Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Agosti 12, 2024 jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete alisema kuwa serikali imeratibu na kusimamia miradi ya kimkakati ikiwemo kutengeneza ajira, kupanua masoko na kutoa mikopo kwa vijana ilimkutatua tatizo la ajira nchini
Your browser is not able to display this video.
Amesema "Mwaka 2023/2024, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana umetoa mikopo yenye thamani ya bilioni 1.2 kwa miradi 57 ya vijana."
Pia, amesema ”Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika mwaka wa Fedha 2024/2025 imetenga fedha ya Tsh. bilioni 7.3 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na kuwakopesha vijana [wa programu ya BBT] wanaofanya kazi katika maeneo hayo punde wanapohitimu mafunzo ili kuwawezesha kujiajiri."