GE2025 Ridhiwani: Zaidi ya watu 1,200 wenye ulemavu wameajiriwa Serikalini

GE2025 Ridhiwani: Zaidi ya watu 1,200 wenye ulemavu wameajiriwa Serikalini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema serikali ya awamu ya Sita imefanikiwa kufungua milango ya ajira kwa watu wenye ulemavu ambapo zaidi ya watu 1,213 wameajiriwa katika taasisi mbalimbali za umma

Amesema ajira hizo zimepatikana katika kada mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, Uhasibu, Ustawi wa Jamii, Lishe na Maendeleo ya Jamii, jambo linaloashiria hatua kubwa ya usawa katika upatikanaji wa ajira kwa watu wenye ulemavu

Soma pia: Majaliwa: Rais Dkt. Samia yupo tayari kufanya mambo makubwa kwa wenye ulemavu


Mhe. Ridhiwani ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kupokea tuzo ya shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliyotolewa na Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope, kama ishara ya kutambua mchango wake katika kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu nchini

Amesema utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. Samia umeendelea kuleta matokeo chanya, ikiwemo uwekezaji katika mikopo ya asilimia 10, ambapo hadi sasa zaidi ya shilingi bilioni 16.4 zimetolewa kwa vikundi mbalimbali pamoja na watu binafsi wenye ulemavu

“Haya yote niliyoyaeleza yanadhihirisha wazi kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi wa kipekee anayejali maslahi ya watu wenye ulemavu. Nataka niwahakikishie kuwa huu ni mwanzo tu — katika miaka mitano ijayo, mafanikio yatakuwa makubwa zaidi,” amesema Ridhiwani
 
Back
Top Bottom