Rigathi Gachagua huwa akihitubia anachekesha sana

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Wakuu,

Leo Ikulu ya Kenya imeandaa iftar sasa kama kawaida hotuba za viongozi, Riggy G baada ya salamu kasema kwanza amefurahi kufika kwenye sherehe ile, yaani iftar kwake ni sherehe tayari.

Ukisikia anasema hii mzee ya maandamano ujue anamsema Raila.

Ukisikia anasema hii mutu ya cerelac ujue anamsema Uhuru kuwa ni muoga kalelewa na vyakula vya kizungu tu.

Ngoja niendelee kuandika vituko vyake kila nikipata nafasi.
 
Yaani ukifuatilia hotuba zake utajua tu kenya wamepatwa kwanza alimtukana Rais Mstaafu siku ile ile wanaapishwa mbele ya wageni wa kitaifa na kimataifa
Ni kama alikuwa haamini amefikaje pale.Na anaonesha alikuwa ana chuki na familia ya Kenyatta/matajiri/watu wenye madaraka kabla ya kuyapata aliyonayo sasa.Na yeye ajiandae kupata maadui.Watu sampuli yake hawafai.Wamejaza nafsi zao visasi,visirani na mihemko.
 
Wakuu,

Leo ikulu ya Kenya imeandaa iftar sasa kama kawaida hotuba za viongozi, Riggy G baada ya salamu kasema kwanza amefurahi kufika kwenye sherehe ile, yaani iftar kwake ni sherehe tayari.

Ukisikia anasema hii mzee ya maandamano ujue anamsema Raila.

Ukisikia anasema hii mutu ya cerelac ujue anamsema uhuru kua ni muoga kalelewa na vyakula vya kizungu tu.

Ngoja niendelee kuandika vituko vyake kila nikipata nafasi.
mutu ya cerelac [emoji23]
 
Ni kama alikuwa haamini amefikaje pale.Na anaonesha alikuwa ana chuki na familia ya Kenyatta/matajiri/watu wenye madaraka kabla ya kuyapata aliyonayo sasa.Na yeye ajiandae kupata maadui.Watu sampuli yake hawafai.Wamejaza nafsi zao visasi,visirani na mihemko.

Kenyatta family ni wakikuyu lakini watoto wa mjini, ujue kwa sasa ilipo ikulu ya kenya jirani yaani wanapeana fence tu ndio nyumbani kwa kenyatta , halafu Riggy G sio kiongozi mzuri sana kama wengi walivodhani,
 
Mtu mzima,siku ya kwanza madarakani akaanza kumu-attack mstaafu.Hiyo ni hekima kweli?Mwenzie kakulia ikulu kutokana na jasho la baba yake.Angekataa maisha ya ikulu?Kama yeye alichoka kula ugali wa mtama au githeri kwa sukuma ni matokeo ya maandalizi ya wazazi wake.Asione umasikini wake kama credit kwa wapiga kura.Bure yule Gachagua.
 
mutu ya cerelac [emoji23]

IMG_1372.jpg

IMG_1370.jpg

Anakueleza Uhuru ni muogamuoga alitishiwa na Muzee ya maandamano akakubali sababu kakuzwa na hayo madude ya wazungu,
 
Halafu majuzi Ruto alitaka wakae wazungumze na Raila jamaa katia ngumu kishingo upande Ruto amebadili kauli wakati anaendeshwa na Naibu wake
 
View attachment 2584737
View attachment 2584742
Anakueleza Uhuru ni muogamuoga alitishiwa na Muzee ya maandamano akakubali sababu kakuzwa na hayo madude ya wazungu,
Hana lolote huyo.Mbona yeye na bosi wake Ruto,at last,wamekubali matakwa ya Muzee na kuomba pooh maandamano yasitishwe.Ujicheleweshe au uitike matakwa ya mkinzani mapema,mambo ni yaleyale tu.Halafu,asijisahaulishe.Wafanyakazi wanadai mishahara yao.
 
Mtu mzima,siku ya kwanza madarakani akaanza kumu-attack mstaafu.Hiyo ni hekima kweli?Mwenzie kakulia ikulu kutokana na jasho la baba yake.Angekataa maisha ya ikulu?Kama yeye alichoka kula ugali wa mtama au githeri kwa sukuma ni matokeo ya maandalizi ya wazazi wake.Asione umasikini wake kama credit kwa wapiga kura.Bure yule Gachagua.

IMG_1375.jpg

Hapo ni Rais Kenyatta senior, amekaa pembeni na dogo uhuru, halafu aliyeinama ni kibaki huyo aliesiamama kwa kunyooka ni mzee moi a.k.a nyayo, baadae Moi akawa Rais hapo baada ya jommo kenyatta, halafu Kibaki akaja akawa Rais, baadae yule dogo aliekaa na Baba yake hapo nae kawa Rais kwahiyo hiyo picha ilitabiri marais wanne wa kenya,
 
View attachment 2584746

Sasa picha kama hizo huyo Gachagua ndiyo zilikuwa zinampa hallucinations maishani.
 
Uongozi wa kenya wa sasa unachukuliwa kama uongozi wa watu washamba, watu wa porini, sasa watoto wa mjini akina Raila na uhuru wanawachezesha wanavotaka yaani wakiamka leo wakijisikia ni maandamano basi wanakiwasha tu,
 
Siasa za Kenya ngumu sana

Ni ngumu kupita kiasi, sema Ruto alichosafanyia akina Uhuru hawakuamini walikuja kustuka dakika za mwisho, Chebukati ni shemeji wa wetangula ambae ni spika wa bunge la kitaifa, halafu CJ koome na mke wa Ruto wanaundugu hivi kwahiyo mambo yakaharibika hapo, umafia waliofanyiwa pamoja na kua walikua na dola hawakuamini
 
Uongozi wa kenya wa sasa unachukuliwa kama uongozi wa watu washamba, watu wa porini, sasa watoto wa mjini akina Raila na uhuru wanawachezesha wanavotaka yaani wakiamka leo wakijisikia ni maandamano basi wanakiwasha tu,
Na hapo ndipo waliopo madarakani wanapaswa kuwa makini.Watachezewa akili kwa kutengenezewa changamoto kwa mikono yao wenyewe.
 
Back
Top Bottom