Ridhiwani Kikwete ataja 11 wanaotosha kugombea urais 2015

Ridhiwani Kikwete ataja 11 wanaotosha kugombea urais 2015

huyu dogo ameongea kaiwa kama nani????
 
Hata jina la Pinda na Karume hayamo kweli huyu dogo katumwa ingawa anataka kufa na Membe.

Hizo ni fikra zake kawaweka pembeni wengi tu Bilal, Sumaye, Maghufuli, na wengine.
 
Kila mtu ndani ya CCM anautaka urais,list ni ndefu sana.
1.Membe
2.January
3.Wassira
4.Sumaye
5.Sitta
6.Magufulli
7.Ngeleja
8.Nchimbi
9.Karume
10.Lowassa
11.Mwandosya
List ni ndefu sana,hivi kuna usalama kweli au ndio mambo ya mnara wa babeli ,lazima mgombane wenyewe kwa wenyewe.
 
list yake ni nzuri.Alichokosea ni kuwaweka na mafisadi katika list yake.Mtu kama lowasa na ngereja kweli?Na Nchimbi pia anataka urais.Haa,haa,haa hii ni hatari sana
 
RIDHIWAN AMTAJA MRITHI WA DINGI YAKE.

Dar es Salaam. Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametaja majina 11 ya wanachama wa CCM wanaofaa kuwania urais kurithi kiti cha baba yake, Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake mwakani.

Ridhiwani (35), ambaye alishinda kiti cha ubunge wa Jimbo la Chalinze Aprili mwaka huu, alitaja majina hayo katika mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.

Miongoni mwa aliowataja kuwa wana sifa ni makada watano walio chini ya uangalizi wa CCM wa mwaka mmoja baada ya kubainika kuanza kampeni za urais mapema, mawaziri wawili waliopoteza nyadhifa zao katika kashfa ya Operesheni Tokomeza, mwanamke mmoja na Rais wa Zanzibar.

“Kutaja majina tu, naweza kuorodhesha wengi tu. Naweza kuorodhesha hata watu 500, kwa sababu tunaona wengi sana,” alisema mtoto huyo wa Rais Kikwete ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa muda mrefu akitokea umoja wa vijana wa chama hicho, UVCCM. “Kwa mfano, kwa upande wa Bara tunao Emmanuel Nchimbi, William Ngeleja, January Makamba, Bernard Membe, Steven Wassira, Edward Lowassa na Asha-Rose Migiro,” alisema.

Aliongeza: “Hawa ni kwa uchache zaidi… ni baadhi ya watu ambao wanatajwa kwa upande wa Bara, lakini jambo la msingi ni nani mwenye sifa za kuwa rais.”

Alisema pamoja na kwamba wanasiasa hao wote wanazo sifa za kuiwania nafasi hiyo ya juu, vikao vya chama ndivyo vitakuwa na nafasi ya kuwachuja ili kupata wanaotosha. “Kama wanatosha au la, vikao vya chama vitakaa kuamua licha ya kuwa hao wote niliowataja, kwa sifa za kugombea urais wote wanajitosheleza. Wana sifa, wana uwezo wa kugombea na wana uwezo wa kushinda, hao ni kwa upande wa Bara,” alisema.

Alipoulizwa hali ikoje kwa upande wa Zanzibar, Ridhiwani alisema, “Sisi chama chetu kina utajiri wa watu kwa upande wa Zanzibar kuna Shamsi Vuai Nahodha, Hussein Ali Mwinyi, Dk Seif Ally Iddi (Makamu wa pili wa Rais Zanzibar) na Dk Mohammed Ali Shein, Rais wa Zanzibar. Hawa ni watu ambao wana uwezo na hata wakipewa jukumu la kuongoza nchi hii wanaweza. Tunao wengi sana.”

Membe, Wassira, Lowassa, Ngeleja na Makamba walipewa adhabu na Kamati ya Maadili ya CCM ya kutogombea nafasi yoyote ndani ya chama wala kufanya kampeni baada ya kudaiwa kukiuka taratibu za chama hicho, wakati Nchimbi na Nahodha walilazimika kujiuzulu nyadhifa zao za uwaziri kutokana na kashfa ya Operesheni Tokomeza ambayo ililenga kushughulikia majangili, lakini ikahusishwa na vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.

