Rick Ross anunua nyumba ya Evander Holyfield yenye vyumba...

NEW NOEL

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2011
Posts
863
Reaction score
408
CEO wa Maybach Music Group na rapper ambaye yupo kwenye peak sasa,namzungumzia Rick Rozay amenunua nyumba iliyokuwa inamilikiwa na bondia wa miaka mingi Evander Holyfield.
Nyumba hiyo ambayo ipo Georgia ikiwa katika eneo la hekari 235 na ikiwa na vyumba vya kulala 109 na sehemu ya wageni kulia chakula ikiwa na vuwezo wa kupokea wageni takribani 100.
sifa nyingine kubwa juu ya nyumba hii ni kuwa miongoni mwa nyumba zenye mabwawa ya kuogelea(swimming pools) kubwa zaidi marekani.
Kama utakumbuka jamaa aliwahi kuwa na ugomvi na rapper mwenzake 50 cent ambaye pia aliwahi kununua nyumba iliyokuwa inamilikiwa na bondia Mike Tyson.
Kuweza kuitunza nyumba hii itamgharimu Rick Ross takribani dola za marekani 17000(zaidi ya shilingi milioni 27) kulipia umeme na kiasi kingine cha dola milioni 1 kwa mwaka kama matunzo kwa nyumba hii.

rick house2.jpg

rick house 3.jpg

rick house 4.jpg

rick house 4.jpg

rick house.jpg

rick house.jpg
 
Attachments

  • Rick-Ross-Motorcycle.jpg
    Rick-Ross-Motorcycle.jpg
    26.8 KB · Views: 962
kwa wenye nazo wanaweza.nyumba vyumba 109,vyumba vingine vinaweza vikapita mwaka hata kuvifungua hujavifungua SI MCHEZO!
 
Hao ndio Mastaa sasa,achana na hawa wanaohangaika na kubeba sembe kila kukicha na mafanikio yao yanaishia clubs mbalimbali za usiku.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Nyingine sifa tu za bure hasa kwa hawa wenzetu weusi wana shida na tashtiti wanapopata hela!asa mavyumba yote ayo ya kazi gani mwee
 
huo mjengo akija kufilisika na yeye, lazima ataupiga bei tu. kamwe hataweza kumudu kulipa bills atafanya kama wenzake kina tyson na wengine, anyway mwacheni nigga rozay ale bata, teh teh teh teh teh
 
CEO wa Maybach Music Group na rapper ambaye yupo kwenye peak sasa,namzungumzia Rick Rozay amenunua nyumba iliyokuwa inamilikiwa na bondia wa miaka mingi Evander Holyfield.
Nyumba hiyo ambayo ipo Georgia ikiwa katika eneo la hekari 235 na ikiwa na vyumba vya kulala 109 na sehemu ya wageni kulia chakula ikiwa na vuwezo wa kupokea wageni takribani 100.
sifa nyingine kubwa juu ya nyumba hii ni kuwa miongoni mwa nyumba zenye mabwawa ya kuogelea(swimming pools) kubwa zaidi marekani.
Kama utakumbuka jamaa aliwahi kuwa na ugomvi na rapper mwenzake 50 cent ambaye pia aliwahi kununua nyumba iliyokuwa inamilikiwa na bondia Mike Tyson.
Kuweza kuitunza nyumba hii itamgharimu Rick Ross takribani dola za marekani 17000(zaidi ya shilingi milioni 27) kulipia umeme na kiasi kingine cha dola milioni 1 kwa mwaka kama matunzo kwa nyumba hii.

View attachment 135680

View attachment 135682

View attachment 135683

View attachment 135683

View attachment 135685

View attachment 135685

Tatizo mabondia wengi hawana elimu, ni vijana wa mitaani, hali kadhalika wana muziki vivyo hivi. Hasa hawa African American wao wakishatunisha mifuko tu mambo ya juu juu kabisa wakati pesa hizo angewekeza kwenye real estate kama kujenga jengo la ghorofa mjini lingemwinua hadi wajukuu wakashtukia kazi aliyofanya imetoa matunda.
 
Si kila mtu atafanya biashara ya real estate hawa watu wanamabiashara yao mengi tu na yanawaingizia faida sana

Rozay anatengeneza cognac,ana-clothing line yake maduka ya nguo,migahawa na na matangazo ya biashara na vitu kibao tu

Alafu sahivi elimu si dili saana kama utakuwa na knowledge ya biashara na kuajili wataalamu

Bawse!!
 
Evander kafilisika na kama sikosei hata mkewe kamukimbia,tatizo la ngozi nyeusi hata iwe wapi na iwe na fweza kiasi gani kufilisika kwao nikitu cha kawaida ,kisa ulimbukeni ,atataka kile dame mzuri mwenye sifa hapo mademu bomba wa kizungu ndio hupenda kujilengesha,atanunua jumba la kifahari na kufanya part kila kukichwa,kuwekeza kwao inakuwa hakupo,baada ya muda akianza kuchoka (kwa mabondia /wanamichezo)ndio madeni yanaanza na kuanza kuuza uza vitu ili kujikimu,afadhali kidogo wanamuziki wanakuwa kwa game muda mrefu ,lakini baado maisha ya kifahari,anasa ndio chanzo cha kufilisika kwahawa waliokuwa mamilionia tena mamilionia wa dola na si fedha za madafu
 
Si kila mtu atafanya biashara ya real estate hawa watu wanamabiashara yao mengi tu na yanawaingizia faida sana

Rozay anatengeneza cognac,ana-clothing line yake maduka ya nguo,migahawa na na matangazo ya biashara na vitu kibao tu

Alafu sahivi elimu si dili saana kama utakuwa na knowledge ya biashara na kuajili wataalamu

Bawse!!

Kwa vile hujanielewa endelea na safari. Huyo holifield kama angekuwa na akili ninaosema ambayo ni mfano tu asingefilisika na leo kubaki historia. Yaliyowapata mabondia wengi wamarekani weusi ni hayo hayo.
 
Back
Top Bottom