Elections 2010 Ridhiwan Kikwete avamiwa na vijana wa CHADEMA ashindwa kufanya kampeni

Elections 2010 Ridhiwan Kikwete avamiwa na vijana wa CHADEMA ashindwa kufanya kampeni

Maelezo haya hayathibitishi kwamba ni vijana wa Chadema wamevamia na kumzuia Ridhiwan kuhutubia hii Shule ya Msingi. WaTz. walio na akili timamu hawawezi kuruhusu watoto wao wasitishe masomo kumsikiliza punguani.

Hata hivyo WaTz tusipojihadhari tarehe 31 Oktoba, Chifu Ridhiwani Mwakikwete atatutawala ifikapo 2015 na kuendelea. Tutakuwa kama Korea ya Kaskazini. Kwa sasa J.K. anaendesha Tz. kwa staili ile ile ya Mobutu Ssese Seko. Ona mashangingi hayo ya Ikulu, Chifu Ridhiwani Mwakikwete anayotumia!!!!!!!!!!

Tujizatiti na kusema "HATUDANGANYIKI !!!!!!!"
 
KWANINI VIJANA WA CHADEMA NA SIO VIJANA WA CCM WANAO MTAKA MWAKALEBELA? AU VIJANA AMBAO HAWAONI UMUHIMU WA MISAFARA YA RIDHIWANI.














Exaggeration is a billion times worse than understatement! .
 
Mmm ikiwa mwalimu yupo hali kama hiyo sasa wanafunzi unawategemea watakuwa katika hali gani ?

Mpe heshima yake, huyo ni mwalimu mkuu au Headteacher.
Inasikitisha sana, hii ni reflection ya jinsi mambo yalivyo huko mikoani, na tukumbuke kuwa hii shule iko mjini maana ingekuwa milimani au porini hayo mavx yasingefika. pga picha ya huyu wa town yuko hivi je huyo wa madongo poromoka atakuwaje??
Dawa ni moja October 31 tumwambie CCM enogh is enough
 
Ridhiwan anusurika kipigo

• ATIMUA MBIO MKUTANONI


na Francis Godwin, Iringa


MTOTO wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete, jana ameonja joto ya jiwe katika harakati za kumnadi baba yake, baada ya kutimuliwa wakati akijiandaa kukutana na wana CCM katika moja ya majengo ambayo kisheria hayaruhusiwi kufanyia mikutano ya kisiasa.


Ridhiwan ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) taifa, akiwa ameambatana na mshindi wa kura za maoni wa Jimbo la Iringa Mjini aliyeenguliwa, Frederick Mwakalebela na mmoja wa wagombea waliobwagwa, Jescar Msambatavangu, walifika katika Shule ya Msingi Ipogolo, wakitaka kukutana na vijana wa eneo hilo ili mjumbe huyo aweze kuwapatanisha Mwakalebela na mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Monica Mbega.


Kabla ya msafara wa Ridhiwan kufika shuleni hapo kwa ajili ya kikao chake kilicholenga kuvunja makundi ndani ya chama hicho, aliyekuwa mmoja wa wana CCM 12 walioingia katika kinyang’anyiro cha ubunge wa jimbo hilo na kushindwa, Msambatavangu, alipita mitaani kuwaomba vijana kwenda kumsikiliza Ridhiwan, lakini waligoma kwa madai kuwa hawadanganyiki na ujio wake.


Hata hivyo, baada ya vijana hao wa vijiweni kugoma kwenda katika shule hiyo, kwa ajili ya kukutana na mjumbe huyo kwenye chumba cha darasa la pili, bado msafara wa Ridhiwan na wapambe wake walifika huku kukiwa na vijana wasiozidi 10.


Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mvutano mkubwa ndani ya ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Amani Mkeremi, kati ya viongozi wa UVCCM mkoa wakiongozwa na Katibu wa Mkoa, Rhoda George na wale wa vyama vya upinzani walioongozwa na Katibu Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata (CHADEMA) wakivutana juu ya CCM kuzuia wanafunzi kuendelea na masomo kwa ajili ya kampeni za uchaguzi.


Tukio hilo ambalo lilitokea majira ya saa 7 mchana lilisababisha mkuu wa shule kupata wakati mgumu kulitolea ufafanuzi, huku walimu wake wakijifungia ofisini kukwepa vurugu iwapo ingejitokeza kati ya wafuasi hao.


Akielezea tukio hilo, kiongozi wa vijana hao wa upinzani, Kimata, alisema walilazimika kuweka mtego katika shule hiyo baada ya kuona hekaheka za makada wa CCM.


“Kweli sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inakataza taasisi za umma kuingia katika kampeni ...sasa tulipatwa na wakati mgumu kuona CCM inatumia shule ya msingi kufanya kampeni ndiyo sababu ya kuweka ulinzi ili kuhakikisha sheria haivunjwi ...tunashukuru tumefanikiwa baada ya viongozi wa CCM kumkimbiza mgeni wa Rais Kikwete,” alisema.


Hata hivyo, alisema kabla ya msafara wa Ridhiwan kufukuzwa shuleni hapo, kulikuwa kumetokea mvutano ndani ya ofisi ya mkuu wa shule, huku akitaka watu wa CCM wabaki ndani na wale wa upinzani watoke nje.


