USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 10,904
- 26,184
Balozi wa USA Mark Green kipindi cha Richmond aimbia dunia kuwa kilichomponza Lowassa ni kuonekana ni tishio kwa wanaotazamiwa kumrithi Kikwete (alipaniwa).
Hapa kuna mtu anayeonekana kuwa frontline kumrithi Magufuli kwa uwezo, utendaji, dini, ukanda na umri, Kassim Majaliwa anazunguka zongo linalomuandama la magari ya kufru yaliyopitishwa chini ya ofisi zake, yalipitishwaje na mtu anayeonekana yupo makini sana walioko chini yake wanamnyooshea kidole.
Akihojiwa na tume ya Dkt. Mwakyembe na baadae bungeni aliyekuwa naibu waziri wa nishati na madini wa wakati huo Ibrahim Msabaha anasema "Naona mimi nitakuwa mbuzi wa kafara kwa hili " maDED wote wanasema ihojiwe ofisi ya waziri mkuu wao wasiwe mbuzi wa kafara.
Kama umemsiliza waziri mkuu kule Mwanza anaona kuwa wenye makosa ni walioitisha ombi la ununuzi wa magari hivyo wawajibike baada ya uchunguzi, walioagiza wanasema shida sio wao kuomba maana ombi lina kukubaliwa na kukataliwa hivyo aliyelipokea na kuidhisha ndie mchawi hapa na huyu si mwingine ni ofisi ya waziri mkuu.
"Tulifuata utaratibu wa ununuzi wa umma kuanzia kwenye kamati ya halmashauri, baraza la madiwani, wizara ya ujenzi na baadae ofisi ya waziri mkuu" DED wa Geita anaongea kwa kujiamini kuwa kwa nini walipewa na aliyetoa anasema kwanini waliomba, kuna utata hapa.
Watanzania hawataki kujua mambo ya nani aliomba na nani alitoa wanataka kufahamu kwanini pesa zao million 400 zote zinunue gari la mtu mmoja tu huku wakiwa na matatizo chungu mzima.
Rais anaonekana yuko wa wananchi wanaolia pesa zao kufujwa na kutaka waliohusika wawajibishwe, waliohusika wanarushiana mpira.
Kwa kuwa hofu kuwa Majaliwa anaandaliwa hakuna anayeweza kumhoji na badala yake yeye ndio anahoji (hapa kuna utata).
Maadui wa Majaliwa kisiasa wanaojipanga kuelekea 2025 wanakesha wanachochea kuni ili kitumbua kiiingie mchaga.
My take; Ule msemo wa kuwa waziri mkuu wa Tanzania hawezi kuwa Rais unaweza ukajitokeza hapa tena!
Soma