Richard Sorge: Jasusi aliyeamua hatma ya Vita kuu ya pili ya Dunia

Richard Sorge: Jasusi aliyeamua hatma ya Vita kuu ya pili ya Dunia

Habari za weekend wanajukwaa natumaini wote wazima bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada ya leo.
View attachment 840492

UTANGULIZI
Richard sorge a.k.a Ramsay alikuwa jasusi wa urusi ya zamani yaani Jamhuri ya kijamaa ya soviet (USSR) na alitumika wakati na kabla ya vita kuu ya pili ya dunia akiwa kama mwandishi wa habari huko ujerumani ya wakati wa hitler na japan akikusanya taarifa mbalimbali ambazo zilikuwa muhimu katika kuamua hatma ya vita kuu ya pili ya dunia na anatazamiwa kuwa moja ya majasusi muhimu zaidi katika historia ya tasnia hiyo.
View attachment 840473
Sorge alizaliwa nchini arzebaijan (iliokuwa chini ya Urusi) kwa mzazi wa kijerumani na mama wa kirusi mwaka 1895 na Baba yake alikuwa mhandisi wa uchimbaji madini huko Baku,Arzebaijan ila baadae wakarudi ujerumani. Alipofika miaka 18 alijiunga na jeshi la ujerumani na kupigana vita kuu ya kwanza ya dunia mwaka 1914 ila bomu lilimjeruhi vibaya mikono na miguu hivyo baadae aliachishwa jeshini. Wakati huu ndio ulibadilisha taswira nzima ya maisha yake maana aliingia kwenye tafakuri ndefu na kusoma vitabu vya kijamaa (karl marx) akaona alipigana vita isiyo na maana sababu hivyo akaamua kujiunga na sera za kijamaa/kikomunisti ambazo kwa muda ule zilikuwa zinatamalaki Urusi na wakati huo anahitimu masomo ya uchumi na baadae Siasa ngazi ya PhD akajiunga na chama cha kikomunisti cha ujerumani ila baada ya msimamo yake mikali alitimuliwa na akaamua kuhamia urusi ambako huko alichukuliwa kuwa jasusi wa Urusi ila aliyevaa uandishi wa habari mwaka 1924.

MISSION ZAKE
Moja ya mission zake akiwa kama jasusi wa urusi ilikuwa kupandikizwa china 1930-32,ujerumani na uingereza (1929) na japan 1933 ambapo kote huko alikuwa mwandishi wa habari mahiri na aliaminika hivyo kuwa nafasi nzuri ya kupata taarifa nyeti. Mfano ujerumani alikuwa mshabiki mkubwa wa hitler na alisoma vitabu vyake na kujichanganya na chama chao cha NAZI na aliaminika kiasi hata kiongozi mwandamizi wa NAZI Joseph goebbels alihudhuria sherehe ya kuagwa kwake pale alipotumwa kwenda kuripoti habari za japan kwa ajili ya magazeti ya ujerumani. Hivyo ushawishi wake huu ulimbeba hata alipoelekea japan ambapo alikuwa muandishi maarufu zaidi wa ujerumani maana Frankfurter Zeitung lilikuwa gazeti maarufu zaidi ujerumani na kikubwa zaidi akapewa cheo kisicho rasmi cha kuwa mshauri na msaidizi kwa balozi wa ujerumani huko japan!!! Yaani jikoni kabisa kiasi hata mipango ya kivita na kisiasa ya ujerumani ililetwa kwake ili amshauri balozi!!!

Pia akiwa japan alikuwa mkandiaji wa siasa za Urusi na alishabikia sana utawala wa kidikteta wa japan na Ujerumani hivyo kupendwa sana na mataifa hayo maadui wa Urusi. Akiwa huko alitengeneza timu ya watoa taarifa wake ambao walijipenyeza kwa kufungua biashara kubwa mwingine alifanyia kazi kampuni ya habari ya ufaransa n.k hao wote ndio walikuwa wakiongoza genge la majasusi hao urusi ambapo walifanikiwa kudukua siri nyingi za Hitler na Emperor Hirohito ambapo ziliisaidia Urusi kushinda vita kuu ya pili ya dunia.

