya fedha ni biashara kama biashara zingine unapewa pesa ambayo hujaifanyia kazi ukae nayo miaka 6 halafu uirudishe kama ilivyo???

Bank wanazosema hawatozi waislam riba ni usanii. Wanakuuliza unataka kununua nini? Labda ni pikipiki ya milioni 2 hawakupi hiyo hela wanakununulia hivi: wanaziagiza nyingi kwa bei ya jumla kisha wanakupa kwa bei kama ya walanguzi wengine hii ni riba pia.
 
Dah bas tu tunakuwaga no option, ila mikopo ya benki ni utumwa sana, yaan unakuta unarejesha pesa karibia mara mbili ya uliyokopa

Na bank zinawapenda sana wakopaji ambao makato ni kwenye mshahara, marejesho yao hayana usumbufu kabisa
 
Milioni kumi na mbili,baada ya miaka mitano milioni 22 na laki mbili au,?? ,,,poleni mnaokopa ,,,
Na apo bado bima ya mkopo na application ya mkopo ambayo uwa ni asilimia kama 1.5 ivi sasa apo sijajua wanakata Kwa starting point au na miaka inayokuja
 
Kopa kwa sababu maalum
tapatalk_1515828571630.jpeg
 
Biashara yoyote ambayo utanunua kitu kwa 5000 na kuuza 6000 basi ni haramu.
Biashara ya fedha ni biashara kama biashara zingine unapewa pesa ambayo hujaifanyia kazi ukae nayo miaka 6 halafu uirudishe kama ilivyo???

Bank wanazosema hawatozi waislam riba ni usanii. Wanakuuliza unataka kununua nini? Labda ni pikipiki ya milioni 2 hawakupi hiyo hela wanakununulia hivi: wanaziagiza nyingi kwa bei ya jumla kisha wanakupa kwa bei kama ya walanguzi wengine hii ni riba pia.
Kuna wapiga debe wa benki fulani walikuwa wanainadi hiyo mikopo isiyo na riba wakidai haina riba bali wanaweka faida. Nikajiuliza tofauti kati ya riba na faida nikakosa jibu. Nikamwuliza, nikikopa milioni kumi (fedha) kwa miaka 6 na pia nikakopa vifaa vya milioni kumi Kwa miaka sita vile vile nitarudisha kiasi gani at the end of the day kila upande? Sikuona tofauti ya maana. Haya mambo ya riba au no riba ni maneno tu
 
Milioni kumi na mbili,baada ya miaka mitano milioni 22 na laki mbili au,?? ,,,poleni mnaokopa ,,,

Milioni 22 baada ya miaka 5 ni hela kidogo sana muhimu ni kukopa kwa malengo.
Baada ya miaka 5 hiyo milioni 10 uliyokopa sitegemei kama ukiingiza kwenye mzunguko wa biashara kama itakuwa chini ya milioni 40.

Nakupa mfano halisi kama ifuatavyo;
Chukua hiyo milioni 10 kwa sasa wekeza kwenye biashara ya mpunga.
Gunia moja la debe 10 Tsh 70000 jumlisha10000(usafirisha, uhifadhi, na kukoboa)

Toa milioni moja kwa ajili ya matumizi utakapokuwa site unakusanya mzigo.

9000000/80000~ gunia 112
Kaweke stock huu mzigo uuze ukiwa umekobolewa kuanzia December hadi March
Gunia moja linatoa kilo 85 za mchele na kila kilo uza kwa 1600 bei ya kawaida kabisa.

112*85*1600~ 15M
Hii ni kwa mwaka mmoja.
Ukiendelea na biashara hii baada ya miaka 5 hela hii itakuwa chini ya 22M?
Tatizo tunakopa bila malengo au bila kuwa na uelewa wa kile unachoenda kukifanya.
Biashara yoyote ili ifanikiwe inahitaji usimamizi wa karibu. Sasa shida unakopa unamwachia mtu akusimamie mkopo wako hiyo nayo ni changamoto nyingine.
Kimsingi mkopo ukiusimamia vema unalipa na muhimu unatakiwa uwe angalau na experience ya unachoenda kukifanya. Mkopo sio wa kufanyia biashara ya majaribio.
 
Napata wakati mgumu kuelewa, hizi bank ukienda kuuliza riba ya mkop wa kias flan ni sh ngap.. Wanakujibu kwamba ukichukua kiasi flan let say 13m rejesho lake ni kiasi flan.... Bila kukuambia actual riba. Sasa naomba wenye ufaham zaid kwenye hii issue.

CRDB ni 16% Per Annum/Kwa Mwaka + 1% Insurance/Bima ! Hivyo jumla ni 17% Per Annum ! Pia wana Gharama za mkopo/Loan Fee !
 
Back
Top Bottom