BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
MHE. RIDHIWANI AZINDUA KIKAO CHA WENYEVITI MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA, ASISITIZA UADILIFU NA KUKEMEA VIKALI RUSHWA.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete Jana Aprili 05, 2022 amezindua Kikao kazi cha Mafunzo kwa Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba wa Wilaya nchini, Kikao chenye lengo la kuwaongezea Wenyeviti hao mafunzo ya namna bora ya kuendesha mashauri ya Ardhi.
Uadilifu unaolenga haki ndiyo msingi wa kumaliza mashauri yanayopelekwa Kwenye Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya, alihimiza Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza na Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi, Waliokutana Tanga.
Katika Kikao hicho pia, Mhe. Ridhiwani amekea vikali rushwa katika Mabaraza ya Ardhi na kusisitiza kuondoa mlundikano wa mashauri ili haki itendeke kwa wakati.
Kikao hicho cha Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba kinacholenga kuwaongezea ujuzi zaidi wa kutatua migogoro mbalimbali ya Ardhi ni cha siku 4 na kimeanza Aprili 04 na kinatarajiwa kumalizika kesho Alhamisi tarehe 07 Aprili 2022.