Ridhiwan akwaa uongozi UVCCM

Ridhiwan akwaa uongozi UVCCM

ChingaMzalendo

Senior Member
Joined
Nov 9, 2008
Posts
192
Reaction score
3
Na Waandishi Wetu

KATIKA hali inayoonyesha utaratibu wa kurithishana uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeanza kushamiri , watoto wa vigogo kadhaa wa chama hicho akiwemo wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, wamechaguliwa kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM).

Matokeo ya uchaguzi huo yaliyopatikana jana kutoka mikoa mbalimbali, yameonyesha kuwa mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete ni miongoni mwa viongozi waliochaguliwa kwa kishindo kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM taifa, akipata kura 274 kati ya 315 zilizopigwa.

Wengine waliochaguliwa na Ridhiwan kuongoza jumuiya hiyo mkoani Pwani na nyadhifa zao kwenye mabano ni Abdalah Ulega (mwenyekiti) na Mkomwa Mtiga (Mjumbe wa Mkutano Mkuu taifa).

Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, wengine waliochaguliwa kuongoza jumuya hiyo mkoani Pwani ni Josephat Msonde (Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa), Hilda Mzengo (Mwakilishi wa UWT) na mwakilishi wa wazazi mkoa, Siza Mjokaba.

Mkoani Morogoro, mtoto wa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto, Lucy Nkya, Jonas Nkya, alichaguliwa kwa kura 290 kuwa Mwenyekiti wa Mkoa UVCCM.

Jonas aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wapinzani wake Musa Kingu ambaye ni ndugu wa katibu wa uchumi na fedha wa CCM Taifa, Amos Makala na Adela Ng'atigwa.

Nkya alishinda katika kura za marudio baada ya matokeo ya awali kushindwa kumtoa mshindi aliyepata zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa.

Hata hivyo, Musa Kingu alibahatika kushinda nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM taifa, huku Pili Jabiri akijishindia nafasi ya mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM taifa.

Aliyechaguliwa kuwakilisha vijana UWT mkoani Morogoro ni Sepesina Lugalila, huku Masumbuko Igebya akichaguliwa kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM mkoa na Antony Muhando akiwawakilisha wazazi.

Amosi Makala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi huo, aliwataka vijana kuwa na mshikamano na kutokubali kugawanywa na viongozi wachache ndani ya chama kwa kuwa vijana ndio nguzo kubwa na tegemeo la chama.

Naye mtoto wa Mbunge wa Jimbo la Kwella, wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, Chrisant Mzindakaya, Paul Mzindakaya, ameibuka mshindi wa kiti cha mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoani humo.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo kutoka Makao makuu ya umoja wa vijana, Thomas Mwang'onda ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa, alimtangaza Paul Mzindakaya kuwa amewashinda wenzake kwa kupata kura 205.

Katika uchaguzi huo mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Afrika, Kituo cha Rukwa, Sammy Kissika, alishinda nafazi ya ujumbe wa Baraza Kuu la Vijana taifa Mwang'onda alimtangza Bernard Mukasa kuwa ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM taifa.

Mkoani Mwanza, Maghembe Boniphace Koneli amechaguliwa Mwenyekiti wa UVCM katika uchaguzi huo uliofanyika juzi.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza, Barnabas Essau aliliwaambia waandishi wa habari jana kwa kura 365 na kuwashinda wagombea wenzake Abel Maiga Kaitila aliyepata kura tisa na John Dea aliyepata kura 184.

Essau alisema kuwa nafasi ya mjumbe wa Baraza Kuu Taifa la chama hicho ilikwenda kwa Barnabas Mathayo, mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa amechaguliwa Barnabas Mathayo, nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa ilikwenda kwa Peter Yona Minga, uwakilishi wazazi ilikwenda kwa Muhoja mwinamila Mapande na uwakilishi wa UWT ilikwenda kwa Rehema Laurent.

Mkoani Mbeya UVCCM ilipata sura mpya baada ya kumchagua Regnand Msomba kuwa Mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Naye Benedict Ngwenye alichaguliwa mwenyekiti mpya wa UVCCM mkoa wa Ruvuma kwa kura 331.

Akitangaza Matokeo hayo jana katika ukumbi wa shule ya wasichana Songea Msimamizi wa uchaguzi huo Livingstone Msinde ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tunduru alisema,wajumbe waliopiga kura ni 391 ambapo kura halali ni 387 na kura nne ziliharibika.

Mkoani Kagera, Deusdedith Katwale kuwa mwenyekiti mpya ya jumuia hiyo Mkoani Kimalinjaro Godliving Mosha ambaye ni mpiga debe alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa mkoa baada ya kumpa kura 259 dhidi ya Antony Malisa kura 127 na Gilbert Temu aliyeambulia kura 102.

Mosha mwenye elimu ya Sekondari, aliwabwaga wasomi wawili Malisa na Temu ambao wana elimu ya chuo kikuu.

Wakizungumza na Mwananchi baada ya matokeo kutangazwa, baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu walisema wameamua kumchagua Mosha kwa vile anafahamu vema shida na matatizo ya vijana wa mkoa wa Kilimanjaro
.

