Ridhiwani: Serikali ya Rais Samia itaendelea kupima ardhi ili kupambana na migogoro ya ardhi

Ridhiwani: Serikali ya Rais Samia itaendelea kupima ardhi ili kupambana na migogoro ya ardhi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
RIDHIWANI: SERIKALI YA RAIS SAMIA ITAENDELEA KUPIMA ARDHI ILI KUPAMBANA NA MIGOGORO YA ARDHI.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kupima Ardhi kila sehemu Nchi nzima ili kupambana na migogoro ya Ardhi.

Mhe. Ridhiwani ameyasema hayo kwenye ziara ya Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Philip Mpango aliyeko kwenye ziara Mkoani Katavi.

"Katika kulinda Milki za Maeneo ya Huduma za Jamii, Serikali ya Awamu ya Sita imeelekeza na tunaendelea kuhakikisha maeneo yote yamepimwa na kutolewa Hati Milki."

Kwenye ziara hiyo, Makamu wa Rais JMT amekabidhi hati ya Kituo Cha Afya Nsemulwa, Manispaa ya Mpanda.

#KaziInaendelea
IMG-20220722-WA0030.jpg
IMG-20220722-WA0031.jpg

 
Back
Top Bottom