UMAARUFU
Sorge ametambulika zaidi kwenye dunia ya kijasusi na inteligentsia kwa taarifa zake mbili muhimu zaidi ambazo ndio ziliamua kwa namna moja ama nyingine ushindi wa Urusi na kuangushwa kwa Adolf Hitler. Mwaka 1941-42 akiwa japan aliweza kuvujisha mpango wa Hitler kuvamia urusi hivyo ikawapa nafasi Urusi kufanya maandalizi mapema ya kimbinu kupambana na Hitler hivyo alipovamia haikuwa mshtuko zaidi waliweza kumzuia na mwishowe kumtandika na kumfurusha hadi ujerumani.

Ikumbukwe wakati huo wa uvamizi wa Ujerumani huko urusi ukiwa umepamba moto hasa battle ya "operation barbarossa" ambapo urusi ilionekana kuzidiwa jasusi huyu aliweza kudukua taarifa kuwa mshirika mkuu wa Hitler yaani Japan hana mpango wa kuingia upande wa hitler kuvamia Urusi maana alishapanga kuivamia marekani na uingereza huko pacific. Taarifa hii ilikuwa muhimu ikizingatiwa mnamo miaka ya 1930s japan ilishavamia jimbo la manchuria huko china ambalo lilikuwa linatawaliwa na Urusi na hivyo urusi ilimuona japan ni tishio kuliko ujerumani ukizingatia kwenye vita ya russo-japanese mwaka 1905 urusi alipigwa vibaya sana na wajapan hivyo walikuwa wamejaza majeshi kwenye mpaka wa mashariki ili kujihami na uvamizi wa majeshi ya japan.
View attachment 840490

Hivyo, uwepo wa taarifa hii muhimu ilisababisha warusi waondoe vikosi zaidi ya 18 yaani wanajeshi takribani laki 2 kutoka huko siberia iliyo karibu na japan na kuvielekeza moscow ambapo vilienda kuongeza nguvu kwa vikosi vilivyokuwa vinamzuia hitler kuivamia moscow na vikosi vile vilipowasili vilileta nguvu mpya na hivyo kumzidi nguvu hitler na ndipo ujerumani akachakazwa na tokea hapo nguvu yake ikamalizwa na mwishowe akapinduliwa na Urusi, yote haya ni kutokana na intelijentsia iliyotukuka ya bwana sorge.

MWISHO WAKE
Richard sorge mwezi mmoja baada ya kutoboa siri hii ya japan kwa Urusi na ambapo ujerumani alitandikwa, polisi walifanya msako mkali sana na inasemekana kuna mmoja wa kikundi chao alisaliti kwa kutoboa siri ya Sorge kuwa ni communist mwenzao!! Baada ya kukamatwa waliwekwa gerezani baada ya mateso makali mnamo November 7, 1944 Sorge na mwenzake alieitwa ozaki walinyongwa kwenye gereza la sugamo na ili kuwaumiza zaidi waliwanyonga siku ya kuadhimisha siku ya mapinduzi ya kikomunisti ya urusi. Na huo ndio ukawa mwisho wa maisha ya jasusi huyu wa kirusi.

HITIMISHO
kuna mengi sana ameyafanya huyu mtu ila mengi yanatufundisha kuwa unaweza toa kafara furaha yako kwa ajili ya furaha ya wengine kama ambavyo sorge licha ya kuonywa aondoke Japan aligoma na hata kutumia pesa binafsi ili kuendesha genge lake maana alisukumwa na uzalendo kwa urusi na ndio maana hata alipokamatwa hakujuta wala kulialia aokolewe bali alifurahi maana alikuwa ameokoa nchi yake dhidi ya uvamizi wa kijeshi. Ila ambacho hakijapata majibu ya kueleweka je ni kipi hasa kilisababisha agundulike ilihali miaka yote 9 hakuwahi kushtukiwa i hope great thinkers wote humu mtanisaidia hapa