Habari hii imeandaliwa na Julieth Ngarabali, Kibaha, Lilian Lucas,Morogoro, Paulina David, Mwanza, Brandy Nelson, Mbeya, Joyce Joliga, Songea, Lilian Lugakingira Bukoba, Mwandishi Wetu, Sumbawanga na Ally Sonda,Moshi.*
 
kwanini iwe ni watoto wa vigogo, au ndio maana kenya wanatusimanga?
 
acheni upumbavu... kama baba yake angemteua kuwa kiongozi wa chama then sawa. The guy kachaguliwa na wanachama wenzake. It does not look very good lakini at the same time... anakila haki yakugombea.. Nachukia kuona article zakijinga kama hizi ambazo hazina a shread of objectivity.. For one, the conclusion seems to be mwanzo wa article. This is what is popularly termed as BS... It goes to show a rather recurrent theme here at JF
clearly represented by the formula below

(HOJA)-(Objectivity) = JF

NB: The formula does not apply to everyone of course but, the exceptions are an endangered species in this lil world.
 
Hapa ni kwamba amejitokeza mwenyewe na kugombea nafasi hiyo;ila kama angeteuliwa hata na kiongozi yeyote japo siyo ndugu yake,hapo hata mimi ningeona ni mambo ya kurithishana madaraka.
Wenzake wamechagua kwa kura ni haki,vinginevyo labda isibitishe kuhusu usanii katika kupata huo ushindi.
 
Inachoudhi ni jinisi gani JF kama media inayotegemewa na watu wengi sana inaweza ruhusu post zakijinga zinazokosa objectivety. Kama tungekuwa tunataka biased media tunge subscribe to FOX news or something.. Huu ni ujinga.
 
Ni kweli kachaguliwa na wananchi na ana haki ya msingi kama raia wengine na sijuhi mleta habari alikuwa ana lengo gani hasa.Ila kwangu mimi nina swali kama ,je amechaguliwa ana sifa hizo ama ni kwa kuwa baba yake ni JK?Maana hapa kuna mengi inawezekana amechaguliwa kwa sifa zake kuwa watu wamona katika wagombea wao yeye anafaa,au wengine wanaompenda baba yake (JK) automatically wamemshobokea mtoto pia au imetumika fraud kwa kuwa mtoto wa kigogo.Inawezekana kati ya hivi ama combination ya hivi.
Sasa cha msingi hapa ni kusaidi kuelimisha wananchi kuwa kuna umuhimu wakimchagua mtu kwa sifa zake,maana bongo wananchi wakawaida bado sana ni rahisi mno kuyumbishwa(sisemi kuwa huyu kachauguliwa kwa mizegwe ,mimi sijuhi :maana nimeona kuna attacking machine hapa)
 
Inachoudhi ni jinisi gani JF kama media inayotegemewa na watu wengi sana inaweza ruhusu post zakijinga zinazokosa objectivety. Kama tungekuwa tunataka biased media tunge subscribe to FOX news or something.. Huu ni ujinga.


Kinyambiss, you need to chill!
 
I think by common sense we are stupid. Tunapenda kukumbatia sana hiki kitu. Karume Sr. Karume Jr then Karume???? etc. Mwinyi Sr. Mwinyi Jr. Mwinyi ????? etc. Kikwete Sr. Kikwete Jr. Kikwete ???? etc.

Are we that pumbafu to believe on genetics and take the country to run on governance by genetics.? It would have been better if we had a gene from Nyerere, or Sokoine, or at least Mwinyi but not the one we know already are not favourite.

If the baba ana kigugumizi cha maamuzi then so the son since we believe in the same kinasaba etc.

That is the essence of genetics and that is the importance of thinking outside the box rationally. Wote tumesoma biolojia BUT bado mbumbumbu tu. We can not integrate and apply knowledge and thats where we fail all the time.

Is there anyone who has ever thought anything on application of genetics in politics. No never or no often, but we need to; all the time as a prerequisite.

Cite a vivid example: Bush Sr. fought nearly all his time in the white house. Big big war with a lot of aftermath socially, financially, economically etc and so his son, Bush Jr. Since we know genetics and just take it for granted. Even the prevailing economic crisis is the aftermath from Bush Jr. We do not see and when intellectual mind question about it one keeps saying we need not be biased. When, where and to whom we should be biased. This is our country bwana we love so much! Huku ugaibuni ni matatizo matupu, we are prepared all the time to expect un-expected.
 
this is what we call dynasty!!! hana upeo wala uwezo ni jina tu. tunakoelekea sasa ni kuwa na PRESIDENTIAL MONARCHY
 
Nyie mnapiga kelele zisizo namaana democracy means even people u dnt like can run atakama baba yake alikuwa Rais na Babu yake alikuwa Rais na Queen of England alikuwa bibi yake... Ukichukia mnyime kura, sio kulalamika vitu ambavyo havina kichwa wala kiwiliwili.

