Wakati mwingine hatuhitaji kujua mchakato wa upataji fedha za kuendeshea miradi kwa sababu Magu anajenga taifa, hajinufaishi yeye mwenyewe. Ninachohisi ni kuwa fedha hizo zimeenda kwenye ujenzi wa reli na ununuzi wa ndege pamoja na miradi inayoendelea. Mwisho wa siku tutaona reli, barabara, ndege na stiglar george dam vyote hivyo si vya Magu bali ni vya kwetu hata ww utazitumia. Ukiniuliza mm mwananchi wa kawaida jinsi gani mchakato wa kupata hela umepitia sihitaji hilo. Ila nyinyi ambao michakato inawafaidisha hamtaacha kuuliza hasa pale ambapo pesa haitapitia bungeni kuna watakaokosa posho na ndio watakaopiga kelele.
Kama Rais ni mzalendo anataka kujenga nchi atumie tu tuone matunda michakato baadae
Watanzania ni kweli matajiri;
but wa akili za kijinga siyo mali;
Ni walewaleeee!
Hiyo miradi yooote ni kizunguzungu tu na kufaidisha makampuni mama ya wazungu nje, laiti ingekuwa ni teknorojia yetu,weusi ningefurahi sana. au hata angenunua hizo ndege S/Africa, au Nigeria, Equatorial guinea ningempa big up. Watanzani walivo mazuzu wanashangiliaaa ndege na blinded cheers nyiiingi ,ambapo kamwe hawatakaa wafaidike wao?.
Naamini Daktari binafsi bila familia wa kawaida wa serikali anaeishi Dar, tuseme mfano Temeke hosp, hawezi tumia mshahara wake km nauri ya ndege. kwenda na kurudi (Musoma - Dar,! ) hata kwenda tuu! hautoshi na atatesa familia, labda ale rushwa sana, Narudia ale rushwa sana, hao ni wenye mishahara ya serikali, je wewe mleta mada si ndo kabisa.
Unanunua Ndege kwa mkoloni? sijui treni la umeme, adui yako? lazima tena anakupa kibovu, sababu hakupendi japo! yatamfia kabla ya kuondoka! richa ya hapo yeye mzungu akale wapi? ili akukule vizuri utakuwa mtumwa wa kununua vipuri na mafuta mpaka Yesu arudi.
African huna akili japo ya kutengeneza vipuri kutokana na matrekta machakavu,
Bora angekula sambamba na wavumbuzi wa machines za viwandani kwa njia zetu weusi wenyewe, wapo vijana wanafanya kazi nzuri sana, km mgari wetu ule wa Nyumbu,Ndege tena za mianzi. Bwire manyonyi aligundua namna ya kulifumua trekta na kulisuka upya kwa kuweka vyuma vya Dhahabu ndani ili lidumu miaka mingi. alihitaji msaada kidogo tu , but imezimwa. kingine Miundo mbinu iliyopo uiboreshe tu, pia Wafugaji, na wakulima mashambani, hayo tunayamudu.
Drop iririgation ni wazo la mtanzania huyuhuyu bwana Bwire manyonyi, lkn wazungu ndo wanamiliki hii teknolojia. viongozi wa Bongo walijichekesha chekesha tu wakimpongeza kinafiki, bila msaada akaigawa kwa Israel kwa $ kibao mpaka leo, na harudi huyo tena.