Naomba kuwasilisha

View attachment 840494
aisee huyo jasusi kweli alikua na moyo mgumu, maana miaka ile kuwa mCommunist alafu ukaenda kujichanganya na wajerumani sio mchezo,

alafu inawezekana na ujasiri wake ulitokana na kwamba alishawahi kuishi ujerumani na kuwapigania vita kabisa....hasira ya kufukuzwa pia labda ilimfanya atake kuangusha utawala wa hitler,

sasa hapo kwenye ilikuaje akakamatwa lazima patakua na siri, haya mambo ya ujasusi kutoana kafara ni kawaida sana...huenda labda baada ya kufanikisha ushindi wa vita ile kubwa hakuitajika tena maana kumbuka pia jamaa alikua na asili ya mataifa yote mawili hapo....na mataifa yote yanajua umahiri wake na misimamo yake,

wanasema "prevention is better than cure" waRusi naona walijihami mapema labda....sina uhakika lkn.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachosema ni kweli mkuu haya mambo ya ujasusi wakishakutumia wanakuwa hawakuamini tena wanaweza kukutoa kafara ikumbukwe huyu jamaa akiwa kizuizini wajapan waliweka mpango na warusi kwamba wabadilishane maspy wao waliokamatwa ila cha kushangaza alikataa dili hili maana alihisi jama anaweza kurudi kumbe akawa double agent!!! Hivyo wakaona wasimuokoe pia ukizingatia baba yake ni mjerumani naona hawakutaka kumuamini kabisa. All in all hawa jamaa huwa wana kazi ngumu sana ila cha kushangaza sifa zote wanapewa wanasiasa ilihali 80% ya mzigo wanaubeba majasusi.
 
wanaisasa ni wahuni tu...wanawatumia wengine kwa manufaa yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nataman siku zije story za majasusi wa Tanzania ambao waliisaidia nchi kwa namna moja au nyengine mpka tukafanikiwa jambo fulani. Maybe hatuna hao majasusi huku kwetu

sent using samsung galaxy s8
Wapo wengi tu,waulize makaburu wa south afrika,msumbuji,commoro,idd amini wa uganda,huwezi pigana vita bila ya kua na taarifa za uhakika za adui yako ukashinda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu zitto junior bandiko lako zuri na linafikirisha. Taarifa zinasema urusi USSR ya wakati ule waliweza kusalimika kutoka kwa jeshi la Hitler kutokana na hali ya hewa na si ubora wa jeshi lake. Inasemekana kulikuwa na baridi kali sana. Kuna ukweli hapa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hii sababu imekuwa ikirudiwa na wachambuzi wa masuala ya kijeshi kwamba kama Hitler angeshambulia baada ya msimu wa baridi basi angempiga Stalin!!! Naweza kukubali kwamba Ujerumani alikuwa ana silaha na mbinu bora kuliko Urusi lakini pia tukumbuke chanzo hakikuwa hicho pekee kwa sababu ikumbukwe hitler alivamia Urusi kwa mara ya kwanza majira ya joto june,1941 kupitia mission ilioitwa operation barbarossa ila kuna wakati walikaribia moscow lakini hitler aliwaambia wasubiri kwanza na wavamie Kiev,ukraine hivyo wengine wanasema hiyo Subiri subiri ndio ilimponza hitler urusi na sio baridi hata kidogo sababu aliwapa muda wa kujipanga upya.

Ilipofika october hitler aliamua wavamie rasmi moscow (Baridi halijaanza). Walipovamia wakafika kilometer chache tu nje ya jiji lakini hali mbaya ya hewa hasa mvua ndio iliwakwamisha lakini pia ujerumani ilikuwa tayari inapigana maeneo mengi hivyo supply kama mafuta,chakula,silaha na watu ikawa ngumu kufikiwa haraka kwa misaada hiyo tofauti kama angeamua kuvamia urusi kwanza ndipo aanzishe vita nyingine maeneo mengine ssa akawa anapigana kuanzia Afrika mpaka ulaya magharibi, kaskazini na sasa ulaya mashariki yaani ni vita kila upande hii pia ilichangia sana kuwamaliza nguvu kiasi kwamba baridi lilipokuja ndio likamaliza kila kitu.

