Elections 2010 Ridhiwan Kikwete avamiwa na vijana wa CHADEMA ashindwa kufanya kampeni

Kampeni za Ridhwan zinawauma sana chadema. kama hazina manufaa kelele zote za nini?


............majuha kalulu wapo wengi!!!

..hivi huoni huo ni uchuro......CCM chama chenye mtandao wa kuaminika kinakosa sweapers kwenye kampeni zake hadi kinafikia kuwatumia RIZWAN na SALMA....nani alisema hii nchi ni MONARCHY......isitoshe ofisi ya kuratibu kampeni wamehamisha toka Lumumba hadi upanga...na anayeratibu mambo ya ofisini.,IT na kuwalipa wasanii wa bongo fleva na baadhi ya malipo mengine ni yule chizi MIRAJ....
watoto wake waliobakia wenye umri wa wastani kama YUSUF na wengine anazunguka nao yeye mwenyewe kumsaidia shughuli binafsi ndogondogo....simply hamuamini mtu kwenye team ya kampeni ya CCM ndio maana amewekeza kwenye familia.........SASA KWELI CCM IMEKOSA WATU WAAMINIFU MPAKA TEAM YA KAMPENI INAKOSA WATU...WANAOWEZA KUAMINIKA???

HIVI NYERERE ANGEAMUA KUFANYA HIVI NA ENZI ZILE..UELEWA ULIKUWA MDOGO...LEO HII NCHI SIINGEKUWA YA KIFALME....NA HUENDA TUNGESHAZOEA!!
 
Kampeni za Ridhwan zinawauma sana chadema. kama hazina manufaa kelele zote za nini?
Tatizo siyo kampeni za ridhwani bali ni uhalali wa familia kuingilia masuala nyeti ya kiserikali kwa kutumia nembo ya chama kuhalalisha maslahi ya kifamilia.
Naomba kudeclare Interest kwamba mimi siyo mwanachama wa chadema, sijawahi kukaribishwa huko ila kwenye kura nitapiga kura zangu kwa wagombea wa chadema kwa kuwa wana sera makini na hata ufuatiliaji wake ktk utekelezaji wa ilani yao umenivutia.

Tunapomsema RIZ1 sio kwamba tunamuonea gere bali tunamhurumia kwa balala la kisheria atakalokumbana nalo huko mbele. Take my word. He is stupid ever to exist. Endelea kushabikia na kushadidia uvunjwaji wa sheria za nchi halafu uone mwisho wake inakuwaje.
 
Mmm ikiwa mwalimu yupo hali kama hiyo sasa wanafunzi unawategemea watakuwa katika hali gani ?
 
Wakati wanyakyusa wamemtunuku uchief mtoto wa Rais, wenzao wanyalu wamemtimua. Inapendeza.
 
kitu kimoja kimenifurahisha sana hapa. Vijana wa kijiweni wanasema "Hatudanganyiki" very good. All Tanzanians say
" MWAKA 2010, ... HATUDANGANYIKI"
 

.
You are true mheshimiwi, huyu Riziwana anafanana sana na mtoto wa Chiluba Kastro aliyejiweka juu ya sheria na kufanya atakacho wakati baba yake akiwa rais wa Zambia. Huyu Kastro sasa hivi ni marehemu, huwezi amini kuwa amekufa akiwa amevishwa pingu kwenye kitanda cha hospitali kwani alitiwa nguvuni na serikali iliyochukuwa madaraka baada ya baba yake. Haikumwonea huruma kwa uvunjifu wa sheria za nchi japo serikali yenyewe ilikuwa ni ile ile ya chama cha baba yake. Huyu ridhiwani sii tu kwamba chama pinzani kama kikifanikiwa kutwaa dola ndio kinaweza kumchukulia hatua za kisheria, bali hata ccm yenyewe ikiendelea kuwepo madarakani haitamvumilia kwa uvunjifu wake wa sheria za nchi na matumizi mabaya ya rasilimali zake. Hajang'amua bado ni kwa nini marais wote wastaafu pamoja na mawaziri wote wakuu wamejinyamazia kimya bila kumpigia debe baba yake. Kama hili toto limechagua kuwa pumbafu acha liendelee na upumbafu wake bali wakati wa kuvuna utafika.
 
hivi nikilia nina dhambi????????
Embu angalieni jamani hayo mashangingi halafu linganisha na huyo mwalimu mkuu. Inawezekana kwenye maisha yake hajawahi kupanda hata shangingi . Dah!! Hi hii Tanzania jamani. Mwalimu mkuu kabisaa angalia hata mikono yake.. Sijui kama mshahara wanamlipa Tshs ngapi au labda hata hawajamlipa mda mrefu. Duh!!
 
mie heading imenichanganya mwenzenu, aliyevuruga kikao ni vijana wa chadema au???
 
