MENE MENE TEKELI NA PERES....sijui kama nimepatia, ila anguko la ufalme huu litakuwa kuu kuliko mnavyodhani. Gharama ya kuingiza watoto wote kwenye siasa za uzandiki kama hizi si ndogo. Ikitokea mapinduzi, ndo kizazi kizima kitaisha...inanikumbusha Bushelvic Revolution kule Russia, ambapo Czar na familia yake walifyekwa wote. Na hata waliosalimika hawathubutu kutumia jina la ukoo ule wa kifalme, maana watmalizwa. Siwaombei mabaya, ila kuna watu wameizunguka hii familia na hawairuhusu ipate mahali pa kuwaza kwa maslahi yao. Mke yuko busy kwenye siasa, baba, watoto, nani wa kuwashauri? Mwisho watajikuta wote wamo katika kila kashfa...na endepo anguko lao litatoke ( na si mbali) basi litakuwa kuu. Hapo ndipo mtashuhudia familia nzima ikisimama kwenye mahakama kwa aibu kuu. Ni maneno yanyoudhi, ila haihitaji PHD kuona mwisho wa ufalme huu. JK yabidi atafakari......washauri wake ndio wanamuingiza king, hawaonekani wao, ila yeye na familia. La UVCCM ni dokezo ya haya