Nilivyo iona thread nilianza kupata hasira..ujue mi huwa sipendi dharau..inakuaje huyu Bonge Nyanya adharau vitu vyetu..ila baada ya kusoma comment za baadhi ya washiriki hasira zikapungua kidogo na sasa hasira zinawageukia bodi ya Utalii, kwani wakienda Marekani kuutangaza huu Mlima huwa wanautangazaje??? Ina maana hawa jamaa wanamaliza kodi zetu kuutangaza mlima wetu kuwa ni kilevi tena kilevi haramu....au manegro wenzake walivyo kuja kupanda mlima walishuka wamelewa au nini hasa kilimfanya afikiri ML. Kilimanjaro ni Bange???