Richmond yazizima mjengoni

Richmond yazizima mjengoni

PhD

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Posts
4,692
Reaction score
3,891
lile sakata la Richmond inaendelea huko mjengoni mjadala umekuwa moto kweli ya lowasa yanaweza kujirudia???
 
Kuzizima means nini? Nani na anasema nini ? Yapi yanaweza kujirudia una maana Pinda apinden naye ?
 
Kulikuwa na mjadala mkali na wabunge karibu wote waliozungumza, ukiacha Karamagi, walipingana na ripoti ya serikali inayoonyesha kuwa maofisa wa serikali (Hoseah na Mwanyika) hawakukutwa na hatia yoyote. wabunge wamesema kuwa hawakubaliani na njama za serikali kuwasafisha watu ambao ripoti ya kamati teule ya bunge ilionyesha wazi kwua walikuwa wamefanya makosa.
lakini Sitta nadhani ameiokoa serikali kwani alipoona wabunge wanazidi kuchachamaa, alisitisha mjadala, akashauri kuwa kamati ya madini ikae na kuandaa ripoti ya nini kinachopaswa kufanywa na serikali ili kikao kijacho hoja hiyo ndio imalizwe. Ngeleja alikubali ghoja hiyo kwa niaba ya serikali na shelukindo, mwenyekiti wa kamati, naye akakubali, na wabunge wote nao wakakubali.
Hivyo ngoma ya Richmond hadi Novemba
 
sasa linaunguruma suala la Kiwira. Mpendazoe ameomba ruhusa kwa Spika ili awasilishe doecuments zinazoonyesha ANBEN, mmoja wa wanahisa wa Kiwira ni nani na diozument nyingine zinazoonyesha jisni ubinafsishwaji wa Kiwira ulivyofanyika.
Anasisitiza kuwa ni lazima nchi iwe na utaratibuw a kuwaadhibu viongozi wanaopewa dhamana ya juu kabisa pale wanapokiuka maadili ya uongozi
 
bado anendelea kuzungumza "kama watanzania tusipojali maadili leo, itafika siku nchi itasambaratika.... Serikali ya awamu ya nne haikuapa kulinda serikali ya awamu ya tatu na serikali ya awamu ya tatu haikuapa kuilinda serikali ya awamu ya pili... waliapa kuilinda katiba"
Lakini Sita amemkataza kuendelea kuzungumzia suala la serikali za awamu kwa sababu halimo kwenye hoja na inakatazwa na kanuni za bunge.
Mpendazoe anamalizia kwa kusema ni bora waliohusika na suala la Kiwira waombe radhi kwa watanzania
 
Mjdala umezizima au umezimwa?

Kha hivi huwa wanafanya rehearsal za hii mijadala siku moja kabla kwenye caucus?

Eti mjadala utafungwa November, mbona hawakuuongezea siku kama wa ule wa elimu?
 
Last edited:
Huyu mzee wa Urambo bwana ana matatizo .Au ndiyo njia ya kutaka Ulinzi uongezwe ?Kila mara lazima aibuke na kuzima issues .
 
Kulikuwa na mjadala mkali na wabunge karibu wote waliozungumza, ukiacha Karamagi, walipingana na ripoti ya serikali inayoonyesha kuwa maofisa wa serikali (Hoseah na Mwanyika) hawakukutwa na hatia yoyote. wabunge wamesema kuwa hawakubaliani na njama za serikali kuwasafisha watu ambao ripoti ya kamati teule ya bunge ilionyesha wazi kwua walikuwa wamefanya makosa.
lakini Sitta nadhani ameiokoa serikali kwani alipoona wabunge wanazidi kuchachamaa, alisitisha mjadala, akashauri kuwa kamati ya madini ikae na kuandaa ripoti ya nini kinachopaswa kufanywa na serikali ili kikao kijacho hoja hiyo ndio imalizwe. Ngeleja alikubali ghoja hiyo kwa niaba ya serikali na shelukindo, mwenyekiti wa kamati, naye akakubali, na wabunge wote nao wakakubali.
Hivyo ngoma ya Richmond hadi Novemba