Ridhiwani hakumtaja Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye ambaye pia anatumikia adhabu hiyo ya Kamati ya Maadili ya CCM.

Baadhi kukwama

Hata hivyo, Ridhiwani alidokeza kuwa wapo baadhi ya wanasiasa watakaokwama kufikia lengo hilo kutokana na kukabiliwa na kesi ndani ya chama, ambazo hakuzitaja wala kutaja wahusika.

“Kuna watakaopungua kutokana na kesi zinazowakabili katika chama ambazo zinawafanya wapungukiwe sifa. Kwa maana hiyo kuna watu kama wanne hivi (wa Bara) unawatoa na ukiwatoa unabakiwa na watatu, sasa unaweza kujiuliza hao watakaobaki watatu, je, wanatosha?”
 
Dah uchambuzi yakinifu Wenye akili ndogo ndo wanaombishia ukweli ndiyo huo
 
akafiye zake huko ataje warithi wa utajili wa baba yake na wa kwake.
 
He is just a political novice trying to play in the super league of Tanzanian politics, his father's position notwithstanding! Wananchi walishaonywa kuwa tusipoangalia wakati utafika wauza madawa ya kulevya ndio watakaotuchagulia viongozi!!
 
RIDHIWAN AMTAJA MRITHI WA DINGI YAKE.

Dar es Salaam. Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametaja majina 11 ya wanachama wa CCM wanaofaa kuwania urais kurithi kiti cha baba yake, Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake mwakani.

Ridhiwani (35), ambaye alishinda kiti cha ubunge wa Jimbo la Chalinze Aprili mwaka huu, alitaja majina hayo katika mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.

Miongoni mwa aliowataja kuwa wana sifa ni makada watano walio chini ya uangalizi wa CCM wa mwaka mmoja baada ya kubainika kuanza kampeni za urais mapema, mawaziri wawili waliopoteza nyadhifa zao katika kashfa ya Operesheni Tokomeza, mwanamke mmoja na Rais wa Zanzibar.

"Kutaja majina tu, naweza kuorodhesha wengi tu. Naweza kuorodhesha hata watu 500, kwa sababu tunaona wengi sana," alisema mtoto huyo wa Rais Kikwete ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa muda mrefu akitokea umoja wa vijana wa chama hicho, UVCCM. "Kwa mfano, kwa upande wa Bara tunao Emmanuel Nchimbi, William Ngeleja, January Makamba, Bernard Membe, Steven Wassira, Edward Lowassa na Asha-Rose Migiro," alisema.

Aliongeza: "Hawa ni kwa uchache zaidi… ni baadhi ya watu ambao wanatajwa kwa upande wa Bara, lakini jambo la msingi ni nani mwenye sifa za kuwa rais."

Alisema pamoja na kwamba wanasiasa hao wote wanazo sifa za kuiwania nafasi hiyo ya juu, vikao vya chama ndivyo vitakuwa na nafasi ya kuwachuja ili kupata wanaotosha. "Kama wanatosha au la, vikao vya chama vitakaa kuamua licha ya kuwa hao wote niliowataja, kwa sifa za kugombea urais wote wanajitosheleza. Wana sifa, wana uwezo wa kugombea na wana uwezo wa kushinda, hao ni kwa upande wa Bara," alisema.

Alipoulizwa hali ikoje kwa upande wa Zanzibar, Ridhiwani alisema, "Sisi chama chetu kina utajiri wa watu kwa upande wa Zanzibar kuna Shamsi Vuai Nahodha, Hussein Ali Mwinyi, Dk Seif Ally Iddi (Makamu wa pili wa Rais Zanzibar) na Dk Mohammed Ali Shein, Rais wa Zanzibar. Hawa ni watu ambao wana uwezo na hata wakipewa jukumu la kuongoza nchi hii wanaweza. Tunao wengi sana."

