Rigobert Song alazwa hospitalini Cameroon

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Nyota wa zamani wa Liverpool na West Ham Rigobert Song amekimbizwa hospitalini akiwa katika hali mahututi baada ya kuugua kiharusi.

etoo.jpg

Ujumbe wa Samuel Etoo katika ukurasa wake wa Instagram "Namtakia ndugu yangu mkubwa ujasiri na uponaji wa haraka," ameandika kwenye Twitter na Instagram".

Song, 40, ambaye ni mjomba wa aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, West Ham na Charlton Athletic Alex Song, alichezea timu ya taifa ya Cameroon mechi 137.

Taarifa zinasema alikuwa nyumbani kwake Odza, Yaounde alipopatwa na kiharusi na akakimbizwa hospitalini siku ya Jumapili.

Song, ambaye alikuwa nahodha wa Indomitable Lions, ndiye kocha mkuu wa timu ya taifa ya Chad, kazi aliyokabidhiwa mwishoni mwa mwaka jana.

Ndiye mchezaji aliyechezea timu ya taifa ya Cameroon mechi nyingi zaidi.

Wachezaji wengine nyota wa Cameroon, akiwemo Samuel Eto'oo, wamemtakia afueni ya haraka.

"Namtakia ndugu yangu mkubwa ujasiri na uponaji wa haraka," ameandika kwenye Twitter na Instagram.

Song alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa dhidi ya Mexico mwaka 1993 na alikuwa nahodha wa Cameroon kwa miaka 10 tangu Eto'o alipochukua majukumu hayo 2009.

Alistaafu soka ya kimataifa 2010 baada ya kucheza Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

Chanzo: BBC
 
View attachment 411309

Asee huyo jamaa namkumbuka sana kakimbiza kombe la dunia mwaka 1998!!kipindi hicho yeye pateick mbona akina vieira wakati huo camerooo ilikimbiza mbaya[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Mtanisamehe kama swali langu la kijinga,hivi kiharusi kina uhusiano na ugonjwa wa moyo?
Nauliza hivyo kwa sababu taarifa nilizo nazo ni kuwa Song alipatwa na stroke ya kichwa(brain aneurysm) ambayo husababisha damu kuvuja kwenye ubongo.
Ni mbaya sana,namuombea kwa Mungu apone maana hii kitu ni mbaya mno,ukipona shukuru Mungu.
 
Back
Top Bottom