Mpaka sasa sijaona habari kamili inayoelezea chanzo cha kuachana kwao.....zaidi ya vilio vya mabinti dhidi ya huyo bwana mdogo......utadhani labda wao ni malaika......
Sijui ni kwanini wanawake wanapenda kujiweka kwenye upande wa kuonewa kila kwenye scene ya mapenzi......!!???
Yaani wanapenda kuonekana innocents hata kama wana makosa.....wanapenda kuonekana wanaonewa hata kwenye mambo ya kipuuzi wanayoyafanya.....!!
Ukweli wote anaufahamu huyo bwana mdogo na huyo mpenzi wake......mambo ya ndani ni mambo ya siri ya watu.......
Kuna jamaa alikwa anampiga mkewe kila siku na mkewe alikuwa wala haendi popote....na pia jamaa akawa mlevi wa kupindukia huku mkewe akiwa hasemi chochote.....tulipokuja kufahamu sababu ya jamaa kuwa vile....hapo hapo tukampa cheo cha ujemedari wa uvumilivu.......
Kuta nne za chumbani zina siri nyingi......watu wanaachana baada ya kuvumiliana kwa muda mrefu....na sio kwa kukurupuka......