Hata hivyo alisema wao wameelekeza tuhuma zao kwa mkuu wa shule hiyo, ambaye amekuwa akionyesha ukada wake wazi wazi dhidi ya CCM hata kuruhusu shule hiyo kugeuzwa jukwaa la siasa kwa CCM.


Kwa upande wake, mkuu huyo wa shule alikiri akisema alipewa taarifa za CCM kuomba eneo la kufanya kikao na si kufanya kampeni na kukusanya vijana kama ilivyokuwa.


Hata hivyo alisema hana barua yoyote ya CCM kuomba darasa katika shule yake kwa ajili ya kufanya kampeni hizo.


Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa Rhoda, ambaye alikuwa mwenyeji wa Ridhiwan, alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi hakuweza kupokea, zaidi ya kukata.


Hata hivyo mmoja wa makada waliopo katika msafara huo alisema kikao hicho kilikuwa maalumu kwa ajili ya kampeni za wagombea wa CCM kupitia vijana hao na kumaliza tofauti ya Mwakalebela na Mbega.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarest Mangalla, alipoulizwa na gazeti hili alisema hana taarifa zozote, kwa kuwa suala hilo halikuripotiwa ofisini kwake.
 
Bravo vijana wa CHADEMA kuzuia ufedhuli huo, yaani watoto waache kusoma kupisha uchafu wa CCM!
 
Safi sana wapiganaji kwa kuzuia shule kugeuzwa uwanja wa siasa,bado tuna kazi kubwa ya kutoa elimu ya uraia.
 
Ivi kweli NEC ipo? yani nikiona huu ujinga ninashikwa na hasira! Alafu watasema Chadema ni chama cha fujo???
 
Kwa hali ilivyo hivi sasa muda si mrefu tutaanza kucharazana bakora!
 
September 30, 2010

SITAZIBWA MDOMO KWA VITISHO ,NIPO TAYARI KUFA KWA KUSEMA KWELI DAIMA........


Mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin

UPO usemi kuwa ukitaka kazi ya jeshi usiogope kufa na siku zote mkweli hutengwa wa waongo kama hivyo ndivyo basi kwa mara ya kwanza leo kwanza ninapenda kuanza kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye amepata kunileta duniani na kuniongoza kwa kila jambo na kunilinda na maadui wangu kwa kuwapa roho ya upendo na huruma mwingi.

Pia napenda kuwapongeza wanahabari wenzangu wote wa Tanzania ambao tumekuwa nao bega kwa bega katika kuipasha habari jamii ya kitanzania kulingana na uwezo wetu kweli nawapongeza wote bila kuwasahau wakurungezi wenzangu ambao tunamiliki vyombo vyetu yaani Blog na Website .

mimi Francis Godwin kama mmiliki wa mtandao huu na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima napenda kutumia uwanja wangu huu wa kujidai kueleza masikitiko yangu kwa wale wote ambao wameendelea kunipigia simu za vitisho kuhusiana na habari hii chini ya japo sijapokea simu ya wahusika wenyewe ila wapambe wa nje wameendelea kuwa na nguvu hata kutoa vitisho dhidi yangu kuwa iwapo nitaendelea kujifanya mkweli siku zangu zinahesabika .

Napenda kupingana na wote walionipigia simu nakutoa vitisho kama hivyo huku nikiamini kuwa kifo kwangu ni mipango ya Mungu na sitoogopa wala kuingia katika dhambi ya kusema uongo kwa jambo la ukweli hivyo ni heri kuteswa hata kufa kwa kusema ukweli kuliko kuliangamiza taifa langu kwa kuendekeza rushwa na kusema uongo kwa faida ya wachache .


Pia ninapenda utambue kuwa habari hii iliyopewa nafasi ya mbele katika gazeti la Tanzania Daima la leo na katika mtandao huu ndiyo ambayo imeonekana watu hata wale ambao ni rafiki zangu wakubwa na viongozi wangu ninao waheshimu zaidi kuninyoshea vidole na bila uchunguzi wakinituhumu kuwa mimi ni Chadema japo si dhambi kuwa chadema wala chama chochote cha siasa kwa mtanzania ila ni vema watambue kuwa mimi ni kada wa CCM na nimepata kugombea ubunge kupitia CCM na hapa nilipo ni mjumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Iringa vijijini japo taaluma yangu haina chama ,dini wala kabila.
 
Haya ndiyo matatizo ya kuwateulia wananchi viongozi wasiowataka, wanatumia nguvu kubwa kutangaza muafaka 'feki' kati ya Mbega na Mwakalebela.

Tatizo la wananchi sio muafaka, tatizo lao wanahitaji kiongozi bora wa kuwaletea maendeleo.

Kazi kwenu CCM.
 
Mimi ni mpenzi sana Wa blog ya hii Mutu! huyu jamaa hana ubaguzi katika kuhabarisha watu! Naombeni mutembeleee Francis Godwin ni mzee wa matukio daima halafu mtoe judgment. Sometimes unaweza sema anaifagilia CCM
 
Pole sana francis lakini nataka nikutie moyo kuwa hao ni waovu tu usijali na endelea mbele, kila binadamu siku zake zinahesabika hata hao wanaokutabiria hayo hawajui siku wala saa, endelea kueleza yale unayojua ukweli wake na hamna lolote litakalotokea.
 
Back
Top Bottom