Nakumbuka niliwahi soma kanuni na sheria za Uchaguzi mkuu ya kwamba hairuhusiwi chama chochote kupeleka siasa zake mashuleni...Sasa hii wakuu zangu imekaa vipi au mimi ndio sikuelewa sheria ile.
 
mie heading imenichanganya mwenzenu, aliyevuruga kikao ni vijana wa chadema au???

Ukisoma maelezo yote, nina mashaka kwamba waliovamia hicho kikao ni vijana wa CCM waliokuwa kambi ya Mwakalebela na hawataki suluhu na tayari wameisha-declare wazi kwamba kura zao ni kwa Msigwa. Sina hakika kama Msambatavangu angeweza kwenda kuwaita vijana wa CHADEMA waende kwenye kikao cha UVCCM.

Kwa hali ilivyo kwenye jimbo hilo, Vijana waliokuwa wakimuunga mkono Mwakalebela wameelekeza nguvu zao kwa Msigwa kama kisasi. Kwa kufanya hivyo watakuwa wamepeleka salaam kwa JK na CCM yake kwamba wenye maamuzi ni wanachama na siyo CC na NEC. Next time hawatakuja kufanya makosa ya kijinga ya kukata majina bila sababu za msingi.
 
Ahaa haaa! Naukumbuka mwimbo we2 wa michezo zamani enzi za umitashumta.... Maji ya kisima mkorogo umedunda... Umedundaa... Pia huyu ticha Mkeremi a.k.a minjino. Amenikumbusha mbaali sanaa... Ticha wangu wa michezo enzi za umitashumsta! Katupiga sana stiki mchachakamchaka asubuh ktk kambi ya michezo.... Mkeremii... Ah... Ah...akhsante Francis God umenipa raaha eli in ze moningi...
Hivi Rizi wani ndo mpatanishi? Aaah! Jamani tangu lini tembo wapiganao wakaamuliwa na Sungura?
CCM Acheni utani mbona mnafanya mambo kama hamlijui game la Politiks...
 

Tusipomwondoa JK kwa kura, yatatukumba ya Korea KasKazini!
 
Yap! Ndiye Kim Jong-un wetu waTZ

Huyu ana fanana na Captain Kongolo wa TZ;akifanana kabisa na ufujaji wa fedha za UMMA na mtoto wa kwanza wa Hayati Mabutu Seseseko aliyeitwa Kongolo,ambaye ilifikia hatua akaogopwa hata na vyombo vya dola nchini Zaire na kufanya lolote lile alipendalo,kabla hajafariki ghafla mwishoni mwa miaka ya 90!

Kuna tofauti gani kati ya Captain Kongolo mtoto wa Mobutu na Ridhiwan wa JK kwa ufujaji wa mali za UMMA za TZ?
 
Nakumbuka niliwahi soma kanuni na sheria za Uchaguzi mkuu ya kwamba hairuhusiwi chama chochote kupeleka siasa zake mashuleni...Sasa hii wakuu zangu imekaa vipi au mimi ndio sikuelewa sheria ile.

:confused2::confused2: nadhani hiyo sheria au kanuni iliwekwa kwa ajili ya UPINZANI siyo Chama TAWALA :becky::becky::becky: mkibisha muulizeni TENDWA
 
la msingi ni kumuondoa huyu kiwete ooops! kikwete pale ikulu maana anaweza kuigeuza ikulu ndo familia yake ilipo

hana maana kabisa huyu mzee na tuna bahati huyu mtoto sio mwanajeshi maana gafla mngesikia ndo mkuu wa majeshi
:becky::becky::becky:
 
safi sana, huyu riz 1 anajiandaa kupewa urahisi kama mama yake wa kufikia salma? angetakiwa achapwe viboko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…