Pia hata wakati wa baridi ulipofika ujerumani bado waliweza kusogea mpaka kilometer 8 kutoka moscow ila walishakuwa wameishiwa supply za kutosha na hata majenerali waliposema waretreat ili wajipange upya hitler alikataa hivyo warussia walipo counter-attack waliweza kummaliza kabisa nguvu ujerumani za kushambulia tena na tokea hapo ujerumanu haikuweza kurudisha nguvu zake

Kiufupi maamuzi mabovu ya hitler,kupigana vita nyingi kwa wakati mmoja,ukubwa wa ardhi na wingi wa watu urusi na ikichangiwa na hali ya hewa ndio ilipelekea ujerumani kupigwa ila tukisema baridi pekee haitakuwa kweli maana walishaanza shambulia wakati wa kiangazi

Labda mtaalam Malcom Lumumba atupe maoni yake
 
Mkuu zitto junior hongera kwa bandiko zuri, tunahitaji mabandiko kama haya.
Naomba nisiseme sana lakini ni kwamba NKVD walikuwa wametambaa dunia nzima wakieneza ukomunisti hasa baada ya Stalin kuwa kiongozi ndiyo wakafika hadi Marekani. Kuhusu kukamatwa hao majasusi wa Urusi kikubwa ni kwamba Ujerumani kabla ya vita alikuwa anashirikiana na Uingereza na Ufaransa (Anti Communist Coalition) katika kupambana na ukomunisti barani ulaya. Jambo jinge ni kwamba Ujerumani alikuwa na shirika la kijasusi la kijeshi kama The Abhwer ambalo liliundwa tokea kipindi cha wakina Kaiser Wilhelm na kuja kufahamika rasmi mwaka 1921 . Ukisoma harakati za Abhwer utakuja kushangaa kwamba walikuwa na mtandao mzito sana barani ulaya hata kabla ya vita ya kwanza ya dunia, na baada ya kuchukua madaraka mwaka 1933 Hitler aliendelea kulitumia hilo shirika mpaka mwaka 1945.
 
Mkuu nimekuelewa sana ila najiuliza hivi inakuaje system zina rely kwenye taarifa za spy moja kiasi anaweza kuwa double agent na kuwauza.... Mfano sorge hapo ingekuwa amewauza kuwa japan hawatovamia urusi in the near future hivyo wangehamisha majeshi yote moscow ssa ingetokea Japan anavamia siberia si ingekuwa catastrophic?? Kwa faida ya sote humu unaweza kutusaidia jinsi wanavyoweza kuhakiki uhakika wa taarifa za kijasusi kabla hawajazikubali maana inashangaza jinsi gani mtu anaweza kuwa pandikizi wanashindwa kugundua na wanaamini taarifa zake bila kuwaza mara mbili.

Cc Richard
 
Hahaha,
Mkuu Zitto kule Japan George hakuwa peke yake, kulikuwa na jasusi mwingine kama Hotsumi Ozaki ambaye alikuwa mshauri wa Waziri Mkuu wa Japan. Kikubwa zaidi Intelligence Bureau huwa zikipata taarifa huwa hawazifanyii kazi moja kwa moja tu inabidi zichambuliwe na zithibitishwe halafu yafanyike maamuzi.

Pia jasusi anapopelekwa kufanya kazi sehemu mara nyingi lazima hasa nje ya mipaka lazima huwa anakuta mazingira yameshaandaliwa na Jasusi Mkazi (Resident Spy) au Handler ambao mara nyingi huwa mabalozi au maafisa ubalozi. Hivyo taarifa nyingi za kijasusi huwa hazitoki kwa jasusi moja kwa moja kwenda kwa mkuu wa nchi, bali hutoka kwa jasusi (Field Officer) kwenda kwa Jasusi mkazi (Resident Spy) ambaye yeye na jopo lake ambao wako kwenye nchi ya adui huweza kufanya uthibitisho wa taarifa.

Kikubwa jasusi kama Sorge huwa hafanyi kazi peke yake bila kuwa anafuatiliwa au mashirika ya kijasusi kuwa na leverage kwake. Ndiyo maana anaweza kuwa yuko Japan lakini familia yake iko Moscow, akituma taarifa za wongo imekula kwake. AU NKVD na KGB walikuwa na mchezo wa kufanya recruitment kwa njia ya Honey Trap au Rushwa. Ambapo wanakulazimisha uwapelekee taarifa au wanavujisha mauchafu yako. Kuna jasusi wa MI6 aliwahi kufanyiwa hivyo: Sasa kwa mwendo huo sidhani kama litakuwa jambo la busara kuwadanganya waliokutuma.
 
Back
Top Bottom