We unaesema nichill.. For what reason should I chill? when I see that kunamisuse of the forum.... kwanini nisiseme!?! Au JF cant fathom the extremities of freedom of speech!?lol
Inakuwa kama waistreli walipoona Hamas imeshinds elections in Gaza.. Watu wanataka democracy when it best suits them and not otherwise.hahaha.... Aint no such... talk about chillin...ki2gani.
 
Inachoudhi ni jinisi gani JF kama media inayotegemewa na watu wengi sana inaweza ruhusu post zakijinga zinazokosa objectivety. Kama tungekuwa tunataka biased media tunge subscribe to FOX news or something.. Huu ni ujinga.

Mkuu,

Haina maana kwamba wewe ukiona kitu ni cha kijinga, basi wote wakione hivyo. Tuna mitizamo tofauti. Thats the challenge of diversity na ndo democrasia tunayoipigania. Kuheshimu mawazo ya wenzetu. Hata kitu kama hukubaliani nacho siyo lazima uki-brand kwamba ni ujinga, simply because you dont agree with the topic.

Hata hiyo Fox NEWS UNASEMA IKO BIASED kwa sababu umesema wewe. Si kila mtu anaona hivyo. Perhaps kuna wengine watasema CNN iko biased au BBC..and on and on...Cha muhimu HESHIMU MAWAZO ya wenzako bila kuita hoja zao kwamba ni za kijinga. It will serve you well.
 
Haya watoto wa vigogo, mwenzenu huyooo keshaukwaa, anapiga ndogo ndogo za uraisi miaka 15 ijayo. Mnasubiri nini huko mliko?
 
ok let em do what you people want then.lol

-----------------"----------"-----------------"---------------" happy.lol
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka na si kenge!!!! Ukweli ni kwamba hata kama hao watoto wengi wao hawana sifa wanachaguliwa kwa sababu ya ushabiki tu!!!! Wapiga kura waoga hao!!! Wanaogopa kuchukiwa na vigogo hao!!! Haiwezekani kuwa kila mtoto wa kigogo akisimama kwenye uchaguzi eti anapata kura kwa kishindo ati ina symbolize kuwa ana uwezo wa kazi!!!!! La hasha!!! Narudia watanzania bado hatujaweza kutumia demokrasia vizuri, tunafanya demokrasia ya woga tu. Tuamke sasa na wenye vyombo vya habari wahabarishe elimu ya demokrasia na NGOs jamani ombeni mipesa ya good governance kwa wahisani wa maendeleo kwa ajili ya elimu ya uraia, mkazo utiliwe kwenye demokrasia.
 
kwanini iwe ni watoto wa vigogo, au ndio maana kenya wanatusimanga?

Hivi wewe ukiwa Daktari ama Mbeba maboksi ni kosa mwanao kuwa Daktari ama mbeba maboksi?

Hiyo nafasi mnayopigia kelele mnaijua lakini? Yaani mjumbe wa baraza kuu la vijana la CCM akiwakilisha mkoa/wilaya huko nako anahitaji kubebwa na baba yake?

Kwani wakati alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa fKitivo cha Sheria pale UDSM alichaguliwa na wana CCM ama wanafunzi wenziwe? Je utendaji wake ulikuwaje kule? Alishindwa kuwatetea wanafunzi wenzake? Unajua ni wenzake wangapi waliepuka madhila ya elimu ya UDSM kutokana na jitihada zake? Je wakati huo baba yake alikuwa Rais ama mwenyekiti wa CCM?

Kumbuka kijana ni mwanasheria na ana upeo wa mambo ya siasa zaidi ya wengi humu ndani na hakuibuka tu bila ya kupitia nafasi nyingine za kiuongozi.

Mimi naamini mwendo anaokwenda nao ni mzuri na unaonyesha kukomaa kuliko wenzake wengine waliobahatika kuwa na wazazi viongozi katika ngazi mbalimbali za chama na serikali...

Kama ni makosa ya ujana naamini Ridhwan anajitahidi kuwa makini kuliko wengi wetu humu. Kama kuwa mtoto wa kiongozi mkubwa naamini Ridhwan anajitahidi sana kuwa mwangalifu kuliko watoto wengine wa so called vigogo wa zamani na wa sasa. Wote mnawaona jinsi wengine wanavyoharibu....

Mtu yeyote anayemjua Ridhwan atang'amua kuwa ni kijana mwenye nidhamu, upendo, msikivu (ingawa kwenye kuamua huamua anavyona yeye ni sawa) na zaidi anayejua nini la kusema na nini la kunyamaza...na hii ndio siri kubwa ya mafanikio katika siasa


Tanzanianjema
 
Tanzanianjema, shukrani kwa hayo maelezo. Tumepata mwanga, maana wengine tulikuwa gizani tukiwa na picha tofauti vichwani. Hata hivyo, naomba nikupe changamoto kidogo, kwa kuliangalia hilo swali ulilochagua mwenyewe kulijibu 🙂
kwanini iwe ni watoto wa vigogo, au ndio maana kenya wanatusimanga?
Wanahabari wameandika mara kadhaa kuhusu watoto wa vigogo "kuandaliwa".
Hao wengine je, waliotajwa kwenye habari hapo juu?
 
Back
Top Bottom