BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndugu Ridhiwani Kikwete ameshiriki Uzinduzi wa Wiki ya Maji huko Simanjiro Mkoani Manyara iliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Mje. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Akitoa salamu za Wizara ya Ardhi, Mhe. Kikwete amempongeza na kumshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga Bajeti itakayowezesha utekelezaji wa majukumu ikiwemo kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji, mipaka baina ya Wilaya, Mikoa na Hifadhi na Usalama wa Ardhi.
Pia Mheshimiwa Naibu Waziri Kikwete amewahakikishia Watanzania kuwa Wizara ya Ardhi imejipanga kuleta amani na utulivu kwa kutatua changamoto hizo.