Kwa nini Spika atoe upenyo kwa jambo ambalo liko wazi. Nilimsikiliza Dr Slaa kwa muda mfupi na kuhisi kuwa serikali iko hatarini. Kama siyo Spika, ya Feb 2008 yangeweza kujirudia. Hata hivyo siwezi kushangaa kwa sababu wote ni CCM na kwa hiyo mwisho wa siku wanatataka kulinda chama wanachowajibika kwake badala ya wananchi wanaodhulumiwa. Sina hakika kama hiyo Novemba itakuja na jambo la maana. Mkakati wa kuchezea hii hoja ulionekana toka siku nyingi na kwa hiyo ilibidi leo kieleweke. Basi tena, wandanganyika ndo tumeingizwa mjini kwa mara nyingine. Drama inaendelea!!🙄
 
Hakuna siri katika mambo ya kitaifa. Kwani ukificha leo , lakini kesho atatokea mwandawazimu na kuyafunua yooote. hata ikipita miaka 50 lakini lazima watashitakiwa.
 
Mjdala umezizima au umezimwa?

Kha hivi huwa wanafanya rehearsal za hii mijadala siku moja kabla kwenye caucus?

Eti mjadala utafungwa November, mbona hawakuuongezea siku kama ule wa elimu?

Comrade, mjadala umezimwa hadi November halafu utazimwa tena hadi Febrauri 2010 halafu utazimwa tena hadi kiako cha bajeti 2010 then uchaguzi mkuu halafu Watanzania tutafungwa tena kamba kama kawaida
 
Huyu mzee wa Urambo bwana ana matatizo .Au ndiyo njia ya kutaka Ulinzi uongezwe ?Kila mara lazima aibuke na kuzima issues .

Mkuu Kumbuka limo la USD 300,000, kumbuka pango la dola 8,000 kwa mwezi.....and the list goes on....unadhani atawasahau wanaomwezesha ki hivyo?
 
Yule mama aliyeongea kwa uchungu kabla ya Karamagi ndio Stella Martin Manyanya?

Hii danadana ya Richmond, Kiwira na North Mara kwa mwendo huu itaisha Novemba?
 
Hakuna siri katika mambo ya kitaifa. Kwani ukificha leo , lakini kesho atatokea mwandawazimu na kuyafunua yooote. hata ikipita miaka 50 lakini lazima watashitakiwa.

Sawa mkuu ila "justice delayed is justice denied". Wewe unaonaje?
 
Yule mama aliyeongea kwa uchungu kabla ya Karamagi ndio Stella Martin Manyanya?

Hii danadana ya Richmond, Kiwira na North Mara kwa mwendo huu itaisha Novemba?
Ndiye mwenyewe.
Hii danadana haitaisha Novemba kwa sababu imeshaonyesha kuwa kuna aina fulani ya kulindana. nadhani yaliyoibuliwa na baadhi ya wabunge yameonekana kuwa mazito. Mkakati wao ulianza kufeli tangu juzi walipowakutanisha wabunge wa CCM ambao wengi walionyesha 'uasi' wa wazi wazi, kwa hiyo nadhani wameamua kujipa muda ili kupanga mikakati zaidi
 
Mkuu Kumbuka limo la USD 300,000, kumbuka pango la dola 8,000 kwa mwezi.....and the list goes on....unadhani atawasahau wanaomwezesha ki hivyo?

Mi dola hizo zinaniuma we acha tu alafu lile benz analo tembelea sasa atauziwa yeye mwenyewe kama gari chakavu uliza bei yake utaambiwa kanunua kwa milioni 2 au 5 limetengenezwa mwaka 2006 leo hii chakavu mmmh!
 
Pinda ameshaliahirisha Bunge hadi Novemba. nadhani sasa ni wakati wa kuwabana kwa hoja
 
Back
Top Bottom