Suala la Richmond kurudi bungeni, naliona kwa mtazamo tofauti kidogo.
Kwanza imelenga kumsafisha EL, Kwasababu zipo tetesi kuwa toka awali mama Makinda aliposhawishiwa na kundi la EL kugombea uspika, nia ilikuwa ni kumpata mtu atakayeirudisha Richmond bungeni ili sitta , mwakiyembe na kundi lao waonekane walichemsha ktk kulitia taifa hasara, kuleta migogoro isiyoisha ndani ya chama na serikali n.k.
Pili nachelea kusema kuwa Mnyika katumwa!!, ama kwakujua au kwakutokujua. nitaeleza.
Ikiwa katumwa akiwa anajua. Hii huenda ni dhamira ya chama chake (chadema). Kuwa, kimemtuma apeleke hoja hiyo ya Richmond bungeni ili EL asafishwe ili chadema ijihakikishie ushindi 2015 endapo ccm itampitisha El, kwakuwa wamekuwa wakiamini kuwa nguvu ya El kwa Umama ni ndogo ukilinganisha na nguvu ya cdm.
Pia upo uwezekano wa mnyika kutumwa bila ya yeye (mnyika) kujijua kwamba katumwa. El ni mtu anayefanya siasa za kiwango cha juu sana, ana mtandao mpana sana vijana kwa wazee, ndani ya chama chake na ndani ya vyama vya ushindani (upinzani), hivyo ni rahisi hoja hii ya Richmond kufikishwa kwa mnyika kupitia kwa marafiki zake (mnyika) au hata yeye mwenyewe kwa namna moja au nyingine bila Mnyika kulitambua hilo.
Naamini hoja hii ya Richmond kurudishwa bungeni, haikosi mkono wa mafisadi. Naamini hoja hii ilifikishwa kwa Mnyika bila ya yeye kujua, akidhani hoja imeletwa na wazalendo wenzake. Lakini yote kheri coz it is just a political strategy for both political party!!.