- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu Salaam,
Nimekutana na na barua ambayo inasambaa mtandaoni ambayo inaonekana kama imeandikwa na Naibu wa Rais wa Kenya ikiwa na dhumuni la kujiudhulu, je kuna uhalisia wowote juu ya suala hili?
Nimekutana na na barua ambayo inasambaa mtandaoni ambayo inaonekana kama imeandikwa na Naibu wa Rais wa Kenya ikiwa na dhumuni la kujiudhulu, je kuna uhalisia wowote juu ya suala hili?
- Tunachokijua
- Tovuti rasmi ya naibu wa Rais wa Kenya inaeleza kuwa Rigathi Gachagua mhitimu wa chuo kikuu cha Nairobi mwaka 1988, ni Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya ambaye alichaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Rais William Rutto kupitia tiketi ya chama cha United Democratic Party (UDA) na kushinda uchaguzi uliofanyika mwezi agosti 9 2022 hatimaye kuapishwa mnamo september 13, 2022.
Kabla ya kuwa naibu wa Rais Rigathi Gachagua alihudumu kama mbunge wa Mathira katika kaunti ya Nyeri kuanzia mwaka 2017 mpaka mwaka 2022 alipochaguliwa kuwa naibu wa Rais wa Kenya.
Kutokana na madai yaliyoibuliwa dhidi ya Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ikidaiwa mienendo yake inakiuka maadili ya uongozi, siku ya tarehe 07 Oktoba alionekana akimuomba radhi Rais wa Kenya William Rutto akimsihi amsamehe endapo kama ailimkosea kwa namna yoyote.
Hivi karibuni bunge la Kenya lilipitisha uamuzi wa kumuondoa madarakani Naibu wa Rais Rigathi Gachagua baada ya kuwasilishwa kwa madai 11 yanayomshutumu Naibu wa Rais huyo na mnamo Oktoba 09 wabunge 282 walipiga kura ya ndiyo huku 44 wakipinga uamuzi huo na kura moja ikiwa haina upande wowote.
Kumekuwepo na barua ambayo imekuwa ikisambaa mtandaoni ambayo inadaiwa kuwa imeandikwa na Naibu wa Rais Rigathi Gachagua kuwa amejiuzulu nafasi yake ya Naibu wa Rais nchini humo.
Je uhalisia wa barua hiyo upoje?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa barua hiyo si ya kweli kwani haijatolewa kutoka ofisi ya naibu wa Rais nchini Kenya, wala chanzo cha kuaminika kutoka serikali ya Kenya. Aidha hakuna chombo cha habari kutoka nchini Kenya ambacho kimeripoti juu ya taarifa hiyo.
Kadhalika JamiiCheck imebaini mapungufu kadhaa katika barua hiyo ikiwemo kutokusainiwa kwa barua hiyo na mhusika ambaye ni Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua, vilevile barua hiyo imetumia mwandiko (fonts) ambao ni tofauti na mwandiko maalumu ambao unatumiwa na ofisi ya naibu wa Rais nchini kenya.
Hata hivyo JamiiCheck ilichunguza maandishi ya Barua hiyo kwa kutumia GPTZero ili kufahamu kama maandishi hayo yaliandikwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba ilionesha kuwa asilimia 76% imeandikwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba (AI)
Barua hiyo imechapishwa hapa na hapa