Richard bingwa wa migogoro mwanzo mwisho.

Richard bingwa wa migogoro mwanzo mwisho.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Historia yake ni mitifuano tangu FAT na sasa TFF. Hivi hakuna kazi ingine anawezafanya? Tumechoka kusikia majina yaleyale miaka ndenda rudi huku mpira wetu ukiendelea kubaki palepale.
 
Hapana mi namtetea, Tatizo la Wambura ni kuzisimamia fedha ipasavyo na hapo ndipo anapoanza migogoro na wenzake kwani yeye huwa na misimamo sana.

Nakumbuka enzi za FAT, ilikuwa mechi ya Simba na Yanga ndio ilikuwa upigaji wa kufa mtu, mechi inaisha kwa kuingiza mil 8 au kumi.Alipokuja Wambura akaweka mabaunsa zikapatikana karibia ml 41, nakumbuka mechi hiyo Yanga alilala. Mechi zilozofata zote hakuna iliyoingiza chini ya ml 80.

Pale Simba alifungiwa kisa kukataa Simba isitegemee kamati ya akina Aveva na Kaburu na itumie mapato yake, kilichomkuta ndicho hiki kinamkuta tena TFF akiwa mwenyekiti wa kamati ya fedha.
 
Huyu jamaa huwa nashindwa kuelewa kila sehemu anawekewa zengwe.

Tatizo ni yeye au wanaomwekea zengwe?
 
Back
Top Bottom