Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amekemea tabia ya baadhi ya maafisa rasilimali watu (Human Resources) kuwachongea watumishi wa umma wanapohamia taasisi nyingine kwa kutoa taarifa hasi zisizo za kitaaluma.
Akizungumza Juni 1, 2026 jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha viongozi wa utawala na usimamizi wa rasilimali watu serikalini, amesema mwenendo huo unakiuka maadili ya utumishi wa umma na unapaswa kukomeshwa.