Membe, Wassira, Lowassa, Ngeleja na Makamba walipewa adhabu na Kamati ya Maadili ya CCM ya kutogombea nafasi yoyote ndani ya chama wala kufanya kampeni baada ya kudaiwa kukiuka taratibu za chama hicho, wakati Nchimbi na Nahodha walilazimika kujiuzulu nyadhifa zao za uwaziri kutokana na kashfa ya Operesheni Tokomeza ambayo ililenga kushughulikia majangili, lakini ikahusishwa na vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.

Ridhiwani hakumtaja Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye ambaye pia anatumikia adhabu hiyo ya Kamati ya Maadili ya CCM.

Baadhi kukwama

Hata hivyo, Ridhiwani alidokeza kuwa wapo baadhi ya wanasiasa watakaokwama kufikia lengo hilo kutokana na kukabiliwa na kesi ndani ya chama, ambazo hakuzitaja wala kutaja wahusika.

"Kuna watakaopungua kutokana na kesi zinazowakabili katika chama ambazo zinawafanya wapungukiwe sifa. Kwa maana hiyo kuna watu kama wanne hivi (wa Bara) unawatoa na ukiwatoa unabakiwa na watatu, sasa unaweza kujiuliza hao watakaobaki watatu, je, wanatosha?"

Hii nchi ya ajabu kweli! Baada ya baba wa taifa kuondoka na ni kweli ameondoka na kila kitu. Kumbuka kuwa alisema kati ya speeches zake za mwisho '' hatutawachagua watu wasiofuata utaratibu uliowekwa na katiba na ambao hawako tayari kuilinda katiba ya nchi yetu'' sasa niambie eti mtoto wa Kikwete anakuja kutuambie nani wanaweza kuongoza nchi hii. It is ridiculous!!! Aende akaongoze kule Chalinze ambao watoto hawana mahali pa kukaa wakiwa madarasani!!
 
“Matamanio yangu ni kumwona rais atakayefuata awe mtu mwenye uwezo wa kuendeleza pale Bwana Jakaya Kikwete alipoachia. Siyo rafiki yangu, mchumba wangu wala si mshikaji wangu wala mshiriki wangu katika baishara. La msingi ni mtu ambaye anaweza.”

Hivi umri wa kugombea kiti cha urais wa JMT si ni miaka 40 na kuendelea...

Huu mfano wa uchumba unatokea wapi kwa kijana wa miaka 35?

Au ndio kusema huwa anatoka na mijimama iliyomzidi umri!!!
 
Naomba kuuliza. Huyu dogo ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM? Najua ni MNEC. Lakini je anayo fursa ya kufanya maamuzi kama member wa CC? Again asking the wrong person expecting the "correct" answer by Mwananchi Newspaper.
 
huyu kilaza nae!! na 2015 hata ubunge wa chalinze hashindi. rais ajaye ni dr SLAA acha kutaja mizoga
 
Huyu anajaribu kuwa mnafiki kotekote ili baba yake akirudi kulima rais ajaye aweze kumbeba kisiasa
Kwa maelezo yake lowassa kamtaja kiwoga tu maana hajui kitakacho tokea
Ila watu wake na baba yake ni membe,ngeleja,mingiro hawa wakichukua nchi hii lazima wampatie riz zawadi ya uwaziri,bado hizi naziona ni siasa maji taka!
 
Ridhiwani mbona hujawataja Magufuli, sitta, sumaye wana bifu na baba yako? au wata mkosoa wakiwa maraisi???
 
akafiye zake huko ataje warithi wa utajili wa baba yake na wa kwake.
Mkuu salute. Unajua hili jamaa najiuliza baba yake akitoka pale atakuwa na hali gani? Sasa hivi anajifanya yeye kama vile msemaji mkuu wa maintarahamwe mpaka alifikia kusema eti Rais hawezi kutoka kaskazini.
kwanza ajiulize baba yake alikuwa na sifa zinazotakiwa? Mbona baada ya yeye kila mtu anadhani anaweza kupewa hiyo nafasi? Jee sio sababu kwamba baba yake ameidhalilisha hiyo nafasi?
 
Jamani mbona Hajamtaja mtu Ambae anatarajiwa kuwa ndio kiongizi msafi asie na makundi,ambae watu wengi wanatajia kuwa ndio atakuwa mrithi wa kikwete ambae ni Mh waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda.
 
Back
Top Bottom