Ridhiwani Kikwete: Maafisa Utumishi acheni kuwa miungu watu

Ridhiwani Kikwete: Maafisa Utumishi acheni kuwa miungu watu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amewaagiza Maafisa Utumishi wa Halmashauri zote nchini kuacha tabia ya kukaa ofisini badala yake watembelee ofisi za watumishi zilizopo katika Kata na Vijiji ili kutatua changamoto za watumishi.

Aidha, Kikwete amepiga marufuku tabia ya baadhi ya maafisa utumishiukutoa vibali vya kusafiri kwa watumishi kwenda Jijini Dodoma katika Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa ajili ya kufuatilia masuala yao binafsi ya kiutumishi ilihali kazi hiyo ni ya Maafisa Utumishi hao.

"Acheni ile tabia ya kuonekana miungu watu, tatueni matatizo ya watumishi" amesisitiza Mhe. Kikwete.

Amesema watumishi hao hufika Dodoma kwa ajili ya kufuatilia kupandishwa madaraja, kubadilishiwa miundo na kada, kudai malimbikizo ya mshahara, kuwa vitendo hivyo vinawanyima fursa wananchi kuhudumiwa na watumishi hao waliolazimika kusafiri.

Mhe. Kikwete ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda, ikiwa ni siku yake ya tatu ya ziara anayoendelea kufanya mkoani Mara ambapo amewataka Maafisa Utumishi hao kuleta matumaini kwa Watumishi wenzao.

Chanzo: EATV
 
Hivi hii nchi ni mali ya kina Kikwete !.
 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amewaagiza Maafisa Utumishi wa Halmashauri zote nchini kuacha tabia ya kukaa ofisini badala yake watembelee ofisi za watumishi zilizopo katika Kata na Vijiji ili kutatua changamoto za watumishi...
We muhaya bado upo?

Tangu Magufuli atuage umekuwa kimya sana.
 
Wanoko wengi wakishastaafu maisha uwapiga sana mtaani.

Pana mmoja alikuwa mnoko akastaafu akalipwa milioni 320 Leo anakaanga chips mbagala,pesa zimeisha.
Wanoko mtaani elimu tosha
Milioni 300 umri wa miaka 60 unaimalizaje mpaka uwe choka mbaya! Au alihonga?
 
Hivi huyo naibu waziri hajui kwamba watumishi wanaamua kufika huko wizara ya utumishi na utawala bora kufuatilia malimbikizo yao kwa sababu hao maafisa utumishi hawana majibu ya uhakika kuhusu ni kwa nini madai ya watumishi hayalipwa licha ya kupelekwa huko miaka mingi.Hakuna mtumishi ambaye anaweza ridhika na jibu toka kwa afisa utumishi la kusema madai yako sisi tulishapeleka ila hatujui kwa nini hulipwi au utalipwa lini!Muhimu naibu waziri apush madai yote yaliyohakikiwa yalipwe kuliko kuwapiga biti hao maafisa utumishi.Lasivyo ajiandae kupokea ugeni huko wizarani hasa manesi maveo na walimu wetu
 
Back
Top Bottom