Kulikuwa na mjadala mkali na wabunge karibu wote waliozungumza, ukiacha Karamagi, walipingana na ripoti ya serikali inayoonyesha kuwa maofisa wa serikali (Hoseah na Mwanyika) hawakukutwa na hatia yoyote. wabunge wamesema kuwa hawakubaliani na njama za serikali kuwasafisha watu ambao ripoti ya kamati teule ya bunge ilionyesha wazi kwua walikuwa wamefanya makosa.
lakini Sitta nadhani ameiokoa serikali kwani alipoona wabunge wanazidi kuchachamaa, alisitisha mjadala, akashauri kuwa kamati ya madini ikae na kuandaa ripoti ya nini kinachopaswa kufanywa na serikali ili kikao kijacho hoja hiyo ndio imalizwe. Ngeleja alikubali ghoja hiyo kwa niaba ya serikali na shelukindo, mwenyekiti wa kamati, naye akakubali, na wabunge wote nao wakakubali.
Hivyo ngoma ya Richmond hadi Novemba
Mjdala umezizima au umezimwa?
Kha hivi huwa wanafanya rehearsal za hii mijadala siku moja kabla kwenye caucus?
Eti mjadala utafungwa November, mbona hawakuuongezea siku kama ule wa elimu?
Huyu mzee wa Urambo bwana ana matatizo .Au ndiyo njia ya kutaka Ulinzi uongezwe ?Kila mara lazima aibuke na kuzima issues .
Hakuna siri katika mambo ya kitaifa. Kwani ukificha leo , lakini kesho atatokea mwandawazimu na kuyafunua yooote. hata ikipita miaka 50 lakini lazima watashitakiwa.
Ndiye mwenyewe.Yule mama aliyeongea kwa uchungu kabla ya Karamagi ndio Stella Martin Manyanya?
Hii danadana ya Richmond, Kiwira na North Mara kwa mwendo huu itaisha Novemba?
Mkuu Kumbuka limo la USD 300,000, kumbuka pango la dola 8,000 kwa mwezi.....and the list goes on....unadhani atawasahau wanaomwezesha ki hivyo?
Sawa mkuu ila "justice delayed is justice denied". Wewe unaonaje?